Nahitaji mtu anayeweza kuwekeza kwenye biashara yangu

Khaleid

New Member
Nov 7, 2023
4
8
Salaam wana jamii forums kwa majina naitwa Khalid Munir mkazi wa Dar mwenye umri wa miaka 31.

Elimu yangu ni kidato cha 3 sikufanikiwa kumaliza Elimu sababu ya maradhi.

Nimekuja ktk jukwaa hili kuomba msaada mnamo mwaka 2020 nilipokea mgeni toka Sudan kupitia rafiki yangu mtu huyu alikuja tafuta fursa ya kibiashara nilimuonesha na kabla ya kuondoka niliwashauri tusajili kampuni wakakubali kwa makubaliano ya kuwa mimi nasajil kampuni wao wataweka pesa ya mtaji.

Baada ya hapo waliondoka na mimi nikaendelea na mchakato nlipomaliza niliwajuza na Msudan aliniuliza nini nahitaji kufanya nkamwambia biashara ya vitambaa alinitumia sample na price ila biashara ili shindikana aliponihitaji nitoe 30'/.

Kama mchango baada ya hapo aliniunga na kampuni kubwa toka Turkey inayo jihusisha Power plants, Refinery, Solution technology, Prefabricated house and steel structure, kazi zote za ujenzi na Vifaa vyote vya ulinzi na usalama nimekuwa nazungumza nao toka 2021 mpaka sasa hatujafikia muafaka ila baada ya muda alinipa taarifa za watu tofauti.

Wapo walohitaji kuwekeza katika madawa ya binadam, mafuta ya kula na petrol vipodozi nk na mwaka huu mwez June aliniunga na mtu alikuwa anahitaj kununua madini ya Gold na copper cathode zaidi ya 80 tani gold ikiwa 36 tons na 45 ya copper huyu mtu alikuwa seriously alifika mpaka hapa Tanzania ila bahati mbaya biashara ili shindikana.

Baada ya jambo hili jamaa yangu msudan alinambia kaunda group la wafanya biashara na wako tayar kushiriki nasi kufanya biashara ila swala hili lime fail pia na hivi karibuni aliniunga na watu 2 mmoja anahitaji soko la mbolea mwingine anahitaj kununua maembe nanasi na Avocado kontena 10-15.

Kwa kila matunda kwa mwezi ndani ya mwaka kazi hizi pia zimeshindikana na sababu kubwa ya kushindwa sina pesa ya mtaji nimezunguka sehem tofauti mpaka ktk taasisi za serikali lakini jitihada zangu zimefeli nilihitaj kufika mpaka ikulu kwenda muona mh Rais ila sikupewa ushirikiano zaid ya kukatishwa tamaa.

Nilijaribu kumpigia simu wazir Ashatu kijaji alinambia natakiwa nianzishe biashara ndo naweza saidiwa au niingie ktk kundi la watu 5 ili kupatiwa mtaji mambo yame kuwa ni mengi sana.

Nimekuja hapa katika jukwaa kuomba msaada kama kuna yeyote anaweza nisaidia akawekeza katika kampuni yangu au kama kuna shirika lolote linaweza kuguswa na jambo langu wakanisaidia kutimiza malengo yangu kwani nahitaji kuwa mfanyabiashara mkubwa na lengo ni kushirikiana na serikali ktk kuliletea taifa na jamii maendeleo.
 
Mdogo wangu kuna kitu kimoja nimegundua kutoka kwako na nimeshakusoma ni mtu wa aina gani maana nilishakutana na watu mbalimbali pamoja na marafiki wenye hulka kama yako.
1.Wewe ni mtu mwenye kiherehere au mwenye pupa kwa lugha nyepesi.
Sababu ya kusema hivi ni kwamba unaonekana hujawahi kufanya biashara ya aina yoyote hata ya kiosk umerukia kuanzisha kampuni na hujui unauza nini kwenye hiyo kampuni
2.Una mihemko ya kuingia kichwakichwa kwa watu usiowajua vizuri kwa sababu ya kusikiliza maneno yao mazuri yanakudatisha na kudhani umeshaingia kwenye mafanikio au fursa bila ya kujua kuwa wewe ndio unaandaliwa kufanywa fursa.
3.Ni mtu hauko flexible yaani upo stagnant,baada ya wazo lako kufail karibia mara 3 bado unalazimisha tu badala ya kujiongeza na kuachana nalo utafute mambo mengine ya kufanya lakini bado unalazimisha hadi unakwenda kwenye ofisi ya Rais na mawaziri.
4.Unaonekana pia ni aina ya watu wasioshaurika ambao ukisetiwa kiakili ni ngumu sana mtu kukuvumbua hadi utakapotapeliwa ndio akili inarudi.
5.Mwisho nikupe maoni tu achana na hilo jambo unaloliwaza utakuja uingie kwenye deni kubwa sana ambalo hutaweza kulilipa.
Msudan ana uwezo wowote wa kukusaidia wewe na wenyewe ni maskini tu kama unavyojiona wewe hawana utofauti ndugu.
Na ukija kwa watu wa Asia ni wabahili balaa hela zao hawatumii kizembe bora hata mswahili anatumia pesa kuliko wa Asia wewe fikiria hata wakienda bar wananunua chupa moja ya kinywaji wanakunywa familia nzima ndio watakupa hela wewe wasiyekujua ufungue mradi wako.
Funguka kijana maisha sio rahisi kihivyo.
 
Salaam wana jamii forums kwa majina naitwa Khalid Munir mkazi wa Dar mwenye umri wa miaka 31.

Elimu yangu ni kidato cha 3 sikufanikiwa kumaliza Elimu sababu ya maradhi.

Nimekuja ktk jukwaa hili kuomba msaada mnamo mwaka 2020 nilipokea mgeni toka Sudan kupitia rafiki yangu mtu huyu alikuja tafuta fursa ya kibiashara nilimuonesha na kabla ya kuondoka niliwashauri tusajili kampuni wakakubali kwa makubaliano ya kuwa mimi nasajil kampuni wao wataweka pesa ya mtaji.

Baada ya hapo waliondoka na mimi nikaendelea na mchakato nlipomaliza niliwajuza na Msudan aliniuliza nini nahitaji kufanya nkamwambia biashara ya vitambaa alinitumia sample na price ila biashara ili shindikana aliponihitaji nitoe 30'/.

Kama mchango baada ya hapo aliniunga na kampuni kubwa toka Turkey inayo jihusisha Power plants, Refinery, Solution technology, Prefabricated house and steel structure, kazi zote za ujenzi na Vifaa vyote vya ulinzi na usalama nimekuwa nazungumza nao toka 2021 mpaka sasa hatujafikia muafaka ila baada ya muda alinipa taarifa za watu tofauti.

Wapo walohitaji kuwekeza katika madawa ya binadam, mafuta ya kula na petrol vipodozi nk na mwaka huu mwez June aliniunga na mtu alikuwa anahitaj kununua madini ya Gold na copper cathode zaidi ya 80 tani gold ikiwa 36 tons na 45 ya copper huyu mtu alikuwa seriously alifika mpaka hapa Tanzania ila bahati mbaya biashara ili shindikana.

Baada ya jambo hili jamaa yangu msudan alinambia kaunda group la wafanya biashara na wako tayar kushiriki nasi kufanya biashara ila swala hili lime fail pia na hivi karibuni aliniunga na watu 2 mmoja anahitaji soko la mbolea mwingine anahitaj kununua maembe nanasi na Avocado kontena 10-15.

Kwa kila matunda kwa mwezi ndani ya mwaka kazi hizi pia zimeshindikana na sababu kubwa ya kushindwa sina pesa ya mtaji nimezunguka sehem tofauti mpaka ktk taasisi za serikali lakini jitihada zangu zimefeli nilihitaj kufika mpaka ikulu kwenda muona mh Rais ila sikupewa ushirikiano zaid ya kukatishwa tamaa.

Nilijaribu kumpigia simu wazir Ashatu kijaji alinambia natakiwa nianzishe biashara ndo naweza saidiwa au niingie ktk kundi la watu 5 ili kupatiwa mtaji mambo yame kuwa ni mengi sana.

Nimekuja hapa katika jukwaa kuomba msaada kama kuna yeyote anaweza nisaidia akawekeza katika kampuni yangu au kama kuna shirika lolote linaweza kuguswa na jambo langu wakanisaidia kutimiza malengo yangu kwani nahitaji kuwa mfanyabiashara mkubwa na lengo ni kushirikiana na serikali ktk kuliletea taifa na jamii maendeleo.
Hi umesoma ulichokoandika? Uko all over the place na hakuna ulichosema umefanikiwa. Hujua hata biashara gani unataka kufanya. Msudan anakuundanisha tu kwa watu. Kuna jambo linapikwa
 
Back
Top Bottom