Mzee Makamba ulimi uliteleza, alikuwa kwenye emotions. Je, Bashiru ulimi haukuteleza?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,953
4,326
Ni kweli kabisa hasa kwa wanasiasa wawapo majukwaani, wakiwa wamepandwa na midadi au mihemko (emotions), ulimi wakati fulani huweza kutereza na kusema mambo ambayo hawakukusudia.

Jana Mzee Makamba ulimi ulimteleza na kutamka maneno ya maudhi kusiana na vifo vya marais wetu. Bahati nzuri rais ambaye alikuwapo live wakati Mzee Makamba akitamka maneno hayo, aligundua kuwa Makamba ulimi ulimtereza tu kwani alionekana kupandwa na mhemko (emotions).

Hakuyasema maneno hayo kwa kusudi tulilomuelewa. Hii ni kweli kabisa.

Hivyo hivyo Dr Bashiri aliposema maneno yale bila shaka naye alikuwa kwenye mhemko na ulimi ukatereza kuyasema yale ambayo tuliyaelewa sivyo na aliyokusudia.

Sasa kwa nini hadi sasa Dr Bashiru anazidi kulaumiwa sana kwa maneno ambayo ulimi wake uliteleza akiwa kwenye emotions?

Naamini hata Ndugae naye ulimi ulimtereza tu na aliomba asamehewe kwani hakukusudia hicho tulichomwelewa.

Ulimi kuteleza ni ajali kama ajali zingine. Kila mtu inaweza mtokea hiyo ajali. Tunapojenga tabia ya kuwasakama na hata kuwaadhibu wahenga wa ajali hii tunakuwa tunafanya makosa makubwa. Tunakiharibu chama, kinakuwa chama cha kusakamana. Turudi kwenye desturi ya kuvumiliana na kumezeana pale ndimi zinapoteleza. Huu ndiyo uungwana.
 
Laana ya Lissu, Ben Saana, Azory, Mawazo na wengineo, ndio zinawatafutana bila kusahau maovu mengine kama kupora uchunguzi, kununua wapinzani, kunyanyasa wapinzani, kuvuruga mchakato wa katiba, n.k.

Viongozi wenu hawaropoki kwa bahati mbaya tu, bali huo ni mpango wa Mungu katika kukamilisha anguko lenu.

CCM mnaweza kuanguka madarakani pasipo hata mende kuuwawa bali kwa nguvu sizoonekana na macho ya mwanadamu ingawa mmejaa viburi na kulewa madaraka.

Kama alivyoanguka Ndugai kutoka katika kiti cha uspika, ndivyo ambavyo CCM inaweza kuja kuanguka kutoka madarakani kwa kufanya kosa watalokuja kulijutia baadae, kosa ambalo watatengenezewa ili waanguke moja kwa moja.

Kinachoendelea sasa ni Nature kuidhoofisha CCM ili kosa dogo tu hapo baadae, iwe ni kama kumwagia petrol kwenye moto unaowaka.

Hamtanielewa kwa sass kwasababu ni lazima kwanza Muanguke ndio mje mfumbuliwe macho.

Akili zenu zitapumbazwa, mioyo yenu itafanywa kuwa migumu mpaka pale yatapotimia.

Time will tell.
 
Laana ya Lissu, Ben Saana, Azory, Mawazo na wengineo, ndio zinawatafutana bila kusahau maovu mengine kama kupora uchunguzi, kununua wapinzani, kunyanyasa wapinzani, kuvuruga mchakato wa katiba, n.k.

Viongozi wenu hawaropoki bahati mbaya bali huo ni mpango wa Mungu katika kukamilisha anguko lenu.
Wamekuwa mnara wa Babeli.
 
Ni kweli kabisa hasa kwa wanasiasa wawapo majukwaani, wakiwa wamepandwa na midadi au mihemko (emotions), ulimi wakati fulani huweza kutereza na kusema mambo ambayo hawakukusudia...
Naungana na kauli ya Mzee Makamba. Magufuli alikufa kwa sababu hakuwa mtu mwema. Tulisali tuliomba na Mungu akatusikia.

Huwezi kubomoa nyumba za Kimara- bila fidia halafu za Mwanza unawaambia TANROADS wasibomoe kwa vile ndiyo waliokupa kura.

Mungu hawezi kukuacha
 
Kwani wewe unakuja kumtetea kama nani? Kwani yeye amekuhakikishia hilo kuwa aliteleza au tayari yeye anajua message sent?
 
Laana ya Lissu, Ben Saana, Azory, Mawazo na wengineo, ndio zinawatafutana bila kusahau maovu mengine kama kupora uchunguzi, kununua wapinzani, kunyanyasa wapinzani, kuvuruga mchakato wa katiba, n.k.

Viongozi wenu hawaropoki bahati mbaya bali huo ni mpango wa Mungu katika kukamilisha anguko lenu.
Sio kila mtu ana weza kutoa laana
 
Naungana na kauli ya Mzee Makamba. Magufuli alijufa kwa sababu hakuwa mtu mwema. Tulisali tuliomba na Mungu akatusikia.

Huwezi kubomoa nyumba za Kimara- bila fidia halafu za Mwanza unawaambia TANROADS wasibomoe kwa vile ndiyo waliokupa kura.

Mungu hawezi kukuacha
Pole kwa yaliyokukuta Ila ulishahili kubomolewa kabisa
 
Laana ya Lissu, Ben Saana, Azory, Mawazo na wengineo, ndio zinawatafutana bila kusahau maovu mengine kama kupora uchunguzi, kununua wapinzani, kunyanyasa wapinzani, kuvuruga mchakato wa katiba, n.k.

Viongozi wenu hawaropoki bahati mbaya bali huo ni mpango wa Mungu katika
kukamilisha anguko lenu.
Kwani kuna mtu ambaye hajawahi kuropoka aka ulimi kutereza, au hatakuja kuropoka? Ndivyo binadamu wote walivyoumbwa. Cha msingi ni kuvumiliana.

CCM walikuwa mabingwa sana wa kuvumiliana hadi hivi karibuni. Chadema, on the other hand, walikuwa mabingwa sana wa kusakamana hususani wale akina mama 19 ambao wanaendelea kuwasakama hadi kwenye mahakama kuu.

Haka ka tabia ka kusakamana, CCM watakuwa wameambukizwa na Chadema baada ya kuwakosa bungeni na kukalia viti vyao walivyoviacha na vimelea vya maambukizi ya chuki na kusakamana wao kwa wao.
 
Ni kweli kabisa hasa kwa wanasiasa wawapo majukwaani, wakiwa wamepandwa na midadi au mihemko (emotions), ulimi wakati fulani huweza kutereza na kusema mambo ambayo hawakukusudia...
Wewe ni doctor wa nini? Suala la Makamba kudhihaki watu waliokufa ni suala la Ethics; unajua maana ya Ethics; kama umesoma huo udaktari wa PhD ungejua maana yake.

Bashiru siyo suala la ethics, ni Siasa

Drop the The Dr before your name
 
Wewe ni doctor wa nini? Suala la Makamba kudhihaki watu waliokufa ni suala la Ethics; unajua maana ya Ethics; kama umesoma huo udaktari wa PhD ungejua maana yake...
Inaelekea wewe ethics kwako ni ile medical ethics pekee. Kwa taarifa yako ethics ziko kwenye masuala yote na taasisi zote. Hata huko kwenye siasa kuna political ethics.

Vyama vya siasa vina ethics zake. Nchi ina ethics zake. Ethics ni maadili mema. Maneno ya Mzee Makamba yalionekana kukiuka maadili mema ya mwanachama wa ccm dhidi ya viongozi wa chama waliotangulia mbele ya haki.

Maneno ya Dr Bashiri yalionekana kukiuka maadili mema ya mwanachama cha ccm dhidi ya kiongozi wake mkuu wa chama chake na mkuu wa nchi. Wote wawili ndimi ziliwateleza na wakaonekana hawana maadili mema ie wamewakosea adabu viongozi wakuu wao.
 
Back
Top Bottom