Na Kila Mmoja Wetu Popote Naawe Mtulivu: Tuliangalie Suala la Mapenzi ya Jinsia

OnTheEarth

Member
Jan 1, 2023
75
63
Jambo lolote ambalo linafafanuliwa kama dhambi ni ouvu. Hii ni kwa sababu dhambi ni kosa dhidi ya akili na dhamiri safi. Kwa hiyo si tu kuhusu mapenzi ya jinsia moja au ndoa za jinsia moja, lakini kwa kweli mambo yote yanayokatwa na amri kuu ya mapendo kama ilivyofafanuliwa na amri kumi za Mungu, ni uovu.

Jamii yoyote, kwa kweli popote; si kweli kwamba inapenda na uovu, lakini kwa bahati mbaya sana duniani kuna uovu. Ni jambo lisiloeleweka bado vizuri, kwamba pamoja na uzuri wa ulimwengu lakini mabaya yanatokea.

Tunajifunza kwamba kila kitu kinaanza kwetu, kwetu sisi binadamu. Mara nyingi hii inatokana na tamaa ya kutaka kuwa bora zaidi na wakati mwingine kutokuwa na uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu. Kwa sababu hii tunagundua baadae au wakati huo, kwamba jinsi yetu ya kufikiri na kutenda au kuendea mambo imesababisha uchungu, maumivu na uharibifu. Tunagundua hayo kwa sababu tunalaumiwa ama na sisi wenyewe au wengine. Hali hii ya kulaumiwa haielezi kitu kingine chochote isipokuwa "Ukweli"; kwamba jinsi tulivyofikiri na kutenda sivyo ilivyo, inavyotakiwa kuwa.

Watu wote kama vilivyo vitu vyote, tunatoka kwa chanzo kimoja. Kwa hiyo mtu kwa sababu ya jinsi yake hawezi kudai moja kwa moja kwamba ni bora kuliko viumbe wengine mbele ya chanzo chao. Kwa hiyo kwa namna historia ya mtu ambavyo imekuwa kizazi na kizazi inafunua ukweli huo. Hapa nataka kusema kwamba mambo yote msingi yahusuyo mtu ya imani na dini: ni ya popote na ya kila mtu. Kwa hivyo, si sahihi kudai kwamba utamaduni huu ni wa jamii fulani na kwamba ule ni wa jamii ile; kama ambavyo si sahihi kudai kwamba ardhi au nchi hii ni yetu.

Katika masuala mazito na magumu: mapenzi ya jinsia moja na mengine yenye kufanana na hayo, kwa bahati mbaya kwenye jamii zetu (Afrika na jamii nyingine za kipagani popote) mambo haya jamii inakataa kuyakabili. Lakini swali ni je, mambo hayo hayapo kwenye jamii zetu? Jibu ni kuwa yapo.

Historia ya ouvu kama ilivyo historia ya uhalifu na dhambi yenyewe, inaanza mbali. Si mambo yanayoweza kufikiriwa au kufafanuliwa pekee; kwamba yanatokana na mageuzo au kukua kwa maarifa na maendeleo katika jamii, lakini ni makosa yenye uhusiano wa moja kwa moja na makosa ya mtu. Kwa hiyo uovu wowote sawa ulivyo uhalifu unakwenda mbali katika imani ya mtu aliyomo au jamii iliyomo.

Kwa imani tunapata mafundisho na maadili: makatozo na tamaduni. Kwa imani tunajua chanzo chetu na hatima yetu: ibada na sadaka.
 
Back
Top Bottom