Nadharia 4 kuhusu kisa cha Mdude na dawa za kulevya

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Wiki jana ndugu Mpaluka Saidi Nyagali maarufu kama ‘Mdude Chadema’ alikamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya bila kuwekwa wazi sababu za kukamatwa kwake. Hakupandishwa mahakamani kwa karibu juma zima, na baada ya shinikizo kutoka sehemu mbalimbali polisi wamempeleka mahakamani na kumshtaki kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzani wa gramu 23.4.

Baadae kidogo zikaibuka taarifa mitandaoni kuwa Mdude aliwekewa mtego wa dawa za kulevya na binti aliyekutana nae mtandaoni, wakaanzisha mahusiano na akamtumia kiasi fulani cha fedha.

Kwa sasa mjadala mkubwa si Mdude kudaiwa kukamatwa na dawa za kulevya bali kile kinachoitwa mtego uliotumika kumnasa, yani binti aliyeanzisha nae urafiki. Inawezekana madai haya yakawa kweli au yasiwe kweli. Nitatoa nadharia nne kuhusu kwanini yanaweza yasiwe kweli.

#Mosi; Kwa sisi tunaomfahamu Mdude (watu wake wa karibu) hatujawahi kumuona huyo binti wala kusikia habari zake kutoka kwa Mdude mwenyewe au ndugu zake. Si nyumbani kwa Mdude, kazini kwake au kwenye vijiwe vyetu vya siasa ambapo Mdude amewahi kumzungumzia kwa kudhamiria au kwa bahati mbaya.

Kwahiyo kama walikuwa na mahusiano basi yalikuwa ya SIRI sana na kukutana nao kulikuwa kwa nadra na kwa kificho sana. Lakini kadri nimjuavyo Mdude si rahisi kuanzisha mahusiano na mtu aliyekutana nae mtandaoni kirahisi. Mdude anajua yeye ni ‘target’ ya serikali kwa muda mrefu, kwahiyo hawezi kuingia mtegoni kirahisi hivyo.

#Pili; Mdude si mtuaji wa pombe wala sigara achilia mbali dawa za kulevya. Jamhuri inaweza kumpima ili kuthibitisha hili. Hanywi hata ‘Serengeti lite’. Mdude ni mwanaharakati ‘sobber’ kuliko wengi wetu tunaofanya harakati. Lakini akishika ‘mic’ sisi ndo hujiona ‘sobber’ kwa jinsi anavyoshusha nondo nzito. Sasa jiulize kama hanywi pombe au havuti sigara, hizo kete za ‘heroine’ alikuwa anazifanyia nini? Kupiga nazo picha aweke instagram?

#Tatu; Kwanini polisi imetumia siku 7 kumkamata hadi kumfikisha mahakamani kama kweli alikutwa na kete za heroine? It could be just simple baaada ya kumkamata wangemfikisha mahakamani kesho yake maana ushahidi wanao. Lakini kumkamata mtu bila kumwambia kosa lake, na kukaa nae siku 7 bila kumpeleka mahakamani inaleta ukakasi. Na hata baada ya siku 7 bado mnasita kumpeleka mahakamani hadi mpate shinikizo kutoka kwa jamii?

Je mtu akisema mlimkamata bila kosa, na mlikaa nae siku zote hizo mkijipanga mumpe kosa gani atakuwa anakosea? Scenario za polisi kubambikia watu kesi zipo nyingi sana. Waziri Mkuu Kassim majaliwa aliwahi kueleza kisa cha mfanyabiashara mmoja aliyekataa kutoa rushwa kwa polisi wakambambikiza kesi ya kukutwa na mali za magendo. Bahati nzuri Rais JPM aliingilia kati na kuagiza polisi na maafisa wa TRA waliohusika wafukuzwe kazi na kushtakiwa. Pia aliagiza ofisi ya TRA Ilala imfidie mfanyabiashara huyo.

Si hivyo tu, wakati wa JK wafanyabiashara watatu wa madini ambao ni ndugu kutokea Mahenge mkoani Morogoro waliwahi kukamatwa na kunyang’anywa fedha (milioni 200) na madini waliyokuwa nayo kisha wakauawa na kupakaziwa ujambazi. Tume ya Jaji Kipenka ilibaini baadae kuwa watu hao hawakuwa majambazi.

Visa vya polisi kubambikizia raia kesi ni vingi sana. Hata katika mazingira ya kawaida unaweza kuzozana na askari ukakamatwa na kuwekwa mahabusu lakini kesho yake ukashangaa umepewa kesi ya kukutwa na bangi. Na usipohangaika utapandishwa kizimbani na wataletwa mashahidi "waliokukuta" na bangi, na unaweza kuhukumiwa kifungo, wakati kiuhalisia hujawahi kuiona bangi zaidi ya kwenye TV. Je haiwezi kuwa hivi kwa Mdude pia?

#Nne; Kuna uwezekano waliomkamata Mdude ndio haohao waliotoa taarifa kuwa amewekwa mtegoni na mwanadada ili kuhalalisha mashtaka dhidi yake. Michael Barkun wakati akielezea ‘Conspirancy theory’ alielezea dhana inayoitwa ‘Finite insight’ kwenye Event Conspirancy theory. Kwa kifupi dhana hii inahusisha kula njama za kubuni uongo na kuuvumisha ili uongo huo usaidie kuhalalisha uhalifu mlioufanya. Waswahili husema kujamba na kuwasha feni.

Bado hujanielewa? Ngoja nikupe mfano. Mwaka 1980 Rais Augusto Pinochet wa Chile alimuua mkosoaji wake mmoja Julio Parot baada ya kuilaumu serikali kukiuka haki za binadamu. Parot alidai utawala wa Pinochet hadi mwaka 1980 ulikua umeua zaidi ya watu 200,000 kwa njia mbalimbali, ikiwemo kipigo kikali, shoti ya umeme, kutupwa kwenye bwawa la mamba, kuburuzwa barabarani, kukatwa kiungo kimoja kimoja na njia nyingine za kikatili.

Parot alikamatwa na majasusi wa shirika la ujasusi la nchi hiyo National Intelligence Directorate (DINA) wakati huo likiongozwa na Manuel Contreras. Wakati akihojiwa akapewa mateso makali sana na kufariki dunia. Kwa siku mbili alizokuwa haonekani serikali haikusema kama inamshikilia. Kwahiyo alipokufa mikononi mwa vyombo vya dola ikawa mtihani mgumu.

Kwahiyo wakaipiga maiti yake risasi moja kwenye paji la uso, na kuichoma visu kadhaa tumboni kisha wakaibeba usiku wa manane hadi kwenye mtaa wa Pedro de Valdivia karibu na mto Mapocho na kuitelekeza hapo. Asubuhi polisi wakatoa taarifa kuwa wameokota maiti ya mwanaume mmoja anayesadikiwa kuwa amevamiwa na majambazi na kuuawa. Ikabainika ni Julio Parot.

Polisi ikaagiza msako mkali dhidi ya washukiwa wa uhalifu huo. Hatimaye ‘majambazi feki’ watatu wakakamatwa. Wakapandishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kusababisha mauaji ya Parot. Wakapatikana na hatia na kuhukumiwa kifo. Jamii na familia ya Parot ikaamini haki imetendeka.

Lakini jambo ambalo hawakujua ni kwamba serikali ya Pinochet ndiyo iliyomuua ndugu yao. Na majambazi walioletwa mahakamani walikuwa ni maafisa wa DINA. Na baada ya kuhukumiwa kifo ilitangazwa kuwa wamenyongwa lakini ukweli ni kuwa waliachiwa na kupangiwa kazi zingine nje ya nchi. Miaka 10 baada ya Pinochet kufurushwa madarakani, CIA ndio wakaujua ukweli huu.

Nimeeleza kisa hiki ili uelewe vizuri maana ya ‘Finite insight' tunapozungumzia 'Event conspirancy theory’. Unapokuwa huna taarifa za kutosha kuhusu jambo fulani wahalifu wanaweza kula njama za kubuni uongo na kuuvumisha ili uongo huo usaidie kuhalalisha uhalifu waliofanya.

Kwahiyo inawezekana taarifa ya Mdude kuingizwa mtegoni na mwanadada mrembo mwenye hela ni hadithi ya kubuni iliyolenga kuhalalisha mashataka dhidi yake kuhusu madawa ya kulevya. Na kwa kiasi fulani wamefanikiwa kwa sababu hata ukisoma mitandaoni ni kama vile watu wameshaamini kwamba Mdude alikutwa na dawa za kulevya.

Hakuna anayejaribu kuwaza kwamba mashatka ya Mdude yanaweza kuwa ya kubambikiziwa. Wengi wanawaza aliingiaje mtegoni kwa huyo dada?

Kwahiyo inawezekana waliomkamata Mdude ndio waliobuni na kusambaza 'hadithi' ya Mdude kuwekwa mtegoni na mwanadada ili madai yao ya kumkamata na dawa za kulevya yapate uhalali (Event conspirancy theory).

Sijui
.
tumeelewana?
.......
Malisa GJ
 
Dah! Bila kuegemea upande wowote katika sakata hilo ukweli ni kwamba hii lugha iliyotumika haina staha. Unajua hata mabeberu wakiikosoa nchi au kiongozi wasiyempenda au wanae tofautiana nae hua wanatumia lugha ya staha sana. Wanajenga hoja tu kwa kile wanachotaka kufikisha ujumbe
 
Mleta uzi nimekuelewa sana

Mambo yafuatayo yanaweza yakapelekea mtu ukaingia kwenye misukosuko na serikali

1. Kukosoa bila staha, unaweka mitusi humo, kejeli humo, uongo humo, huwezi vumilika
2. Unaposhauri upumbavu. kutwa wewe unashauri mambo ambayo kwa mjinga anaweza kuona unaongea points, lakini kumbe ni ushauri uliojaa hila na nia ovu
3. Kuchunguza siri za serikali, unajua kuna kipengele viongozi wa umma huwa wanaapa kuwa hawatatoa siri za serikali, maana yake watafanya juu chini siri isitoke, sasa unapobainika kuchunguza kwa nia ya kutoa siri za serikali, iwe kwenye gazeti, tv, redioni, mtandaoni na kwa mtu fulani unajitafutia tabu nzito nzito

Wanaharakati wa mtandaoni wote, asilimia kubwa wanapokosoa wanadondokea kwenye kipengele namba moja, wasipo badilika wataisha, hawawezi bora wachague kuwa invisible kama kigogo. Ila wanapochagua kuikosoa serikali na kupata popularity, wataisha aisee.
 
Hakuna anayejaribu kuwaza kwamba mashatka ya Mdude yanaweza kuwa ya kubambikiziwa. Wengi wanawaza aliingiaje mtegoni kwa huyo dada?
Kwa utawala wowote wa kidikiteita, kama ningelikuwa judge, ningelimwachia huru kwa kumpa benefit of doubt based on the history persecution ya utawala huu ( najua the laws is against my contention lkn kwa utawala wa Jiwe , nitamwachia Mdude kwa kumpa a big , big, big benefit of doubt)
 
Wanaharakati wa mtandaoni wote, asilimia kubwa wanapokosoa wanadondokea kwenye kipengele namba moja, wasipo badilika wataisha, hawawezi bora wachague kuwa invisible kama kigogo. Ila wanapochagua kuikosoa serikali na kupata popularity, wataisha aisee.
Mawazo ua utumwa uliyonayo!
 
Back
Top Bottom