Naambiwa nimechelewa

Fazul

Member
Apr 2, 2012
82
9
Kuna bint niliyejuana naye kwa mda sasa,ni binti ambaye anayetumiwa kama mfano mwema katika mtaa wangu,si uzuri wa sura 2,tabia,heshma na myenendo,ni msimple sana.nimemtongoza ivi juzi akanambia labda niwe 2 rafikiye wa karibu kwani nimechelewa ako na mpenzi!kwa kweli nampenda sana na moyo wangu umekataa ukweli wa mambo hata kufikiria kuachana naye pekee huniumisha kichwa,ningefurahia kuwa naye maishani,msinione mbinafsi ni moyo wangu naufwata nisaidieni wana jf nifanyeje ndo ni mpate?
 
mmh...nadhani amekuwa mstaarabu sana kukwambia ukweli. Angekudanganya ungeandika thread tofauti hapa...kubaliana na hali halisi kaka!
 
Fazul ushaambiwa umechelewa jamani kubali matokeo yaishe mana uking'ang'anizi wako ndio utamfanya mdada wawatu aanze kuonekana anatabia mbaya wakati hakuaga nazo
 
mmh...nadhani amekuwa mstaarabu sana kukwambia ukweli. Angekudanganya ungeandika thread tofauti hapa...kubaliana na hali halisi kaka!

yenyewe kafanya vizuri lakini vile nahisi huyu ndie ameniridhi hisia zangu kwa huyu ziko tofauti yani ameniingia moyoni kishenzi.
 
ndio ivo anamtu sasa amuache jamani kisa wewe umempenda
 
yenyewe kafanya vizuri lakini vile nahisi huyu ndie ameniridhi hisia zangu kwa huyu ziko tofauti yani ameniingia moyoni kishenzi.

Jiamin utampata aliye mbora zaidi yake...kung'ang'ania hakutakupa matokeo mazuri ndugu.
 
Kubali matokeo huwezijua labda anataka uwe rafiki yake wakati huo huo anakuchunguza vizuri kama unafaa kuwa nae au la
 
endelea kuwa rafiki yake wa karibu... there is a lot of other things you can enjoy together na wala si lazima kila uhusiano wa jinsia hizi mbili uishie kwenye kutongozana
 
Kuna bint niliyejuana naye kwa mda sasa,ni binti ambaye anayetumiwa kama mfano mwema katika mtaa wangu,si uzuri wa sura 2,tabia,heshma na myenendo,ni msimple sana.nimemtongoza ivi juzi akanambia labda niwe 2 rafikiye wa karibu kwani nimechelewa ako na mpenzi!kwa kweli nampenda sana na moyo wangu umekataa ukweli wa mambo hata kufikiria kuachana naye pekee huniumisha kichwa,ningefurahia kuwa naye maishani,msinione mbinafsi ni moyo wangu naufwata nisaidieni wana jf nifanyeje ndo ni mpate?

Kubali! Kubali unasikia? Mahusiano ya siku hizi lazima yawe na rizavu! Mkubalie huku ukimwambia kuwa bado unavuta subira, mambo mawili yatatokea. Utampiga bao huyo aliyoko au utarithi atakapomaliza shifti yake!
 
Kuwa King'ang'anizi kwa muda kwa sababu majibu ya mwanzoni mwanzoni kwa asilimia kubwa yanaweza yasiwe na ukweli wowote either hakuamini kama ungeweza kumtamkia maneno hayo Or Hafikirii kuwa na Mtu kwa sasa au labda ana sababu zake binafsi. Ni vizuri kuchunguza na kufanya utafiti wa kina wa kujua kama kweli anaye,ukigundua kama naye basi MKUU HAPO INABIDI UKUBALIANE NA MATOKEO maana cha mtu ni sumu na usimuumize Mwanaume mwenzio kwa sababu ya MAPENZI.
 
Kama kweli unampenda we muombe picha yake akikupa tayari utakuwa nae kupitia picha anytime na moyo wako utaridhika.
 
endelea kuwa rafiki yake wa karibu... there is a lot of other things you can enjoy together na wala si lazima kila uhusiano wa jinsia hizi mbili uishie kwenye kutongozana

Aendelee kuwa karibu na bibi wa mtu? Kweli?
 
kuna swali hili hujalizwa.. nakuuliza mie..

Una miaka mingapi?
 
Back
Top Bottom