Mkuu huko ni kuwadekeza, fursa mtu inatakiwa uichangamkie, sio uliletewe ulishwe mdomoni,Serikali zote zinazojielewa duniani zinazothamini watu wake zine mifumo rasmi ya kutafuta, kufuatilia, kutathamini na kushawishi watu wake kuwekeza au kuanzisha jambo fulani lenye manufaa kwa jamii na Taifa kwa ujumla
Nimeona taarifa ya MO kuomba kufunga kiwanda cha kahawa lakini waziri mwenye dhamana na kilimo amemkatalia kwa ajili ya kulinda mslahi ya Taifa.
Kwanini wasingetangaza tender kwa wazawa tu?
Ishu na Mo ni tofauti kabisa na ishu hii ya tender usichanganye mada,
Tuje kwenye kuwabeba wazawa,
Nakumbuka Magu aliwapambania sana wakandarasi wazawa alifika mbali Hadi aliwa organise wakaanzisha kampuni na akawapa kazi ila baada ya kufanya tender kadhaa ile kampuni ikiwa dhofu Hal, na hata Magu aliwachana live kwenye Annual Engineers Day ilifanyika Diamond Jubilee 2018,
Ni kwamba hapakua na msukumo wa ndani Bali walikua na msukumo wa nje kutoka kwa Magu,
Ishu ya mwisho,
Hiyo tender tumeambiwa kampuni 30 ziliomba, mbili tu ndo za wazawa kwa hiyo kama ingetangazwa kwa wazawa tu kama wewe unavopendekeza, basi zingeshindanishwa kampuni 2 tu, sasa pima mwenyewe wapi kuna chance kubwa ya kupata chaguo Bora ukiwa na machaguo mengi au machache,