Nahitaji msaada ndugu zangu kwenye kupata Hati ya kusafiria

Jicholamwewe

JF-Expert Member
Jan 2, 2021
375
460
Nina ndoto za kusoma nje, nilifanikiwa kupata chuo na scholarship lakini napata changamoto nimekosa passport yaani nimenyimwa sababu mzazi alishindwa kujieleza yaani alipishana kauli na Afisa uhamiaji.

Sasa nimepeleka documents zote na barua ambayo nimetumiwa na chuo ili wanisaidie hata passport ya miaka 5 lakini wamegoma kunipa.

Ndugu zangu naombeni msaada hata mawazo sababu nimejaribu kuomba wanisaidie lakini bado.
 
Umeombea wapi passport hiyo? I mean mkoa gani au makao makuu Dsm?
 
Nina ndoto za kusoma nje, nilifanikiwa kupata chuo na scholarship lakini napata changamoto nimekosa passport yaani nimenyimwa sababu mzazi alishindwa kujieleza yaani alipishana kauli na Afisa uhamiaji.

Sasa nimepeleka documents zote na barua ambayo nimetumiwa na chuo ili wanisaidie hata passport ya miaka 5 lakini wamegoma kunipa.

Ndugu zangu naombeni msaada hata mawazo sababu nimejaribu kuomba wanisaidie lakini bado.
Nitafute
 
Hilo la mzazi kupishana kauli na ofisa halina sana mashiko. Hujasema kinaga ubaga kwa nini mzazi alikwama.

Uraia wako ukoje, first and foremost.

Mzazi akueleze ukweli kama kuna uzembe ulifanyika kuhusu nyaraka zako na zake za uzao, majina, ubini , elimu, kughusi taarifa zozote za nyuma na mmetokea pori gani, liko nchi gani.

La mwisho, wanasema uhamiaji ni wala rushwa, lakini kwa experience yangu, pamoja na ula rushwa wao, wao wako makini sana na kazi zao kuliko NIDA, RITA, NECTA na TRA wanakotoa leseni za kuendeshea. Kwa hiyo ukienda Uhamiaji na makaratasi fyongo kutoka taasisi zingine Uhamiaji wanatambua mara moja uozo wa kilichomo humo. Watakwambia pa kurudi kurekebisha halafu wataomba cha juu kulishughulikia jambo lako utakapowarudia.
 
Wewe chalii umeleta maelezo marefu watu wanakuuliza maswali unawwjibu shoti shoti. Yani kama ndio mnajibu hivi si ajabu kunyimwa Passport. Na mkifika kwenye interview ya VISA hamtoboi kwa mtindo huu.
 
Nina ndoto za kusoma nje, nilifanikiwa kupata chuo na scholarship lakini napata changamoto nimekosa passport yaani nimenyimwa sababu mzazi alishindwa kujieleza yaani alipishana kauli na Afisa uhamiaji.

Sasa nimepeleka documents zote na barua ambayo nimetumiwa na chuo ili wanisaidie hata passport ya miaka 5 lakini wamegoma kunipa.

Ndugu zangu naombeni msaada hata mawazo sababu nimejaribu kuomba wanisaidie lakini bado.
Ata kujieleza hujui, alafu unalalamikia migration
 
Hiyo ni haki yako wala siyo msaada, naona unasisitiza kusaidiwa...lazima kuna mahali utakuwa na shida wewe sio bure!
 
Una uhakika unayo makaratasi yote yanayohitajika au unakuja kulalamika tu?
 
Back
Top Bottom