Siku hizi kila mahali ni kiki kwenda mbele kuanzia kwa kaka Mondi na wadogo zake mpaka kwa serikali. Daah maisha yako kasi mno.
 
Walifikiri kwa kiwango cha chini sana, hii tozo ya miamiala inaonesha ni namna gani wanatafuta kodi hata ambazo si rafiki kwa mlipaji.

Hii leo nimetimiza siku 6 bila kutuma pesa kwa njia ya simu.

Acha tu wameporomosha mapato ya makampuni ya simu kwa ukupukaji wao.
 
Watu wengi hasa watanzania hawajui tofauti ya Economics and Finance. Uchumi sio finance, profesion ya Finance hajulikani vzr hivyo watu hupelekea kuwapa wizara ya fedha watu wa uchumi ambao hawana utaalamu kabisa kwenye mambo ya finance...
Mkuu itakuwa umepiga BAF. Umeeleza ukweli mweusi.
 
#ZILIZOTUFIKIA WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa atakutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile pamoja na wataalamu kuzijadili Kanuni za Sheria ya Fedha ya mwaka 2021/22 iliyo anzisha tozo za simu.

Waziri wa Fedha na Mipango ameliambia Shirika la Utangazaji TBC leo Jumatatu (Julai 19, 2021) katika kikao cha pamoja na Waziri wa Mawasiliano kuwa viongozi hao tayari wameshapokea maelekezo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu kuyapitia na kuyafanyia kazi maoni ya watanzania.

"Nimesha elekeza wataalamu wetu kuangalia Paymenent System na Electronic and Postal Payments Acts... Tutachukua hatua katika maeneo ambayo yanahitaji kuchukuliwa hatua ili ujenzi wa taifa letu uweze kuendelea,” alisema Waziri Nchemba na kutahadharisha wanaojaribu kupotosha na kubadili maana halisi yenye maslahi mapana kwa taifa.

#habariLEO #dailynewsdigitalupdates
 
Mama ni msikivu sana. Mwigulu alipotosha baraza kwa hizi kodi za mshikamano
Usikivu upi?
Kwani anaesaini wamwisho ni nani?
Kwani hakujua mapendekezo ya bajeti?
Inamaana siku bajeti inasomwa bungeni nayeye ndo aliisikia kwa mara yakwanza kupitia TBC?

Mwigulu amesema "hiyo ni sheria ya bunge na tayari imeshapitishwa"
Amepitisha nani? Aliisoma kabla hajapitisha? Au ndo mambo yakutengeneza tatizo na kulitatua?
 
Mengine haya hapa yaliyokuwa yanapongeza kwa bashasha hizo tozo jingalao Jumbe Brown Phillipo Bukililo na binamu zao.
Tozo zinaweza kuwa kubwa lakini mantiki yake ipo pale pale.

Ukishaanza kuingia uchumi wa kati hao wafadhili wanakutazama tofauti na yule wa uchumi wa chini.

Zitapunguzwa viwango lakini haziwezi kufutwa. Hakuna mjomba wala shangazi wa kudumu kutoka huko nje, wana matatizo yao mengi tu.
 
Wanaroga kisha wanaagua baadaye wanalazimisha wasifiwe. Hizi zote ni usanii tu na ndio maana hawa watu piga ua hawawezi kukubali katiba mpya.

Wataendelea tu kujipigia kura, kuzihesabu wao wenyewe na kisha kujitangaza washindi. Very stupid indeed.
 
Tozo zinaweza kuwa kubwa lakini mantiki yake ipo pale pale.

Ukishaanza kuingia uchumi wa kati hao wafadhili wanakutazama tofauti na yule wa uchumi wa chini.

Zitapunguzwa viwango lakini haziwezi kufutwa. Hakuna mjomba wala shangazi wa kudumu kutoka huko nje, wana matatizo yao mengi tu.

La msingi ni kutambua kuwa wenye nchi tumedhamiria kumsaidia Mama kuuondoa uozo wote:



Hatutanyamaza tukiona jahazi linakwenda Mrama.
 
Back
Top Bottom