jambotemuv
JF-Expert Member
- Feb 7, 2008
- 224
- 62
Mwenyekiti Uda awashukia wabunge Dar
Na Mwandishi wetu
5th March 2012B-pepeChapaMaoni
Meya Dk. Didas MasaburiMwenyekiti Mtendaji wa Kampuni Simon Group, Simon Kisena, amewashukia wabunge wa Dar es Salaam, kwa kuwataka waache kupiga kelele kuhusu uuzwaji wa shirika la usafiri Dar es Salaam (UDA ) wakati yeye anatoa fedha zake mfukoni kuwalipa wafanyakazi wa shirika hilo tangu Juni 10, mwaka jana.
Akizungumza na NIPASHE mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Kisena alisema anawashangaa wabunge hao kupiga kelele kuhususiana na uuzwaji wa shirika hilo na badala yake wajiulize anapata wapi fedha za kuwalipa mishahara wafanya kazi wa shirika hilo.
Alisema kila mwezi anatoa mfukoni kwake shilingi milioni 70 kuwalipa wafanyakazi wapatao 98 mishahara pamoja na makato mbalimbali yanayotakiwa, hivyo wabunge hao waache kupiga kelele.
"Jamani hawa wabunge na wengine wanaopiga kelele kuhusiana na shirika la Uda kwa nini wasijiulize kila mwezi napata wapi shilingi milioni 70 kuwalipa wafanyakazi? Fedha zote hizo natoa mfukoni kwangu," alisema Kisena.
Kwa muda mrefu kumekuwepo na msuguano kati ya wabunge wa Dar es Salaam na Meya Dk. Didas Masaburi, baada ya wabunge hao kudai ubinafsishaji wa shirika hilo umefanyika kifisadi na ukiukwaji wa sheria.
Nadhani swala halali zaidi ni M/kitu kutujulisha mfuko wake umepata wapi uwezo wa milioni 70 za kugawa kila mwezi. Wakishalewa ufisadi aibu zote huondoka.