Mwenye uelewa kuhusu watu walioitwa kwenye usahili-idara ya uhamiaji.

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
10,043
2,000
Samahanini kwa usumbufu wakuu.mimi ni mmoja wa watu tulioitwa kwenye usahili wa idara ya uhamiaji,tarehe yangu niliyopangiwa ni 17/july,nilikua nauliza,huko huwa wanauliza maswali gani,na je kuna mchujo mwingine unapita huko au mtu ukisha itwa kwenye interview ndio tayari ushapata ajira,na je kuna kupigishwa kwata tena kama jwtz au wao ni training ya kawaida tu?ndio hayo tu wakuu,naomba anae jua anisaidie.
 
Intaview maana yake mahojiano, wanapima uwezo wako kama unafaa, kumbuka mko wengi, so wanaangalia kwanin wakuchukuwe wewe na si mwingne.

Swali lako la pili, jibu ni kuitwa usahili sio ndio kupata kazi, upatikanaj wa kaz utategemea kama utaqualify.

Na ikitokea umepita, then utaenda KWATA mjini MOSHI kwa miez 6, then utapangwa sehem mbalmbal kutegemeana na uhitaji, e.g bandarini, makao makuu, airport, kwenye mipaka e.t.c weng hawavai uniform..
 
Kwata Ni Miezi 10 Had
11.....Hua Mnafanya Na
Polisi Ila Polisi Hua
Wanatoka Baada Ya Miezi
6......
 
jamani mwenye link ya majina ya waliochaguliwa uhamiaji naomba aniwekee hapa nione na mimi maana nipo kijijini sana sina mtandao wa magazeti...tafadhali naomba msaada wenu jaman naomba tafadhali sana jaman
 
Mwisho kabla ya kuchukuliwa kuna kile kipimo kikubwa. Jiandae pia kwa hlo ukipita hapo ndio depo sasa, ukimaliza ndio ajira.
 
jamani mwenye link ya majina ya waliochaguliwa uhamiaji naomba aniwekee hapa nione na mimi maana nipo kijijini sana sina mtandao wa magazeti...tafadhali naomba msaada wenu jaman naomba tafadhali sana jaman

Google is everything
 
Interviw italenga zaidi ile organisation unayoendsa kufanya kazi.Hivyo jitahidi ujue shughuli za organisation hiyo na zipi kazi za afisa uhamiaji.
 
maswali ni ya kawaida tu mambo ya civics, uraia nk baada ya hapo ni kwata kwa kwenda mbele mnaweza kwenda ccp au kiwira au jkt ruvu kati ya miezi 6 na mwaka mmoja zen mnapangiwa vituo pia kuna suala la upimaji afya (ukimwi) kabla wakati na baada ya mafunzo ni hayo tu kiongozi
 
Aaaaah! Mishahara ya hapo uhamiaji we si ndo ulikuwa unaiponda unaita ni POSHO? imekuaje tena!?

Aiseee! Mwenyewe nimekuwa nikipitia comments zake nyingi hapa JF na nilijua ni m2 aliyeajiriwa tena post kubwa sana hapa TZ, Kumbe naye bado ni mlamba nyayo.

Pole sana ndug ila utapata.
ni hayo tu.
 
uzi wa toka june 2012 sijui nani kautifua huko mafichoni anawatia watu kichaa bure ngoja na mimi leo nitifue uzi wa zamani kama huu tuone
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom