Mwanzo

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
Mwanzo
1. Hapo mwanzo,katika hii sehemu tunayoishi,kulikuwa hakuna kitu.Halafu hii sehemu ikaanza kufukuta,kwa sababu ya nguvu iliyokuwa inaelekezwa hapa kutoka Paradise[Mbinguni],anakoishi Mwenyezi Mungu.

2.Ilikuwa inafukuta,lakini hakuna kitu chochote kilikuwa kinaonekana,huu ndio uliokuwa mwanzo wa kuundwa kwa nebula iitwayo ' andronover',ambapo ndipo lilipotoka jua hili linalotuangaza sasa.
3. Baada ya muda mrefu,miaka bilioni mia mbilvitu vikaanza kuoneakana,nebula ikaanza kujengeka,mvuke ukaanza kutokea,moshi,moto. Moto mkubwa ukatokea,ambayo ndiyo hiyo nebula.
4. Miaka bilioni mia tano badaa ya kuundwa,hii nebula ikaanza kumeguka na kutengeneza nyota.
5.Miaka bilioni tano iliyopita,hii nebula ikaitoa nyota ambayo ndio hili jua letu.
6.Mpaka sasa nyota nyingi ilikuwa zimeshatolewa,nazo zilikuwa zimeshatengeneza solar system zao,na moja ya hiyo solar system zilizokuwepo,ilipita karibu na hili jua lililotemwa. Ilipokaribia,kwa ajili ya mvuto wa gravity,kutoka kwenye hii solar system,moto ulitoka katika jua,na kuanza kulizunguka jua. Huu ndio mwanzo wa hizi sayari zetu,mwanzo wa Dunia hii tunayoishi. Sayari 12 ziliundwa.
7. Halafu huu moto uliotoka katika jua ukaanza kupoa,na kuwa jiwe,ndiyo hii Dunia tunayoishi.Dunia ilianza kupoa,na miaka bilioni mbili iliyopita,ulikuwa wakati wa volcano nyingi,na matetemeko ya ardhi.
8. Halafu Dunia ikapoa ,miaka bilioni moja iliyopita,maji yalitanda katika Dunia yote,bahari iliyoifunika Dunia yote,bahari yenye kina cha maili moja Duniani kote.
9. Halafu ardhi iliyokuwa chini ya bahari ipanda juu,kwa hiyo kukawa na bahari na sehemu za nchi kavu.Halafu Nchi ikameguka,continenti lilikuwa moja tu,lakini sasa likaanza kumeguka.
10.Ukitazama ramani ya Dunia,utaona jinsi ambavyo america kusini,na Africa,zinavyoonekana kwamba zilikuwa Bara moja zamani.
11. Miaka bilioni moja iliyopita ndio hasa mwanzo wa histiori ya maisha hapa Duniani,kwa vile Dunia ilianza kupoa,na ikawezekana maisha kuanza. Na maish yalianza katika inanda seas,bahari zilizokuwa zinaingia katika katika nchi,ambazo zilikuwa hazina kina kirefu,na ambapo mwangazo wa jua uliweza kupenyeza,na kuvifikia vile viumbe vidogo vilivyokuwepo pale ndani ya maji,viumbe kama amoeba.
13. Hivyo ndivyo maisha yalivyoanza Duniani,viumbe hivi vikakua,viakawa chura,vikatoka ndani ya maji,vikakuwa kuwa aina ya nyani,mpaka baadaye binadamu wakatokea.
14. Lakini kwanza ilibidi maji ya bahari yawe na chumvi zaidi kabal ya maisha kuanza.kwa sababu huu ni ulimwengu wa maisha ambao msingi wake ni chumvi,sodium chloride.
15.Maisha katika Dunia yalianzishwa sehemu tatu;katikati,yaani Europa na Afrika,Mashariki,yaani,Australia na Asia,na Americas na Greenland. Maisha kwanza yalikuwa mimea ndani ya bahari.Hii ni miaka milioni 500 iliyopita.
16. Miaka milioni 450 iliyopita yakatokea mageuzi,mimea ikabadilika kuwa wanyama wadogo,wanyama wa cell moja.
17.Zipo ishara kwamba mimea ilibadilika kuwa wanyama,lakini ishara hizi siyo dhahiri sana,kwa vile aina[species] mpya yoyote ya kiumbe inapoanza,inakuja ghafla. Kwa hiyo hakuna maana kuitafuta missing link,kiungo kilichokosekana , kati ya mimea na wanyama,au kati ya manyani na binadamu,kwa sababu link hizo hazipo,kwa sababu species zote zinaanza ghafla.
18.Miaka milioni 400 iliyopita kukaanza kuibuka wanyama wenye cell zaidi ya moja.Wanyama waligawanyika mapema katika aina nne,wala nyama,carnivorouos,wala majani,wala matunda,na wanaokula udongo[mud eaters],wanaokula vitu ambavyo havina uhai.
19.Sasa ndipo wakaibuka viumbe kama vile kaa,kamba ,pweza na wanyama wengi wadogo wa baharini.
20.Miaka 250 milioni samaki wakatokea. Wakati huu pia mimea ilianza kuota Duniani. Kwanza ilikuwepo mimea midogo tu kando kando ya bahari,lakini sasa miti jamii ya ferns ikaanza kuenea Duniani. Baada ya samaki kutokea baharini,huu ndio ukawa kikomo cha kukua kwa viumbe baharini. Kuanzia hapo,wakaanza wanyama kuishi nchi kavu.
21.Wakati mimea ilipoanza kuenea Duniani,CO2,carbon dioxide ikaanza kupunguka katika anga,haya yakawa ni masharti mazuri kwa wanyama kuanza kuishi nchi kavu.
Miaka 210 milioni iliyopita wakaanza kuwepo wanyama kama chura,buibui,nge,mende,nzige,panzi.
Kwa hiyo wakati huu,miaka milioni 180 iliyopita,ulikuwa wakati wa vyura na ferns.
22. Miaka 170 milioni iliyopita ikaanza kuwepo miti yenye mbegu. Miaka 140 milioni wakaanza kuwepo katika africa nyoka ,na mamba,mamba pia ni aina ya nyoka,na dinossaur.
Miaka 90 milioni iliyopita ikaanza kuwepo miti,kama vile,mibuyu. Miaka 33 milioni iliyopita,wakaanza kuwepo ndege[birds],ndege kama njiwa. Baadaye wakaanza kuwepo,katika America Kaskazini, wanyama kama vile faru,nguruwe,aina tofauti za nyani. Pia wanyama jamii ya mbwa.
23.Miaka milioni moja iliyopita baada ya vizazi vingi vya manyani aina ya lemur,wakazaliwa wanyama wawili ambao walionyesha kuwa na akili zaidi kidogo ya wanyama wengine. Hawa walikuwa ni lemurs wa Amerika Kaskazini. Ndio ulikuwa mwanzo wa viumbe ambavyo baadaye aliibuka mwanadamu,lakini ilkuwa ni baada ya hivi viumbe kuungana na vingine kutoka Afrika. Hawa lemurs wa Amerika walikwenda Asia,kupitia Bering Straits,kwenda Asia kupitia Alaska.Na kule,eneo la Mashariki ya kati walikutana na viumbe wengine kama hao wanatoka Africa.
24.
Kwa hiyo binadamu alinza katika wale wanyama waliotoka Amerika pamoja na Afrika. Lile kundi la Mashariki halikuchangia sana. Hawa walikuwa ni wanyama ambao ni wadadisi,wana akili kubwa zaidi,wanaonyesha furaha sana wakifanikiwa katika kazi yoyote wanayoifanya,walikuwa wanakula nyama.Walikuwa wanaishi katika miti kujisalimisha.
25.Baada ya miaka elfu moja,vizazi 70 ,wakazaliwa primates wawili tena ambao walionekana wana akili zaidi.Walikuwa wanaishi katika miti lakini pia wanaishi katika mapango,au kujichimbia chini. Wakawa wanaishi katika miti wakati wa usiku tu.Hawa walikuwa ni primates,walikuwa wanafana na binadamu zaidi ya wanyama wengine.Walikuwa wanao uwezo wa kutembea kwa miguu yao ya nyuma,kutembea wima.
Binadamu hawakutokana na gorilla na chimpanzee waliopo Afrika,isipokuwa katika wakati huu,zilitokea famila mbili za sokwe,ambayo moja iliendela kuwa binadamu,nyingine ikawa sokwe.
26.Lakini idadi yao ilivyokuwa inaongezeka,wakawa wanapigana sana kwa ajili ya chakula,na pia kwa ajili ya wanawake. Baada ya miaka 15,000,vizazi 600 ya hivi viumbe wakazaliwa mapacha wawili,ambao ndio walikuwa ndio binadamu wa kwanza. Hawa mapacha walikuwa na uwezo wa kupeana habari kwa kutumia sauti fulani na ishara,lakini walipojaribu kuwasiliana na wenzao,wakaona kwamba hawaelewani.
27. Ingawa hawa wanyama wote walikuwa wanao uwezo wa kutembea wima,hawa mapacha walizaliwa na kutembea wima toka mwanzo.
28.
Kwa hiyo tokea miaka milioni moja iliyopita,wale lemurs wa Amerika walipokutana na Lemurs wa Afrika,ilipita miaka 21,000,wakazaliwa hawa mapacha wawili,binadamu wa kwanza. Walipoona kwamba hawaelewani na wenzao,walihama na kwenda kuishi pembeni.
Kuanzia mwaka huu 2010,mpaka walipozaliwa wale mapacha imepita miaka 993,495.


 
Thanks dude, but I ain't buying none of it: I'd rather stick with the Genesis's version (they may both require a not so insignificant leap of faith, but its a choice between the lesser of two evils).
 
Ganesh,

The most informed scientific model has our universe as less than 14 billion years old (about 13.75 ±0.17 years), where do you get those hundred of billions of years? The Bhagavad Gita? The Vedas and its elephant on tortoises on top of tortoises supporting the world?

Unasema mwanzo kulikuwa hamna kitu, halafu kukaanza kufukuta, kufukuta huku kulitoka wapi wakati kulikuwa "hakuna kitu?"
 
Thanks dude, but I ain't buying none of it: I'd rather stick with the Genesis's version (they may both require a not so insignificant leap of faith, but its a choice between the lesser of two evils).

Dude,

Speaking of leaps of faith, I think the Bing Bang theory of the standard model (not without its problems of course, it wouldn't be science if it hadn't) is the one requiring the least in terms of leaps of faith. Significant less than Genesis. That is only to be expected given that Genesis is found in a book of faith and the Big Bang is a scientific theory. Not that sciente cannot be manipulated, but at least one is not asked to take things on faith.
 
Unataka kutuambia nn hapo?...au info tu mzee, una ajenda iliyojificha!!
 
Dude,

Speaking of leaps of faith, I think the Bing Bang theory of the standard model (not without its problems of course, it wouldn't be science if it hadn't) is the one requiring the least in terms of leaps of faith. Significant less than Genesis. That is only to be expected given that Genesis is found in a book of faith and the Big Bang is a scientific theory. Not that sciente cannot be manipulated, but at least one is not asked to take things on faith.

I'm not sure if what Ganesh has posited above qualifies as the Big Bang Theory, nevertheless, given that the Big Bang theory is derived from the deductive Scientific methodology (almost on its entirety), and given the truth that faith is instrinsic (and forms the basis of) to all forms of deductive reasoning, so at the end of the day it really breaks down to personal convictions (or taste if you will) as to which myth you want to believe in: the Big Bang Theory or the one presented in the Genesis. As they say: Choose your poison!
 
so at the end of the day it really breaks down to personal convictions (or taste if you will) as to which myth you want to believe in: the Big Bang Theory or the one presented in the Genesis. As they say: Choose your poison!

Co-sign.....
 
hadithi haditi, ...............hadithi njoo................., uongo njoo, ......................utamu kolea................, hapo zamani za kale...........................
 
biblia ina sema kwenye kitabu cha Mwanzo 1:1---- Hapo mwanzo alikuwepo neno
Hapana,
Hiyo haikuandikwa katika kitabu cha Mwanzo. Imeandikwa kwenye Gospel of John. Mwanzo inasema kuwa Mungu aliumba mbingu na nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom