My government, this is too much!

bakuza

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
490
100
Serikali na wizi huu hapaaaaaana!!!!

Ktk hali isiyo ya kawaida jana nilifanikiwa kuona salary slip ya mwezi uliopita ya rafiki yangu akiwa analalamikia makato yaliyofanywa bila yeye kujua ni ya nini maana pale wameandika Nanukuu "MCHANGO MAALUM"mwisho wa nukuu,bila kutaja hiyo maalum ni kitu gani.

Nikajisemea moyoni sikubali mpaka nijue haya makato ni ya nini.nawasilisha kwenu Ndugu zangu wenye kujua hili tujuzeni isije ikawa wanachangia vikao vya CCM huko Dodoma.

Maskini ya Mungu huyu jama ni mwl na anaonesha hajui pa kuanzia kujua sababu ya makato hayo na si peke yake bali ni walimu wengi ambao jana walikuwa wakilalama.

Saidia wanyonge hawa wajue pesa yao iliko elekea.

Nawasilisha.......
 
walimkata shs ngapi_kwenye huo mchango maalumu...to start wth....
 
walimkata shs ngapi_kwenye huo mchango maalumu...to start wth....

ilitegemea kiasi cha mshahara kwa niliyeona pay slip yake ni 2500/= sijui wengine walikatwa kiasi gani
 
ilitegemea kiasi cha mshahara kwa niliyeona pay slip yake ni 2500/= sijui wengine walikatwa kiasi gani

mambo ya ku deal na serikali usifuatilie hii 2,500. utatumia zaidi ya hii.

labda ufanye tu kama mwana harakati.
 
mambo ya ku deal na serikali usifuatilie hii 2,500. utatumia zaidi ya hii.

labda ufanye tu kama mwana harakati.

Ndiyo hii ni ndogo kwa kila mmoja ila ukizidisha na wafanyakazi wote waliokatwa ni pesa nyingi sana.na si makato hayo tu mwingine ameonesha wamekata pesa kwa ajiri ya Envelope,etc.
what does it mean Vivian.Mimi simo ktk makato hayo bali ni kujua tu watumishi hawa wanachofanyiwa na serikali yao.
 
Acheni kulalama,mnafikiri huyo RZ1 hayo magari ya kubeba abiria na vitega uchumi vyote anavyomiliki anatoa wapi?????hakika walimu wa TANZANIA hii wangeungana katika mgomo na kuisuport chadema hiyo dhulma isingekuwepo.utidharau hiyo 2500 alakini ukiizidisha mara laki moja ndipo utajua uwingi wake,sidhani kama nchi hii kunamtu anadharaulika na kunyanyaswa kama mwalimu.............unganeni walimu mpiganie haki yenu ya msingi.
 
Tuungane kuwaelimisha maana hii kazi ni yetu sote.Revolution is coming soon.
 
mwajiri hana mamlaka ya kumkata mshahara mwaajiriwa bila idhini yake
waungane watafute wakili wafungue shauri la madai waombe na rejesho na riba
na pia serikali iwajibike kuwalipa fidia zidi.
huu ni uhuni wa waziwazi.
 
mwajiri hana mamlaka ya kumkata mshahara mwaajiri bila idhin yake
waungane watafute wakili wafungue shauri la madai waombe na rejesho na riba
na pia serikali iwajibike kuwalipa fidia zidi.
huu ni uhuni wa waziwazi.

asante mkuu
 
waungane kumwona wajiri wao kupata ufafanuzi wa makato hayo wakinyamaza kila mwezi itakula kwao
 
unachangia maendeleo ya nchi. tunataka kuthubutu zaid, tutaweza na tutasonga mbele mpaka wananchi mtugadaffi.......haha...ha ha........aaaaa.
 
Back
Top Bottom