Mzinduzi wa kampeni za CCM

mkirua vunjo

Member
Nov 11, 2011
25
5
Jamani wana Arumeru nimesikia kuwa Mzee Mkapa ndio atakuwa kiongozi wa uzinduzi wa kampeni za CCM hapa kwetu Arumeru MAshariki.

Naomba akija ajibu maswali haya

1. Shamba la Madira Estate walilojigawia na Kimaro litarudishwa lini kwa wananchi wa Arumeru wenye ufinyu wa Ardhi.
3. Shamba la Mauwa analomiliki na Mholanzi Jerome na kutoa ajira mbali na wananchi wa Arumeru, Je atatuambia nini sisi wana Arumeru MAshariki.
3. Kwa nini Mashamba ya huyu bwana Jerome hayalipi Service levy
3. Kuna shamba lililoko Tengeru ambaye amekuwa akimiliki na singa singa ammoja lenye ukubwa wa Ekari 3000, Je kwa nini asiwe anatupa tulime mazao ya muda mfupi kwakuwa shamba hilo hukitumia wakati wa kilimo tuu, Na je alijipatiaje hilo shamba huku wana arumeru tukiwa na ufinyu wa Ardhi.

Naomba aanzwe na hayo kwanza

Naomba kuwasilisha
 
haturuhusiwi kuhoji wajibu wetu kusikiliza tu.elimu yetu ni ndogo kuuliza maswali.
 
Cha ajabu kuna watu wataenda kumsikiliza na kumshangilia huyo fisadi.
 
Nawaomba Wana Arumeru mashariki wasipoteze muda kwenda kusikiliza mikutano ya Magamba,maana hawana jipya wao wawe na nia moja ndani ya Mioyo yao kumchangua Joshua Nassari kuwa mbunge wao siku hiyo ya April 01-2012.Kutomchagua Nassari nikuhalalisha na kusheherekea the so called siku ya wajinga duniani!
 
Back
Top Bottom