Mwigulu Nchemba: Mnasema maisha magumu? Magari namba E yamejaa Barabarani, na Benki kuna foleni

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,054
49,743
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amewashangaa na kuwazodoa wanaodai Kuna maisha magumu wakati Kuna Utitiri wa magari Namba E Yamejaa Barabarani,Harusi na Bar Zinajaza na Benki Kuna Foleni ya kutoa na kuweka pesa.

Mwigulu anasema Suala la ugumu wa Maisha ni hakuna siku litaisha Duniani ndio maana hata Mataji wakubwa wanajiua.

---
".... Kila kipato kinapoongezeka na matamanio nayo yanaongezeka, hiki ndicho kinachosababisha ugumu wa maisha.

Nilipita hapa mjini juzi, kila baada ya gari mbili unakutana na namba 'E' zinafululiza kama tano ndiyo zinakuja namba nyingine.Nenda kalinganishe na miaka miwili au mingine huko nyuma"

"Zipo hatua tumepiga. Nenda hata benki unakuta viti vimejaa na wengine wengi wamesimama.......

Nenda kwenye harusi kaangalia, huko nyuma hata michango tu ya harusi ilikuwa inatupiga chenga wakati huo.

"Hili jambo la ugumu wa maisha kuanzia tu unapozaliwa ni mpaka unapomaliza. Ndio maana wanasema mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi ni chache tena zilizojaa tabu.

Hamna siku hilo la ugumu litaisha ndio maana hata matajiri wakubwa duniani wanajirusha na kujiua."

Kubwa zaidi tunaloliangalia kama serikali ni uwekezaji mkubwa unaoelekezwa kwenye shughuli za uwekezaji kwasababu huo unaenda kupunguza pengo kati ya walionacho na wale wasionacho.

"...Uwekezaji unaolenga kwenye kukuza sekta binafsi na kwenye sekta inayoajiri watu wengi zaidi ndio unaotoa jawabu la kudumu kwenye maisha na ustawi wa watanzania.

- Mwigulu Nchemba

Waziri wa fedha Tanzania


My Take
Naungana na Mwigulu,Maisha magumu ni subjective na sio jukumu la Moja kwa Moja la Serikali.

View: https://twitter.com/mhdhamad/status/1763258665778168077?t=X45ySDz8mj4S_H21nOcuPQ&s=19
 
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amewashangaa na kuwazodoa wanaodai Kuna maisha magumu wakati Kuna Utitiri wa magari Namba E Yamejaa Barabarani,Harusi na Bar Zinajaza na Benki Kuna Foleni ya kutoa na kuweka pesa.

Mwigulu anasema Suala la ugumu wa Maisha ni hakuna siku litaisha Duniani ndio maana hata Mataji wakubwa wanajiua.

View: https://twitter.com/Jambotv_/status/1763230060654318057?t=CxsEpOsdZjyLYxbzzsT2gg&s=19

My Take
Naungana na Mwigulu,Maisha magumu ni subjective na sio jukumu la Moja kwa Moja la Serikali.

mabega yamebeba kichwa cha kufugia nywele....
 
Kwahio Peasants kule vijijini akaunti zao zinasomaje ?; Hao wanaosema maisha magumu ni hao wenye namba E au majority ambao hata milo mitatu kwao ni anasa...

Huyu mpuuzi kitu ambacho hajui ni kwamba middle class inapungua by the day; Ili jamii istawi inahitaji kuwa na middle classes wengi sio matajiri na middle classes wachache na masikini wengi

Kwahio tuna wachache wanakula na kusaza wakati wengi hawana basic needs ? Na yeye kama kiongozi mtunga Sera anaona hio ni sawa ? Nani alimchagua huyu Mpuuzi ?!!!
 
Back
Top Bottom