Mzee hataki mdogo wangu aoe binti aliyelelewa na Single Mother

Kuna binti wa kichaga mrembo sana amelelewa na wazazi wake wote wawili ni jirani yetu, baba yake ni mzazi mzuri na very strict kwenye familia yake alijitahidi kumpeleka shule nzuri mpk Nairobi lakini haikufua dafu, huyo binti amezalishwa watoto wa3 na vijana tofauti...hivi ninavyoongea wawili anawalea baba mzazi wa huyo binti na mkewe ambae ni mama wa huyo binti na huyo mtoto wake mdogo wamemfukuza nae akamtafute baba yake wamechoka kulea wajukuu.

Mwingine ni binti flani mama yake ni muhaya, single mother pia nae alikua ni jirani yetu japo alishahama..mama yake alisema alipewa mimba na baba wa yule binti akamtelekeza, yule single mother akaamua akaamua kua mlinzi ikifika usiku anavaa sare zake za "aurora security" anaenda kazini na mchana alikua anajishughulisha na kupika mama ntilie, binti yake alisoma shule za serilali na akafaulu vizuri sana...sasa hv nnavyoandika ni muhasibu mkubwa tu kwenye kampuni fulani, ameolewa na ana watoto wawili! Mama yake alikua anaishi pale kwny ile nyumba km kuilinda tu so amemjengea nyumba mama yake na amemsaidia kumpa mtaji wa upishi wa kwenye masherehe!

Mentality za kiafrica sometimes hua zinasikitisha sana, wengi mnaongelea kwa nn ndugu wa baba wa huyo binti hawapo hivi kweli mwanaume akupe mimba akutelekeze na mtoto utaenda kutafuta ndugu zake?? Yaan upate muda wa kulea mtoto na wa kutafuta ndugu zake kweli? Hao kila siku wanaolia kweye ndoa wamepata wanawake wabovu waliolewa na masingle mama? Na wewe kijana wa kiume umepata mwanamke unaona hafai kwa nn uzae nae? Na ikitokea umezaa nae hakikisha unamfatilia mtoto wako pia hata km huyo mama yake huna muda nae inasaidia sana ktk kukuza akili ya mtoto na upendo juu ya baba yake.
 
Dogo kapagawa, na mzee ndio msimamo wake sijui nyie wakuu wa hapa JF manasemaje mzee yupo sawa?
Tupe mrejesho wa dogo. Ila kiukweli dogo ashukuru kuepushiwa majanga hapo. Mtoto hawezi kuozeshwa na upande mmoja tu wa wazazi.
 
Mimi nimuathirika katika seals la kuoa binti aliyelelewa na Single mother, yan mzee huyu aliyemkatalia mtoto yuko sahihi 101%, kilichonitokea kwa binti huyu nilikufa na kuoza kwake hakisimuliki, tuliishi miaka kumi ya moto had nikashindwa mwenyewe tukaachana, now ninaye mwingine anayenipenda na kumpenda na ndo naona kama nimeoa sasa make nafasi ya mwanaume kwenye familia naiona.
Dogo afikirie alichomshauri mzazi make wazazi ni Mungu wa piling Duniani.
Hapo hakuna ndoa ni majanga tupu, mama mkwe atakuendeshea familia had ukome uuuuuuuwwwwiiiiii niliyoyapitia sitaman mtu ayapitie, Dogo achaa tena acha kabisaaaaaa
 
Wakuu poleni na majukumu

Mdogo wangu wa kiume alileta taarifa za kuoa kwa mzee wetu nyumbani Marangu Mamba Lekura, mkoa wa Kilimanjaro, Binti aliyehitaji kumuoa ni Mwenyeji wa Mkoa wa Bukoba huko

So mzee alipokea swala lake kwa mikono miwili, wakaitwa wazee wengine siku ikapangwa kuelekea nyumbani kwa Binti Bukoba kwa wazazi wake ili kuweka mambo sawa, kilichotokea baada ya kufika huko mzee akawakuta ndugu wa binti upande wa mama yake lanini upande wa mwanaume hajaonekana hata mmoja

Mzee kuona hivyo ikabidi ahoji kuwa ndugu wa binti kuanzia baba yake mzazi na baba zake wadogo hadi shangazi zake wako wapi, anahitaji kuwaona na kuwafahamu, mama mtu akasema kuwa waliachana na baba wa binti mda hivyo yeye ndio kila kitu kwa Binti

Mzee kusikia hivyo akaliamsha popo kuwa hapa hamna cha ndoa wala kuchumbia , akampiga mkwara mdogo wangu kuwa pale sio pa kuowa ataowa majanga hivyo mzee wakaondoka na wazee wenzake kurudi marangu wakamuacha dogo kule kasusa kurudi na wazee

Mzee ana hoja hizi kwa nilivyomsikia mimi

* Anasema kuoa Binti ambaye alikosa malezi ya baba,kutokana na ugomvi kati ya wazazi wake huwa ni majanga

*Mzee anasema kuwa mabinti wengi walioshuhudia kuachana kwa wazazi wao hasa ukute mama ndio alikuwa na majanga basi na wao mbeleni huwa ni wasumbufu vile vile maana mama zo huwajaza sumu kuhusu wanaume

* Mzee anadai familia yoyote unayoenda kuowa baba wa mwanamke lazima awepo hata kama kashafariki basi ndugu wa baba kama baba wadogo wawepo la sivyo yakitokea matatizo huko mbeleni hutokuwa na mtu wa kumkemea huyo binti kama ana majanga, na ndoa haitokuwa na Baraka

* Mzee pia anadai kuwa masingle mother wengi huachwa na wanaume kutokana n matatizo mbali mbali hasa kutokujielewa hivyo huwalea watoto na kuwajaza sumu kuhusu wanaume hivyo binti huwa tayari kashalelewa vibaya na ashaona mama yake ameishi mwenyewe hivyo hata mkipishana kauli kukwambia achana nae aishi mwenyewe haoni tabu

* Pia anadai mabinti wengi wanaolelewa na mama zao tu wakati baba wapo hai, huwa wana matatizo hata ukioa hiyo ndoa haitodumu

Dogo kapagawa, na mzee ndio msimamo wake sijui nyie wakuu wa hapa JF manasemaje mzee yupo sawa?
Yuko sahihi.. hataukimtendea vizuri vipi atakuwa haridhiki
 
Hint: Ukitaka kuoa angalia mwanamke aina ya familia anatoka kama wazazi wametengana kunauwezekano wa 105% ndoa yenu pia kutosimama..

Ni kama vile ukifatilia majambazi wengi ni watu ambao hawakulelewa na wazazi wote wawili..

Kama ni mjanja hizo dalili utaziona mapema sana kwenye mahusiano yenu.. chunguza kauli zake kuhusu wanaume n.k..
 
Bila kusahau wengi huwa hawana heshima kwa wanaume zao au waume zao

Sio wote ila asilimia kubwa, ndio maana malezi ya wazazi wote wawili kwa mtoto ni muhimu sana unless itokee sababu iliyo nje ya uwezo wa kibinadamu kama kifo

On the other point, hata mimi nimejiuliza, kama mama alishaachana na baba wa huyo binti, na hakuwepo ndugu yeyote wa kiumeni....yaani hata shangazi, hapo ni pa kujuliza mara mbili, that means ukigombana na baba wa mtoto unagombana na ukoo mzima? Ameshindwa hata kuwashirikisha bava wadogo au mashangazi za huyo binti? Siamini kama wameshirikishwa wakagoma kufika au hata kutuma mwakilishi

On contrary, pengine upande wa kiumeni ulisusa labda binti sio mtoto wao walibambikiwa.

Ni baadhi ya maswali ambayo mzee wako anajiuliza na hana majibu
umenena!
 
Mwambie amsikilize mzee anasema nini, otherwise mdogo wako ataish maisha mabaya na magumu sana kwani mzee mpaka kukataa ameona mbali sana .
 
Sasa uende ukaoe kwa nyumba km ya FAIZA ALLY....si unatafuta balaa
Mwanamke anamchamba na kumvua nguo baba wa mtoto wake hadharani..ilhali mtoto wao ni wakike na anakuja kukua kuyakuta mauchafu ya baba alotangaziwa na mama yake....tht girl will neva respct any man...maaana mama kakosa adabu
 
tatizo la ukosefu wa malezi ya baba "Fatherlessness" ni moja ya janga kuu la dunia kwa sasa kuliko hata hiyo CORONA. Umaskini, mimba za utotoni, ushoga, kujiua, matumizi ya madawa ya kulevya, kushindwa kuendelea na shule ni baadhi ya matatizo yatokanayo na ukosefu wa baba/malezi ya baba.Hii ina maanisha kuwa mtoto aliyelelewa bila ya baba ama baba asiyejishughulisha na malezi anayo nafasi kubwa kuingia katika mojawapo ya hatari hizi.

singo mothers wengi hujitahidi sana kufanya kila kitu kuwafurahisha watoto wao, ila "hakuna kitu cha thamani kwa watoto kama malezi ya wazazi wawili". hii ya kununu kila kitu kwa mtoto, kufanya kila kitu kwa mtoto ni kujifariji kwa singo mother.

Athari za malezi ya mzazi mmoja hayaishii kwa mtoto tu, yanakwenda hata kwenye ndoa. Mwanamke anaye olewa akitoka moja kwa moja kwa wazazi/walezi wake, na mwanamke anaye olewa akiwa ameanza kujitegemea, wa kwanza ni bora kuliko wa pili.
mwanamke anaye olewa akiwa ametoka kwa baba na mama (huyu ni bora) na ambaye anatoka kwa mama pekeyake (huyu si bora) , na ndio hanzo cha ndoa nyingi kuyumba miaka yetu hii.

kwa wale ambao hawajaingia kwenye mfumo huu, fikiria mara mbili mbili. kwa walioko kwenye ndoa linda ndoa yako kama roho yako. Ukishindwa kujifunza kwa kusikia, basi utajifunza kwa maumivu.!
Mimi niliolewa na mwanaume ambaye kalelewa na mama tu ni majanga aisee. Kote kote ni tatizo iwe mwanamke au mwanaume. Tujaribu kuwalea watoto wetu kwa pamoja hata kama mmetengana
 
Hivi na sisi tuliofiwa na baba zetu tukiwa wadogo, huwa tunaingia kwenye hili kundi la watoto waliolelewa na single mom?

back to topic....
ndani ya hizo point kuna ukweli ndani yake, nilishashuhudia familia za hivo, mama akilea mwenyewe binti akapata mafanikio lazima anakua na hii "mama amenilea peke ake akafanikiwa hata mimi mwenyewe nitafanikiwa" hivo mme sio kipaumbele kabisa jiandae kwa lolote.

lakini pia sio lazma iwe hivo kwa kila mtu ila kwa wengi ni hivyo.
Na wale ambao Baba zao wanakimbia familia nakwenda kuishi kwa vimada na mke anabakia na watoto na hao vipi sijui wapo kundi gani!
 
Kuna binti wa kichaga mrembo sana amelelewa na wazazi wake wote wawili ni jirani yetu, baba yake ni mzazi mzuri na very strict kwenye familia yake alijitahidi kumpeleka shule nzuri mpk Nairobi lakini haikufua dafu, huyo binti amezalishwa watoto wa3 na vijana tofauti...hivi ninavyoongea wawili anawalea baba mzazi wa huyo binti na mkewe ambae ni mama wa huyo binti na huyo mtoto wake mdogo wamemfukuza nae akamtafute baba yake wamechoka kulea wajukuu.

Mwingine ni binti flani mama yake ni muhaya, single mother pia nae alikua ni jirani yetu japo alishahama..mama yake alisema alipewa mimba na baba wa yule binti akamtelekeza, yule single mother akaamua akaamua kua mlinzi ikifika usiku anavaa sare zake za "aurora security" anaenda kazini na mchana alikua anajishughulisha na kupika mama ntilie, binti yake alisoma shule za serilali na akafaulu vizuri sana...sasa hv nnavyoandika ni muhasibu mkubwa tu kwenye kampuni fulani, ameolewa na ana watoto wawili! Mama yake alikua anaishi pale kwny ile nyumba km kuilinda tu so amemjengea nyumba mama yake na amemsaidia kumpa mtaji wa upishi wa kwenye masherehe!

Mentality za kiafrica sometimes hua zinasikitisha sana, wengi mnaongelea kwa nn ndugu wa baba wa huyo binti hawapo hivi kweli mwanaume akupe mimba akutelekeze na mtoto utaenda kutafuta ndugu zake?? Yaan upate muda wa kulea mtoto na wa kutafuta ndugu zake kweli? Hao kila siku wanaolia kweye ndoa wamepata wanawake wabovu waliolewa na masingle mama? Na wewe kijana wa kiume umepata mwanamke unaona hafai kwa nn uzae nae? Na ikitokea umezaa nae hakikisha unamfatilia mtoto wako pia hata km huyo mama yake huna muda nae inasaidia sana ktk kukuza akili ya mtoto na upendo juu ya baba yake.
Mtu akupe mtoto na kukimbia kisha umlee mwenyewe eti siku ya harusi ukawatafute ndugu wa Baba yake mmm ujinga wakiwango cha rami, huwa najiuliza vijana wanao lelewa na single mother wao sijui vipi ndoa zao wanazitunza vizuri au ndiyo wale kila kitu lazima akaulizwe Mama kwanza, akitaka kununua kiwanja lazima aulizwe Mama, maana wanasemwa mabinti tu!
 
Mimi niliolewa na mwanaume ambaye kalelewa na mama tu ni majanga aisee. Kote kote ni tatizo iwe mwanamke au mwanaume. Tujaribu kuwalea watoto wetu kwa pamoja hata kama mmetengana
Yaani hawajui kabisa kuishi na wake zao huona mbona Mama alikuwa anapambana bila Baba kwanini mie mke anibane bane, kila kitu Mama , hata, ndiyo wale kina Mama wanaowapangia watoto wao wakiume jinsi yakuishi na Mkewe na kuona mke anafaidi sana pesa ya mtoto wake, hizi mambo zipo kotekote sio kwa mabinti tu hata kwa vijana wakiume ni wale wale tu
 
Yaani kwanza adabu hana, anamdharau baba yake mzazi. Kila kitu ni mama yangu alikuwa hivi mara vile,, mara mbabe alikuwa anampiga hadi baba, yaani tabu tupu. Halafu kicheche hatari. Nikaona isiwe tabu, nikaachana naye.
 
Pole sana, ila adabu hawana kabisa wasisemwe mabinti na wakiume ni hivyo hivyo, kila kitu Mama Mama utazani yeye mwanamke hana Baba
 
Back
Top Bottom