Nafasi 17 za FOREIGN SERVICE OFFICERS zimejaa Rushwa na Upendeleo

the struggle

New Member
Jan 10, 2023
4
6
Mnamo tarehe 2022-08-04 2022-08-17 ,WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI walitangaza nafasi hizo 17 kupitia PSRS Watanzania wenye sifa stahiki waombe ili mwisho wakifaulu hatua zote wamsaidie mama katika Utumishi wa Umma.

Kama ilivyo ada tarehe 29/01/2023 PSRS wakatoa majina ya watu waliofanikiwa kuitwa kwenye written, zaidi ya watu 3000 waliitwa kwenye hii Interview mjini UDOM kwenda kupambania ugali a.ka.a mrija wa Asali.
Mchujo ilikuwa hatua 3(tatu),1. written, 2.Practical 3.Oral.

ukiangalia hiyo Ratiba ya UTUMISHI ni week nzima unatakiwa uwe Dodoma ukipambania 'kombe' na mwishowe kupata ajira, Assume hapo wewe ni jobless unga unga kupata nauli mpaka Dodoma huna kitu si chini ya 150k unachoma kusaka ajira, kwenye kutafuta ajira hii si kitu kama ukipata ajira yenyewe,lakini ajira zenyewe zimekuwa za 'magumashi.'

Habari za ndani kabisa zilizonifikia toka MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS &EAST AFRICA COOPERATION ,nafasi hizo zilizotangazwa watu walishaanza kazi muda mrefu ambapo imezua gumzo kubwa miongoni mwa jobless,wanaharakati na watu wote wapenda haki, iweje uwaite watu Dom uwapigishe Interview huku ikiwa nafasi tayari Vibopa/Vigogo mmepeana wenyewe?

Rai yangu kwako mama Samia Rais wa JMT futa hizo nafasi mchakato uanze upya na ufanye maboresho hapo PSRS wanaita kazi wanakaa miezi 6/9 ndo wanaitisha interview!

Mama Stergomena Tax jitafakari hapo wizarani na watumishi wako baadala ya kumsaidia Rais ninyi mnaendekeza rushwa na upendeleo kwa ndugu zenu,haiwezekani mama unabariki haya yafanyike na wewe ukiona wazi wazi.

Mwisho, Hassan Kitenge hapo utumishi umepoa sana au mama akubadilishie majukumu mengine mnamkwamisha sana mama.Interview mwaka mzima na mpaka sasa watu hawajapangiwa nafasi.mf MDAs LGAs.

TISS taifa limewaamini kwanini hamumsaidii mama mnawasumbua jobless go & return Dom kumbe nafasi mnapeana wenyewe,Rais futa hizo nafasi,UTUMISHI tangazeni upya nafasi hizo mchakato uwe huru na haki, wacheni upendeleo hata watoto wa wawakulima wanahaki ya kuenjoy mema ya Taifa hili.

Screenshot_20230320_120225_Gallery.jpg
Screenshot_20230320_121346_Gallery.jpg
 
Back
Top Bottom