Mzigo wa madeni ni hatari kwa taifa

mozze

Senior Member
Aug 27, 2010
185
28
Source: Mwananchi

Inasikitisha sana kuwa na serikali isiyokuwa na nidhamu ya matumizi ya hela. Serikali au taasisi makini huwa inakuwa na budget na kuifuata bila kuongeza kitu. Sasa hapa kwetu kila kukicha deni linaongezeka. Mkapa alijitahidi kupunguza, huyu Rais wa sasa aliyekosa umakini anaongeza mzigo kwa watanzania.

Ukisoma magazeti unakuta habari eti anaenda nje kuomba misaada, au tunasoma serikali imepokea msaada kutoka serikali fulani...huu kwa kiasi kikubwa ni uongo, serikali haisemi ukweli kuwa inachukua mikopo badala yake inafanya wananchi waamini serikali inasaidiwa. Huko baadae watoto wetu ndio watakaopata matatizo....

Wananchi inabidi tupigie kelele hili sio kitu kizuri for future of the economy.
 
mkuu mbona nimesikia bajeti iliyotumika mpaka sasa haivuki 50% ya iliyopangwa? ukitoa mishahara
 
KWA MUKTADHA HUU WA MADENI NCHI HAITAENDELEA.

Mdhibiti na Mkaguzi wa Heasabu za Serikali (CAG),Ludovick Utouh amesema katika ripoti yake ya mwaka wa fedha wa 2009/2010 kuwa deni la taifa katika kipindi hicho liliongezeka kwa asilimia 38 kutoka shilingi 7.6 bilioni hadi 10.5 trilioni.Hizi si habari nzuri hata kidogo kwa mustakabali wa ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo kwa ujumla na ni pigo kubwa sana kwa mwananchi mlalahoi na mlipa kodi wa nchi hii.Ripoti hiyo ya CAG inasema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja tu deni la taifa limeongezeka kwa shilingi trilioni 2.8.Katika deni hili la taifa kiasi kikubwa sana cha pesa kimekopwa kutoka taasisi mbalimbali za nje,kwa maana hii Serikali italazimika kuwalipa wadai wake wa nje na hii kiuchumi ina maana kuwa kiasi kikubwa cha mtaji kitakachopatikana kutokana na makusanyo mbalimbali pamoja na kodi kutoka kwa Watanzania masikini kitalipwa nje ya nchi.

Sio vibaya kukopa kwa sababu hakuna nchi isiyokopa duniani lakini nchi nyingi zinazokopa zinakopa kutokana na hali halisi ya uchumi wa nchi zao kwa kuangalia athari zake kwa sasa na kwa miaka mingi inayokuja.Kukopa kwa nchi kunatakiwa kuende sanjari na hali halisi ya ukuaji wa uchumi ili kutoathiri pato la taifa na maendeleo ya nchi kwa ujumla wake lakini kwa nchi yetu jambo hili ni kinyume kabisa sijui ni kwamba viongozi wetu hawajui haya au ni nini..Uchumi wetu umekuwa ukikuwa kwa kasi ndogo sana wa asilimia 6.5 tu katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.Hii inaonyesha jinsi ilivyo hatari kuendelea kukopa bila kuzingatia viashirio vya uchumi kwa kukopa huku kunazidi kuwa mzigo kwa taifa kwa kizazi cha sasa na kijacho kwa sababu deni hilo litalipwa hata na kizazi kijacho kwa sababu kwa sampuli hii deni hili litazidi kuongezeka.

Wenzetu wanakopa kwa kuangalia na kuzingatia vipaumbele vyao kama taifa lakini sisi serikali yetu siielewi vipaumbele vyao ni vipi kwa sababu kila mara wanakuja na vipaumbele vilevile kila bajeti.Tungeweza kuzingatia vipaumbele vyetu vizuri na kutumia rasilimali zetu tulizonazo tusingekuwa na haja ya kukopa kutoka nje na hata tungekopa tungekopa kwa kiasi kidogo sana bila kuathiri uchumi wetu.Pia kwa kuzingatia vipaumbele vyetu vizuri tungeweza kupanua wigo wa ajira,vijana wengi tena walio wasomi na elimu ya kutosha kabisa hawana ajira,hii ni hatari kwa Taifa.Tunapokwenda kama taifa tunafikia ukomo wa kujiendesha na kuendelea kukopa huko kusiko na tija kutaturudisha katika zama za ukoloni kwa sababu itafikia wakati kila kitu tutapangiwa na mataifa ya nje yaliyotukopesha.Serikali yetu imefika mwisho wa kufikiri na tukiendelea kuwa na viongozi wa sampuli ya hawa tulio nao madarakani hatutaendelea kama taifa.
 
Hivi haya makosa ya serikali ambayo CAG huwa anayaleta serikali ya wenye magamba huwa inachukua hatua gani?
 
Mungu atunusuru na balaa hili ,natamani siku moja nishike dola kama Rais wa nchi hii ni wabomoe wote wawe vibogoyo maana meno yao yanawashawishi kufanya ufisadi fedha hizo zinakopwa kwa ajili ya vimada na watoto zao
 
Hivi haya makosa ya serikali ambayo CAG huwa anayaleta serikali ya wenye magamba huwa inachukua hatua gani?

Huwa inakuwa stroy ya kuuza magazeti na maongezi ya Mrema nyakati za jioni!
 
cag5.jpg

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh

NI jambo la fedheha na aibu isiyo kifani kwa Watanzania kwamba nchi yetu imeendelea kulemewa na madeni kiasi kwamba sasa hata vizazi vyetu vijavyo pia vitapaswa kulipa madeni hayo. Ni maisha ya kero na aibu kwamba familia nzima, yaani baba, mama, watoto na wajukuu kila mmoja anajikuta akiishi na mzigo wa madeni makubwa ambayo anatakiwa awalipe wadai wake.

Lakini maisha hayo ya udhalilishwaji yanazidishwa na kutiwa uchungu na ukweli kwamba madeni hayo ya familia hiyo yalikopwa na baba aliyedai anafanya hivyo kwa niaba ya familia, ingawa familia hiyo haikuhusishwa wala kutaarifiwa kwa namna yoyote katika suala hilo. Baya zaidi ni pale baba alipokopa fedha hizo na kuzitumia kufuatana na matakwa yake binafsi.

Ni katika muktadha huo, mzigo wa deni la taifa ambao umefikia zaidi ya Sh 10.5 trilioni na unaoendelea kuwaelemea Watanzania unapaswa kuangaliwa. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema katika ripoti yake ya mwaka wa fedha wa 2009/2010 kuwa deni la taifa katika kipindi hicho liliongezeka kwa asilimia 38 kutoka Sh7.6 bilioni hadi Sh10.5 trilioni.

Hizi ni habari za kushtusha sana kwani kuongezeka kwa deni hilo ni pigo kubwa kwa wananchi kwa kuwa ndio walipaji wakubwa wa kodi mbalimbali licha ya wengi wao kuwa fukara. Ripoti hiyo ya CAG inazidi kuibua maswali kuliko majibu inaposema kuwa, katika kipindi cha mwaka mmoja tu, deni la taifa limeongezeka kwa Sh2.8 trilioni.

Hali hiyo haitoi matumaini kwa ustawi wa taifa letu, kwa maana ya Serikali kujenga uchumi imara kwa kuhakikisha kuwa nchi yetu haitumii kuliko kile inachopata. Ndio maana tunataharuki ripoti hiyo ya CAG inaposema pia kuwa, katika kipindi hicho, Serikali iliongeza deni la nje kwa zaidi ya Sh2.5 trilioni, sawa na asilimia 44, huku deni la ndani likiongezeka kwa zaidi ya Sh521.2 bilioni, sawa na asilimia 23.

Tafsiri ya moja kwa moja ya hali hiyo ni kwamba, pamoja na Serikali kusheheni wataalamu wa uchumi wanaoishauri, ilikopa kiasi kikubwa cha fedha kutoka katika taasisi mbalimbali za nje kuliko kiasi cha fedha kilichokopwa kutoka katika taasisi zetu hapa nchini. Kama CAG alivyosema katika ripoti hiyo, hii ina maana kuwa Serikali italazimika kuwalipa wadai wake walioko nje na hii kiuchumi ina maana kuwa kiasi kikubwa cha mtaji katika fedha za kigeni kitalipwa nje ya nchi.

Tunaungana na CAG kuishauri Serikali kwamba kwa kuwa uchumi wa nchi yetu umekua kwa asilimia 6.5 tu katika kipindi hicho, ni hatari kwa Serikali kuendelea kukopa pasipo kutilia maanani ukuaji wa hali ya uchumi wetu hasa kwa kutilia maanani kwamba CAG aligundua deni lisilotarajiwa ambapo wizara tisa na mikoa mitatu ilikopa Sh26 bilioni pasipo kuchukuliwa hatua. Madeni yasiyotarajiwa kama hayo ni mzigo kwa Serikali hasa pale yanapoiva na kutakiwa kulipwa.

Lakini jambo la kushangaza ni kuwa, wakati deni la taifa likizidi kukua kwa kiwango tulichotaja hapo juu, ripoti ya CAG inabaininisha kuwapo kwa mikopo isiyorejeshwa ya Sh424 bilioni katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la Sh7.6 bilioni, sawa na asilimia mbili kulinganisha na kipindi kilichotangulia cha mwaka 2008/9. Hii ni ishara mbaya kwa uchumi wetu, hasa ripoti ya CAG inaposisitiza kuwa madeni yamekaa bila kulipwa kwa kipindi cha miaka mitatu.

Sisi tunasema kuwa Serikali iuchukulie ushauri wa CAG kwa umuhimu mkubwa. Tunapendekeza kuwa mtindo wa kukopa pasipo kuzingatia vipaumbele vya taifa letu kiuchumi ukome na ubuniwe mchakato ambao utailazimisha Serikali kupitia kabla ya kutafuta mikopo kwa wafadhili na taasisi za fedha. Serikali isome alama za nyakati na kutambua kuwa wakati wa kukopa fedha na kuitumia itakavyo umepita.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Fika pale Wizara ya Fedha, omba kuonana na katibu mkuu, msaidizi wake, naibu waziri, makamishna, wakurugenzi wa idara na mheshimiwa mmoja anaitwa Mkullo, ni matumaini yangu utapata majibu ya kuridhisha.

Ukishindwa hapo fika, andika barua au piga simu kwenda:
Ofisi ya rais Ikulu, P.O Box 9120 Dar es Salaam au simu nambari 2116898, 2116899. Muulizie mpangaji wa hapo.
 
Thanks man kwa post hiyo. Na sio 7.6bilioni ni 7.6 trilioni. Naweka sawa nukuu zako.
 
mi naona hali kama hiyo ndo nzuri maana jinsi ninavo mchukia JK na utawala wake ============== anajua mwenyewe
 
Back
Top Bottom