Nafasi za kazi 90 kwenye Taasisi ya Benjamin William Mkapa

Ally Msangi

JF-Expert Member
Jun 29, 2010
608
120
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Taasisi ya
Benjamin William Mkapa, inatekeleza Mradi wa Kuimarisha Mifumo Endelevu ya Afya
(RSSH) kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na
Malaria (Global Fund).

Mradi huu una lengo la kuimarisha huduma za afya ngazi za vituo katika mikoa kumi (10)
iliyopewa kipaumbele na mradi huu ambayo ni; Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Geita,
Kagera, Katavi, Tabora, Dodoma na Kigoma. Kupitia mradi huu, jumla ya wataalamu 281
wamepangwa kuajiriwa kwa kipindi cha mwaka 2018 – 2020 na kupangiwa kufanya kazi
ndani ya mikoa tajwa hapo juu.

Ili kukamilisha ujazaji wa nafasi za wataalamu zilizobakia wazi, Taasisi ya Mkapa inapenda
kutangaza nafasi wazi 90 za wataalamu wa afya. Nafasi hizi ni kwa ajili ya wataalamu
waliosomea fani za: -


1. Udaktari nafasi (Nafasi18)
2. Afisa teknolojia Maabara (Nafasi 4).
3. Afisa Tabibu (Nafasi 1)
4. Wateknolojia wasaidizi dawa (Nafasi 34)
5. Wateknolojia wasaidizi mionzi (Nafasi 21)
6. Wateknolojia wasaidizi Maabara (Nafasi 2)
7. Wateknolojia Mionzi (Nafasi 2)
8. Wauguzi nafasi (Nafasi 7)
9. Afisa Muuguzi Msaidizi (Nafasi 1)


Sifa za waombaji;
1. Waliohitimu mafunzo kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali.
2. Wataalamu wenye vyeti kamili vya mafunzo ya fani walizosomea.
3. Wataalamu wenye leseni hai kutoka katika mamlaka za usajili kwa fani zinazotakiwa
kufanya usajili kabla ya kuanza kufanya kazi.
4. Mtanzania mwenye umri chini ya Miaka 45.
5. Wataalamu ambao wameajiriwa katika ajira za serikali na za kidini, hawatakiwi
kuomba ajira hizi.


Maombi yote yaambatanishwe na:
1. Barua ya maombi ya kazi ikieleza Mikoa mitatu ambayo muombaji angependa
kupangiwa kufanya kazi katika moja ya Halmashauri zake.
2. Nakala ya cheti cha Taaluma.
3. Cheti cha kidato cha 4 na 6 kama kipo.
4. Picha mbilmli (2) – Passport size na maelezo binafsi (CV), ikionyesha umri, anuani
kamili na namba ya simu ya kiganjani, pamoja na anuani/ namba ya kiganjani ya
wadhamini wako wasiopungua wawili.
5. Nakala zote za vyeti ziwe zimepitishwa na mwanasheria ili kuthibitisha kama ni nakala
halisi ya cheti cha mwombaji.

Maombi yote yatumwe kwa:

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa,
kwa sanduku la Posta 76274
Dar Es Salaam

au kwa barua pepe - recruitment@mkapafoundation.or.tz.

Mwisho wa kupokea maombi ya kazi itakuwa tarehe 28 Februari 2019.

Tangazo hili la kazi linapatikana pia katika tovuti ya Taasisi ya Mkapa:
www.mkapafoundation.or.tz.

NB: Majibu yatatolewa kwa watakaofanikiwa tu.


IMETOLEWA NA
Afisa Mtendaji Mkuu
Taasisi ya Benjamin William Mkapa


Unaweza pata Matangazo mengine mengi ya kazi kwa kufuata link hizi hapa chini:

1. Mechanic at Coca-Cola Kwanza Limited

2. Job Openings at Gaming Board of Tanzania - 11 Posts

3. Job Openings at Gaming Board of Tanzania - 11 Posts

4. Section Leader – Maintenance Planning at Acacia Mining

5.
Director of Internal Oversight
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom