Hawa watakuwa alshababu walahi tutakpukutika kama vumbi
Mh Mh mh........
Am speechless, Maumivu ya kichwa huanza taratibu, na baadaye kusambaa mwili mzima then husababisha kifo..!!! Mara kadhaa Serikali imekanusha juu ya uwepo wa kikundi hiki cha kigaidi huko Tanga. Haya yanathibitisha nini?
Hivi ile Intelijensia ya Polisi iko wapi kwa Matukio kama haya? Wenzetu Nigeria walianza namna hii, huko Kenya hali ilikuwa kama hii. Sisi Tanzania si Malaika kiasi yasitupate mambo haya...Kikubwa tujifunze kung'amua hatari na viashiria vya Ugaidi kama hivi. Polisi, Jeshi la Wananchi washirikiane kwa pamoja kutokomeza vikundi hivi kabla havijamea mizizi
Otherwise tutalia na kusaga meno.
BACK TANGANYIKA
Fact!Nasema hivi, kwa kuwa kabla ya mauuaji waharifu waliulizia/hoji ni sehemu hipi waharifu wanzao walipo fichwa na Polisi - hapo ndipo pa kuanzia - Polisi iwahoji kwa kina vijana ambao walitiwa mbaroni waseme nani kiongozi wao, nani anawapa mafunzo na kuwafadhili, je, lengo lao ni nini hasa, kumbuka wakati mwingine wanatumia silaha za moto, kuna mwana kijiji alisema sura za wengi wao si wenyeji wa pale kama hiyo nikweli wanatoka wapi?
Wasichukulie vitendo hivi kama ni uharifu wa kawaida, haiwezekani Polisi na jwtz wafanye operation ya kuwatokomeza alafu baada ya mwenzi mmoja wakahibuka tena, ujasiri huo wanaupata wapi i.e wanajiamini nini?
Majambazi gani yanaweza kuwa na ubavu wa kutaka kushindana na vyombo vyetu vya Dola, nani anawapa an inside information ya kujua wazalendo wanao wapa taarifa za kintelijinsia jeshi la Polisi alafu watoa taarifa wakajikuta wanageuziwa kibao na waharifu - there's something seriously wrong down the line in Tanga Region - securitywise, that is!
Uko sahihi mkuu. Hawa wahalifu watakuwa wanakaa huko huko kwenye mapango. Na inaelekea sababu ya kuondoka na mchele, sukari na biskuti baada ya kuwa wamewachinja hao wahanga ni kwa ajili ya kujikimu kwa muda mrefu wakiwa huko huko mapangoni.Mi nafikiri nguvu kubwa ingeelekezwa mahali hapo. Miezi kadhaa ya patrol na aerial surveillance yeyote aliyejificha hapo atatoka mwenyewe kwa njaa. Shida ni yawezekana bado tunaona ni mzaha
Iwe fundisho kwa wengine wanaopenda kushirikiana na hao Polisiccm.
Hawana weledi kabisa wa kazi.
Povuuu linakuchomoka mkuu,tulia usipanic bro!waonee huruma hao waliondokewa na ndugu zao alafu ujitafakari na weledi wenu kwy kazi za ulinzi.Kwani nani alikuomba uchague kutulinda sisi?hata mm nafanya kazi ambayo unategemea sana wewe kuishi kwa hiyo kabla ya Kuanza kujifanya mjuaji sana tafakari,angalai kwa undani?kwa nn mauwaji kila kukicha?wapi mumepwaya?je mafunzo ni hafifu?qualification zenu je? Au tatizo ni rushwa? Suggest improvement plan sio povuu jingiii wkt watu wamepoteza ndugu yao na sio mara moja kwy hiyo sehemu.Jeshi la police linahitaji kufumuliwa na kuundwa upya,mambo yakuchukua form four failed hatututaki tena,si unaona jwtz walivyotulia kwanza wapewe hayo maeneo korofi walinde wao,nyie endeleeni kukaa barabarai muwasaidie tra kukusanya ushuru wa road linces nk,hope umenisoma.Usishushie Jeshi la Polisi lawama zisizo za msingi wala ushahidi, askari wapo well trained hawawezi kufanya kitendo kama hicho tena kwa RAIA wema nachoona kutoka kwako ni chuki iliyo wazi kwa Jeshi, ni kwamba hao watu wame suspect tu kuwa kuna mtu kawa chongea kwa wanausalama.
Una point nzuri ya kudumisha uhusiano uliotukuka kati ya Jeshi na Raia wema ili kutokomeza uhalifu but the way una present UZI wako ni kama una widen the gap na kujaribu kuonyesha kuwa Jeshi halijui majukumu yake kitendo ambacho sio sahihi, vijana wanapambana usiku na mchana kudumisha amani ya nchi we upo kitandani unadondosha tu povu.
Maswala ya kiusalama unaandika ovyo utafikiri upo kwenye jukwaa la mapenzi, urafiki na uhusiano, hujui ulitendalo endelea kubwabwaja kwenye mitandao.
Fanya utafiti sio una kurupuka, nina wasiwasi JF imeingiliwa na mapopoma.
Kesi za namna hii zipo nyingi sana. Na watu wameshajua polisi sio wasiri pindi wanapowapelekea ushahidi.si wote, na hao wachache wataondolewa soon!
Magazeti yote yameripoti habari hiyo kama unataka amini kama hutaki basiKa picha katafanya hii habari iaminike.
Hili Suala Jeshi la Polisi na usalama kwa ujumla wabadilike.Watu kadhaa wa kijiji cha Mikocheni karibu na Mapango ya Amboni mkoani Tanga wameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kile kinachodaiwa kufichua vitendo vya uhalifu vya baadhi ya watu kijijini hapo.
================
Jana nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari, sasa huko Kigoma wanakijiji wanalalamika kuwa kila watoapo taarifa kama watu wema, askari waendapo kuwakamata wahalifu usema ''Asingekuwa fulani sisi tusingejua kama una bunduki/silaha''
Kauli hizo zimesababisha matatizo ya uhasama na wanakijiji wamesema endapo polisi wataendelea kutoa siri za wafichua uovu basi hawatashirikiana nao.
Hapo nilishindwa kuelewa ufanyaji wa kazi wa hao polisi, hawajui huo upuuzi wao unaongeza uhasama kwa wanakijiji na kupelekea mauji na uhalifu usiokuwa na msingi.
Tukirudi Tanga, naona itakuwa vile vile tu (Kumradhi),
Ombi langu kwa polisi: Sisi Raia wema tunapotoa taarifa kama hizi za uhalifu lazima mjua tumechoshwa na vitendo hivyo, tunajua majambazi na wahalifu wengine wana mitandao mikubwa, mnapotoa utambulisho wetu mnatuweka kwenye mazingira ya hofu zaidi. Ni nyema mkafanya kazi kwa weledi mkubwa na sio kutafuta sifa.
Wazo lako zuri sana mkuu.Mi nadhani hayo mapango yazibwe tu matobo yake yote yamwagwe zege la nguvu maana yanatugharimu zaidi.
Mbona husomeki kwani hawa waliouwawa ni wamarekani mkuu?Huko Marekani hakufai kabisa kuishi. Rudini makwenu.