Hjalte
Member
- Oct 20, 2023
- 25
- 100
Kumekuwa na tabia ya hovyo sana inayofanywa na madereva pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mabasi ya Mwendokasi, hasa katika vituo vikuu vya Kivukoni na Gerezani nyakati za jioni ambapo foleni ya watu inakuwa ni ndefu, lakini baadhi ya madereva hubakiza/kuingiza baadhi ya rafiki, ndugu na jamaa zao ndani ya mabasi nje ya utaratibu hata pale walipotakiwa kushuka ili wapange foleni na kukaguliwa tiketi (Kwa wanaoenda Mbezi),na kupanga foleni kama utaratibu ulivyo.
Unakuta gari kabla haijapakia abiria walio kwenye mstari tena kwa muda mrefu,tayari ina abiria 8 hadi 10 walio ndani ya gari na hawajakaguliwa tiketi.
Katika hali nyingine ya kushangaza na ya kibaguzi,ni kwamba baadhi ya watumishi katika vituo vya mabasi haya huwapitisha ndugu,jamaa,na marafiki zao kupandia gari ndani kupitia mlango wa kushoto ambao ni maksusi kushusha tu,na wanaopanda kwa utaratibu wa foleni hutumia mlango wa kulia.
Vitendo hivi vinaondoa usawa na kuleta ubaguzi kwa wasio na ndugu wanaofanya kazi UDART,kwani wanakaa kwenye foleni muda mrefu,lakini kuna watu wanafika na kuondoka ndani ya muda mchache tena wakiwawamekaa kwenye seat.