Mwanza jijini vurugu tena sasa hivi .....

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,554
Hii vurugu inaendelea maeneo ya Nyakato National karibu na kituo cha polisi cha Mwatex, magari yamezuiliwa. Tutaendelea kuwajulisha nini chanzo cha vurugu, ila habari nyepesi ni kwamba kuna kundi fulani lililo rasmi linapigana na kundi jingine lililo rasmi. Nitawajulisheni baada ya kupata habari kamili vijana wangu ndo wameenda kwenye tukio.
 
Ukirudi bora useme pia hayo makundi yanahusianan na nini?
 
Karete umbea

Habari ni kwamba kuna kijana mmoja wa jeshi fulani amempiga mwendesha pikipiki pasipo kujua kuwa naye ni mtumishi wa he jeshi jingine. Hapa ninapoongea, gari la mkuu wa kituo limeishachomolewa vioo. Hakuna gari linalovuka eneo la tukio. Kama kuna waandihi wa habari mlioko Mwanza jijini tembelea kwenye tukio muweze kupata ukweli wa mambo.
 
Mod ...unganisha thread niliofungua na hii if you dont mind.

Katika pita pita zangu kitaa nikakuta magroup ya watu kibao maeneo ya Nyakato Nation nilipofika maeneo ya Mwatex ndio jamaa wakasema kuwa mwanajeshi alikuwa na pikipiki akapigwa na Mapolisi so raia ndio wakaingilia kati yaani ni mshikemshike polisi na risasi na raia na mawe yaani ni full balaa wakati narudi ndio ikawa issue mabomu ya machozi maeneo ya mwatex yamepigwa raia wanakimbizana na askari raia wanarusha mawe ni balaa hata risasi hazioni ndani, mpaka ikabidi turudi tuliko kuwa coz njia haipitiki. mpaka naingia mtamboni.
 
Majimbo yanayoongozwa na CDM utayajua tu! Hawa watu hawatufai kabisa!!
 
Habari hii ni sahihi kabisa ila kwa kuwa mi sio msemaji wa jeshi lolote ndo maana nimeileta kwa ufupi ili wasemaji wa majeshi hayo watueleze kulikoni.
 
Majimbo yanayoongozwa na CDM utayajua tu! Hawa watu hawatufai kabisa!!
Hapa si kesi ya CDM ni mfumo wa uongozi katika majimbo hayo. Vurugu zilizopita alisababisha mtu ambaye ni kada na kiongozi wa sisiemu ambaye amewekwa kwa maslahi ya rais. Kwa namna moja au nyingine hapikiki chungu kimoja na madiwani matokeo yake anafanya maamuzi pasipo kuwashirikisha wenzake. CDM imetoka wapi hapo.
 
  • Thanks
Reactions: Aza
Karibia utakufa kwa ujinga nenda hospitali iliyo karibu mapema wanaweza kusaidia kitu!
Umemuona eti. Vurugu sinahusikaje na CDM? Sasa hivi Kamanda Siro yuko kwenye tukio, Mkuu wa Mkoa yuko kwenye tukio lakini raia kwa kuungana na upande uloonewa hawatoki kwenye sehemu ya tukio
 
  • Thanks
Reactions: Aza
Habari hii ni sahihi kabisa ila kwa kuwa mi sio msemaji wa jeshi lolote ndo maana nimeileta kwa ufupi ili wasemaji wa majeshi hayo watueleze kulikoni.

Ni kweli mkuu kuna vurugu huku Mwanza maeneo uliyoyataja. Tusubiri taarifa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom