Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 59,226
- 79,517
Wana JF,
Imefika wakati sasa kuanza kuhoji nani haswa ni Mzanzibari Asilia kihistoria maana tunakoenda sasa si huko na katika kujua haya inatupasa kupitia historia yetu hata kabla Waajemi na Waomani hawajatua Zanzibar yaani wakati huo visiwa hivi vikiwa na majina ya Kiasili ya kiafrika yaani Unguja n.k. na pia kipindi cha Wareno pia kipindi cha Wajerumani hadi Waingereza na pia siasa na utaifa wa Kizanzibari baada ya uhuru na mapinduzi ya Zanzibar
Tuanze na historia ya Unguja kabla ya mwarabu kuja; inasemekana kulikuwa na waafrika (ngozi nyeusi) wakiishi huko wengi wao walikuwa ni wale wavuvi wanaotoka pwani ya Tanganyika wakiienda huko kutokana na shughuli za uvuvi na hata baadhi yao kuwa na makazi yao huko na pwani pia; watu hawa walikuwa na dini za kiasilia wakifanya matambiko na yale yote yanayofanywa na wenzao wa Pwani yaani makabila ya Pwani kiutamaduni.
Haya yote yalianza kubadilika pale Mwarabu toka Oman alipotia nanga katika visiwa vile kwani utawala wa Asili haukuwa na nguvu ya kumzuia Mwarabu kufanya anachotaka maana alikuwa na silaha za kivita yaani bunduki iliyokuwa bora zaidi ya mkuki, mshale au sime. Kwa mantiki hiyo basi uhuru wa Mwafrika halisi ukapotea pale tu Mwarabu alipotia mguu katika visiwa vile. Mbali na hayo biashara haramu kama utumwa ilianzishwa na Mwarabu na pia biashara ya pembe za ndovu zilizomlazimisha kwenda hadi Ujiji kusaka vipusa hivyo. Kutokana na kushamiri kwa biashara hii ya utumwa na ndovu; visiwa hivi vilitamanisha watu wa mataifa mbalimbali haswa Mashariki ya Mbali hata kusababisha Sultan wa Oman kuamishia makazi yake. Na pia wale wa Magharibi kama Wareno, ambao nia na madhumuni yao yalikuwa kuhodhi biashara ile, matokeo yake mikanganyiko wa kujaribu kuhodhi dola ikawa ni jambo linalojirudia rudia katika jamii hii yenye mseto wa asili yaani Uarabu, Ubantu, Uajemi na Uhindi.
Japokuwa watu wa mataifa mbalimbali wamepita au wameweka maskani Zanzibar, Mwarabu mbali ya kufanya biashara alifanikiwa zaidi kusimika tamaduni zake katika visiwa vya Zanzibar kuliko mataifa yoote yaliyopata kuwapo ambayo yaliwekea uzito suala la biashara kuanzia Wareno na pia Wajerumani na Waingereza ikiwemo ya mali ghafi kwa wale wa nchi za Magharibi haswa kipindi cha Mapinduzi ya viwanda huko kwao!
Historia hii itaendelea.....