Nafuu kumsaidia hawara vyakula kuliko kumnunulia bia demu wa baa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,715
45,177
Siku zote wanaume wameendelea kuwa madaraja yaani wao pesa yao wakiishika inapitiliza kwenda na hasa kwa wanawake.

Ila katika haya makundi mawili bora yule ambaye ni mtu mzima anayejielewa yeye hamalizi pesa kwenye pombe, akishakunywa bia zake tano hana shobo yeye, ana mademu zake wasio kunywa pombe anachofanya anaponunua misosi ya kwake anawachukulia na mademu zake misosi, mahindi, maembe, nyama, nazi, samaki n.k.

Chakula hicho kinakwenda kusaidia familia yote ya mwanamke unakuta mpaka mama wa binti hana kelele wadogo zake binti wanatulia huezi kujua pengine wangelala njaa.

Shida ipo kwa vijana ana hela nyingi na yote inaishia bar Juliana au Kitambaa Cheupe eti kisa kashobokea mademu anawanunulia pombe na mademu wengine wajanja hawanywi wanarudishiwa hela.

Unatumia laki moja halafu unalewa hata demu uliyemnunulia pombe huondoki naye taabu tupu.

Nawasihi tutafuteni mademu wa kitaa wasiokunywa tuwasaidie hata vyakula tu ukiona kumuhonga cash roho inauma.
 
Ndege John hao ma barmaid watakuja kukufilisi

Wakuroge hata usikumbuke yule mkeo
 
Ishawahi nitokea nanunua bia halafu kale kakenge kumbe kalikuwa hakanywi ila dj ni Mwanangu akaja kunisanua.

Asubuhi ndio nakumbuka nimekata 250K wakati nilipanga nitumie 20k.
 
Back
Top Bottom