Mwizi ananiibia ndizi shambani

jogoo wa maajabu

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
664
1,204
Habari zenu wanandugu natumaini mtakuwa salama sana

Miezi 10 nyuma nilifanikiwa kununua eneo nikiwa bado najichanga changa nione nitalifanyia nini hili eneo liweze kunipa matunda muda huo ikanibidi nianze kulipanda ndizi nikaanza kuchimba mashimo ya migomba kwa mikono yangu na nilipoona panapohitaji nguvu kazi kubwa niliweka vibarua wakunisaidia mpaka nkakamilisha mashimo 580 na mbegu za migomba nilichukua kwa majirani zingine nilinunua kwa pesa mpaka nkafanikiwa kupanda shamba zima likiwa na migomba (ndizi) za kupika 350, kuvundika ndizi 100 na ndizi za kuchoma 25 mpaka sasa sijapanda mashimo mengine...

MAFANIKIO
Ndugu zangu ni kwa muda mchache sana kama miezi 8 naanza kuona mafanikio baadhi ya NDIZI zimebeba sana na kuna shule ipo jirani ya mtu binafsi kila ijumaa nmepewa oda niwe napeleka mikungu 20 ya ndizi na kila mkungu wa ndizi nauza mpaka Tsh. 12000 na naweza vuna mikungu ya ndizi zaidi ya 30 kwa mara moja ,

Ndizi zinatoka kubwa na zenye afya kwa sababu kila shimo la mgomba niliweka mbolea ndoo mbili ya samadi.. Na maji yapo karibu kwa hiyo hainipi shida kumwagilia

CHANGAMOTO

Hapa ndo penye umuhimu mkubwa sana na ndo hasa lengo kuu la kuuanzisha Uzi huu kuna wezi wameisha anza kuniibia ndizi shambani nmepata wamekata migomba kama 6 na wameondoka na NDIZI inaniuma sana wadau naombeni msaada najua humu JF kuna watu walishawahi kupitia changamoto kama yangu ama zaidi ila walitatua kwa namna yoyote ile nipo tayari...

"tusameheane kwa mwandiko wangu wakubwa"
 
Habari zenu wanandugu natumaini mtakuwa salama sana....
Miezi 10 nyuma nilifanikiwa kununua eneo nikiwa bado najichanga changa nione nitalifanyia nini hili eneo liweze kunipa matunda
Daaaah pole sana....Kwanza upo mkoa gani?.....Kuna jambo ninaweza kukushauri ila itabidi nikupm tu maana kiukweli umepambana kwa nafas yako...check pm yako
 
Bravooo

Weka mlinzi, Zungusha wavu, kisha otesha bougainvillea, na mbwaa (wanasaidia usiku na mchana manake mlinzi aweza sinzia/ama akaenda kutafuta utumbo wa kuja kupikia ndizi).

Ongee vizur na majirani -- huenda mwizi ni alokuuzia shamba
 
Yupo mtaalamu mmoja anauza nyoka,

Nyoka huyo atakaa shambani na mwizi akija na kumuona lazima atoke nduki.

Ukishindwa nyoka anakupa nyuki au madondola,,, mwizi akiibuka yanamshambulia.

Angalizo: Ukitumia njia hizo uwe na uhakika hutoibiwa na ikitokea umemtuma mtu akakate ndizi utamshika sikio.
 
Kuna jamaa miaka ya nyuma huko ilikuwa ukienda kuiba mbao zake badala ya kupeleka ulikokusudia, unapeleka nyumbani kwake.

Ukifika unamkuta anakusubiria, anakuelekeza sehemu ya kuweka then ndio akili zinakujia unaondoka kwa aibu.

Yaani yeye ukienda kuiba tu, anapata alert anaanza kukusubiri nyumbani kwake na kuandaa vizuri sehemu ya kuweka.
 
Bravooo
Weka mlinzi, Zungusha wavu, kisha otesha bougainvillea, na mbwaa (wanasaidia usiku na mchana manake mlinzi aweza sinzia/ama akaenda kutafuta utumbo wa kuja kupikia ndizi)
Ongee vizur na majirani -- huenda mwizi ni alokuuzia shamba
Ahsante ntafanyia kazi rafiki yangu
 
Weka zindiko mkuu, yaani mtu akiingia shambani anaziona ndizi vizuri, akikata na kubeba kimbembe kianzie hapo, hataiona njia na hataweza kushusha ndizi aliyobeba mpaka unamkuta.
Nishndwa nianzie wapi ili nipate zindiko la uhakika boss
 
Vizia ukiwa na mlinzi wako hata kwa kumkodi mkuu,utakayemkuta aise analipa gharama ya mashimo 300 na itakuwa fundisho kwa wengine,
MLINZI AU ULINZI WA KUDUMU UNAHITAJIKA kwa hatua ulofikia
Nimeanza ulinzi mzito nikiwa silaha...
 
Back
Top Bottom