Mwasisi wa NCCR-Mageuzi afariki dunia

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
JUMATATU, OCTOBA 01, 2012 04:57 NA BENJAMIN MASESE

sirikwa1.jpg

Mwasisi wa NCCR-Mageuzi, Emmanuel Ole Sirikwa

MWASISI wa Chama cha NCCR- Mageuzi, Emmanuel Ole Sirikwa (70) amefariki dunia katika Hospitali ya AICC, iliyopo mkoani Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Mussa Kombo Mussa, alisema Ole Sirikwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kupooza (stroke), hadi alipofariki Septemba 28, mwaka huu hospitalini hapo.

Alisema hadi mauti yanamkuta, marehemu Ole Sirikwa alikuwa kamishna wa NCCR Mageuzi Mkoa wa Arusha, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa chama hicho.

"Marehemu Ole Sirikwa alikuwa mwasisi wa chama aliyekuwa na kadi namba 3 ya NCCR-Mageuzi, akitanguliwa na wenye kadi namba 1 na 2 ambao wamekisaliti chama na kuhamia kwingine kutokana na misukosuko ya kijamii.

"Chama kimempoteza mtu muhimu ambaye hakuyumba na aliendelea kubaki ndani ya chama chake, hali iliyotufanya baadhi yetu kumuona kama mzee wa boma la chama," alisema Musa na kuongeza:

"Marehemu Ole Sirikwa alibaki ndani ya chama kwa sababu ya kuheshimu na kuthamini kile alichokianzisha, huku akiamini lengo na madhumuni yake bado hayajafikiwa, sisi tuliobaki tutaendeleza na kuyasimamia mazuri yote ili kufikia lengo alilokusudia," alisema.

Mussa alisema kutokana na umuhimu wa marehemu Ole Sirikwa, chama kimeamua kuenzi uvumilivu na misimamo yake kwa kuuita ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu jina la Ukumbi wa Sirikwa.

Alisema mazishi yanatarajiwa kufanyika Oktoba 3, 2012 kijijini kwake Olijilah, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, yakiongozwa na Mwenyekiti chama hicho taifa, James Mbatia.

Wakati huo huo, Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi, Faustine Sungura, alisema kitendo cha vyama vingine kuzindua kaulimbiu na kuzifanyia kampeni nchi nzima ni dalili za kuanza kupata hofu ya uchaguzi ujao.

Sungura alisema NCCR Mageuzi imejipanga kujibu kwa vitendo kwa kuibuka na ushindi wa wabunge mwaka 2015, licha ya kutofanya operesheni wakati huu.

"Sisi NCCR Mageuzi tumejipanga na mipango yetu ipo ndani ya chama, tunafanya kampeni zetu kisiri, hatuhitaji maandamano na mziki mkubwa kwenye gari, tunataraji kuwa na mavuno mazuri kuanzia 2014 hadi 2015," alisema.

R.I.P Sirikwa... Ulifanya Vizuri kubaki NCCR kuonyesha kuwa ni UPENDO wa MABADILIKO na sio UTAMU

wa VYEO
 
RIP Kirikwa kazi ya kutetea wanyonge umeitimiza kazi kwa wale uliotuacha hapa dunia maana vijana wengi siku hizi wananunuliwa kama kama mafungu ya nyanya. Mungu akupumzishe pema
 
JUMATATU, OCTOBA 01, 2012 04:57 NA BENJAMIN MASESE

sirikwa1.jpg

Mwasisi wa NCCR-Mageuzi, Emmanuel Ole Sirikwa

MWASISI wa Chama cha NCCR- Mageuzi, Emmanuel Ole Sirikwa (70) amefariki dunia katika Hospitali ya AICC, iliyopo mkoani Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Mussa Kombo Mussa, alisema Ole Sirikwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kupooza (stroke), hadi alipofariki Septemba 28, mwaka huu hospitalini hapo.

Alisema hadi mauti yanamkuta, marehemu Ole Sirikwa alikuwa kamishna wa NCCR Mageuzi Mkoa wa Arusha, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa chama hicho.

"Marehemu Ole Sirikwa alikuwa mwasisi wa chama aliyekuwa na kadi namba 3 ya NCCR-Mageuzi, akitanguliwa na wenye kadi namba 1 na 2 ambao wamekisaliti chama na kuhamia kwingine kutokana na misukosuko ya kijamii.

"Chama kimempoteza mtu muhimu ambaye hakuyumba na aliendelea kubaki ndani ya chama chake, hali iliyotufanya baadhi yetu kumuona kama mzee wa boma la chama," alisema Musa na kuongeza:

"Marehemu Ole Sirikwa alibaki ndani ya chama kwa sababu ya kuheshimu na kuthamini kile alichokianzisha, huku akiamini lengo na madhumuni yake bado hayajafikiwa, sisi tuliobaki tutaendeleza na kuyasimamia mazuri yote ili kufikia lengo alilokusudia," alisema.

Mussa alisema kutokana na umuhimu wa marehemu Ole Sirikwa, chama kimeamua kuenzi uvumilivu na misimamo yake kwa kuuita ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu jina la Ukumbi wa Sirikwa.

Alisema mazishi yanatarajiwa kufanyika Oktoba 3, 2012 kijijini kwake Olijilah, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, yakiongozwa na Mwenyekiti chama hicho taifa, James Mbatia.

Wakati huo huo, Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi, Faustine Sungura, alisema kitendo cha vyama vingine kuzindua kaulimbiu na kuzifanyia kampeni nchi nzima ni dalili za kuanza kupata hofu ya uchaguzi ujao.

Sungura alisema NCCR Mageuzi imejipanga kujibu kwa vitendo kwa kuibuka na ushindi wa wabunge mwaka 2015, licha ya kutofanya operesheni wakati huu.

"Sisi NCCR Mageuzi tumejipanga na mipango yetu ipo ndani ya chama, tunafanya kampeni zetu kisiri, hatuhitaji maandamano na mziki mkubwa kwenye gari, tunataraji kuwa na mavuno mazuri kuanzia 2014 hadi 2015," alisema.

Hivi mwasisi wa NCCR-MAGEUZI siyo Mabere Nyaucho Marando?
 
Ni Olgilai na si Olijilah, MUNGU ilaze roho yake mahala pema peponi Amen.
 
Hivi mwasisi wa NCCR-MAGEUZI siyo Mabere Nyaucho Marando?

Waasisi wa NCCR-Mageuzi si mtu mmoja mkuu. Ni karundo ka watu. Ni kundi la watu waliohudhuria kikao fulani kilichokaa kwenye hoteli maarufu enzi zile ikiitwa Motel Agip-- nadhani ilikuwa 1991. Marando alikuwapo kwenye ule mkutano wa Motel Agip ambapo wajumbe walikubaliana kuunda chama kutokana na mkutano ule lakini watu wakasanzuka kila mtu kivyake. Marando alikuwa katika kundi la ma-ring leaders kwenye mkutano ule ambao uliitwa Convention, ambayo ndiyo hiyo "C" ya kwanza katika jina la hiko chama. Kwa hiyo Marando ni Muasisi wa NCCR Mageuzi, lakini hakuwa peke yake. Wengi katika huu utitiri wa tuvyama tudogo wanaweza kuitwa waasisi wa NCCR-Mageuzi pia japo walisanzuka.

NCCR-Mageuzi ilikwa iwe ndicho chama cha upinzani cha kwanza nchini lakini mpango huu ulivurugwa na baadhi ya wajumbe wa mkutano ule kwenda kujiundia kila mtu chama chake. Mzee Fundikira aliunda cha kwake ambacho inakuwa kama amekufa nacho, Sijui kiliitwa MD nini vile nimesahau. Naye Mzee James Mapalala aliunda chama cha kwake ambacho kilikuja kumezwa na kina Maalim Seif na Shaaban Mloo kutengeneza CUF ya sasa, ambapo Mapalala alikuja kupigwa buti na hao kina Sefu. Mtikila naye alijiundia DP yake, na ukawapo mlolongo mrefu wa tuvyama twa mfukoni.

Namkumbuka zaidi Julius Miselya na TLP yake kwenye begi, ambayo ni kama nilisikia alikuja kumuuzia Mrema kwa sijui laki mbili? sijui milioni mbili hata sikumbuki vizuri. Siasa za Tanzania Ukizifuatilia sana unaweza uvunjike mbavu....zina vituko sana! Upo?
 
watu wengine humu JF mnachojua ni kuandika R.I.P fulani, hivi katika siasa za mabadiliko huyo mzee mmewahi kumsikia? utoto unawasumbua kweli
 
Back
Top Bottom