Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 10,051
- 20,324
Kuna kipindi nilikuwa sina watoto, miaka nenda rudi, nilitafakari maneno haya na kumwambia Mungu kuhusu haya, Mungu alikuja kufungua tumbo la mke wangu, nina watoto hadi tunapambana kuzuia mimba wasije wengine. Mungu ni wa ajabu sana.
Zaburi 127 :3, Watoto ni thawabu toka kwa Bwana.
Mwanzo 9:1,7, Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, zaeni mkaongezeke. We are the remnants of Noah, we are the survivors of the flood and God blessed us to go and multiply.
Walawi 26: 9, kama tukiyashika maagizo ya Mungu, ataongeza uzao wetu. Tutakuwa na uzazi mwingi, na Mungu atalithibitisha hili agano lake analoliweka nasi kwetu.
Zaburi 128:3, yeyote amchaye Bwana, mkewe atakuwa kama mzabibu uzaao nyumbani mwake. Wanawe watachipua kama miche ya mizeituni wakiizunguka meza yake.
Mwanzo 33:5, Yakobo aliinua macho akaona watoto wa Esau, Esau akasema hawa ndio watoto ambao Mungu alimpa kwa neema yake. Mungu wetu ni wa neema na rehema, anatoaga watoto. Bado anayo neema ya kuwapa watu watoto hata leo hivi, kwasababu yeye ni yeye yule jana leo na hata milele. Habadiliki.
Mwanzo 17:6-7, Mungu alimwambia Ibrahim, Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa na wafalme watatoka kwako. Agano hili alilifanya kuwa kwa vizazi vyake vyote. Kitabu cha Wagalatia 3:6-9 kinasema ya kuwa, sisi tu warithi wa ahadi na baraka zote za Ibrahimu.
2wafalme 13:23, Mungu aliwaangalia wana wa Israel, akawasikitikia, akalikumbuka agano aliloliweka pamoja na ibrahim. Mungu huliangalia Neno lake apate kulitimiza. Neno lake linaweza kutimizwa, lazima litatimizwa kwa mtu yeyote anayeamini. Kama Mungu katika Neno lake anasema kuwa watoto hutoka kwake, na hawatoki kwa mganga wa kienyeji wala kwa miungu iwayo yote, basi, ukidai ahadi hii kwa Mungu atakupa watoto. Ijulikane kuwa, Mungu anao uwezo wa kutoa au kutokutoa watoto kwa watu. Mungu ni juu ya yote, akisema ndiyo hakuna wa kusema hapana, akisema hapana hakuna wa kusema ndiyo. Hata kama waganga wa kinyeji au wachawi walikuharibu kimazingara usizae, au manuizo ya kiuchawi ya namna yoyote ile, Mungu ana nguvu kuliko wachawi na waganga wa kienyeji. Anaweza akakuponya na utapata watoto. Uwezo huo Mungu anao. Yeye ndiye aliyeumba mbingu na dunia, aliumba mwanadamu pia. Hivyo, hata kama wachawi au shetani amekudhuru, au hata kama dhambi imekudhuru kabisa, imeharibu kizazi mamba inaporomoka, imeng’ofoa kizazi kimazingara ili wakafanyie biashara, hauendi hedhi, hauna nguvu za kiume n.k, Mungu anaweza akakuumba upya, uwezo huo Mungu wetu anao, anaweza akakuumba upya na ukawa mzima na kutimiza yote unayotaka, na watoto utapata, maadamu tu unamtumainia Bwana peke yake, hautumainii miungu mingine, hautumainii wachawi,waganga na wasoma nyota. Wamtumainio Bwana ni kama mlima sayuni, hawatatikisika milele, mtumaini Bwana ukatende mema, ukae katika nchi upendezwe na uaminifu, nawe utajifurahisha mbele za Bwana,naye atakupa haja za moyo wako.Amina.
1Samweli 1:20, when the right time came up, Hana conceived, akazaa mwana akamwita jina lake Samweli akisema ni kwasababu ametoka kwa Bwana.
Mwanzo 18:14, Malaika walipopeleka taarifa za kuzaa kwa sara, Bwana aliwaambia Ibrahim kuna Neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? And in chapter 21;1,2, Sara conceived of Isaack.
Zaburi 113:9, Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, awe mama wa watoto wenye furaha. (ukianzia kusoma mstari wa kwanza hadi wa tisa; Haleluya, enyi watumishi wa Bwana, sifuni, lisifuni jina la Bwana. Jina la Bwana lihimidiwe, tangu leo na hata milele. Toka maawio ya jua hata machweo yake, jina la Bwana husifiwa. Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote, na utukufu wake ni juu ya mbingu. Ni nani aliye mfano wa Bwana, Mungu wetu aketiye juu? Anyenyekeaye kutazama mbinguni na duniani? Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, na kumpandisha maskini kutoka jaani. Amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, awe mama wa watoto wenye furaha. ).
Isaya 54:1-17, imba wewe uliye tasa, wewe usiyezaa, paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema Bwana. Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako, usiwakataze, ongeza urefu wa kamba zako, vikaze vigingi vya hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto, na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu. Usiogope, maana hutatahayrika; wala usifadhaike, maana hutaaibishwa;kwakuwa utaisahau aibu ya ujana wako pia mashutumu ya ujane wako…(hadi mstari wa 17).
Galatia 4:27, imeandikwa; furahi wewe uliye tasa, usiyezaa, paza sauti ulie, wewe usiye na utungu; maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi kuliko wa huyo aliye na mume.
WATOTO NI ZAWADI TOKA KWA MUNGU
Mwanzo 1 :28, Mungu akawabarikia akisema, zaeni mkaongezeka mkaitiishe nchi.Zaburi 127 :3, Watoto ni thawabu toka kwa Bwana.