Mwandosya alimfanya Nini Kibaya Jk, Hatokisahau?

Status
Not open for further replies.
Ninacokijua ni kuwa mwandosya na JK walikorofishana kipindi ambacho walikuwa wanahudumu wizara ya maji kwa pamoja,kipindi hicho JK alikuwa ni waziri mwenye dhamana na Mwandosya alikuwa akihudumu kama Katibu mkuu wa wizara,seke seke ilikuwa pale ambapo Mwandosya alikuwa 'hakubali' kuongozwa na asiye na elimu tena dhaifu(ikumbukwe huu udhaifu unaosemwa leo haukuanza hapa,hii ni asili ya JK) .Ndipo siku moja katika kutofautiana kwao Mwandosya alishindwa kuvumilia na kuamua kumzabua makofi JK,NA HAPO NDIO ULIKUWA MWANZO WA KUWA PAKA NA CHUI NA SIO KWA SABABU YA USHINDANI WA URAISI KAMA WENGI WAZANIVYO

i heard but am not sure kuwa prof aliwahi kumuambia mkulu enzi hizo"you can be a president but not a professor"
 
Mkuu,
Kiukweli style yako ya uandishi ni burudani tosha!
Kweli najua kuna ban, na pole kwa zote zilizowahi kukukuta hapo kabla. Tafadhali naomba sana hata kwa PM unipe
undani wa hii kitu coz unaonekana unaujua fika.

Nilipata kupewa na mzee mmoja visa vingi sana vya jamaa kipindi kile cha 2005, huyo mtu alikuwa ni wale TISS wa
zamani wale ambao walikuwa recruited toka wakiwa skuli form 5 pale Dodoma Alliance (baadaye Mazengo,na sasa St.John's University). Huyu mzee alinambia jamaa hata TISS wenyewe walikuwa hawamtaki,hata ripoti ambayo
Mangula alimkabidhi Mkapa kuhusu jamaa ilikuwa mbaya sana ila inasemekana Mkapa alitishwa kuwa eti JK asipopita
chama kitamfia Mkapa mikononi mwake!

Hili la kum-black mail Mkapa nina uhakika nalo coz lilitoka kinywani kwa Mangula mwenyewe akimueleza huyu mzee
aliyenipa hizi habari by then(2005).Huyu mzee na Mangula wana uhusiano wa karibu sana coz baba wa huyu mzee
alikuwaga chifu huko Tukuyu na wakati Mangula anaenda kuanza kazi pale Mpuguso Middle School in the 1950s
alipokelewa na huyo chifu na kulelewa kama mwanae na hivyo Mangula na huyo mzee wa TISS (aliyenipa hizi habari)
wakawa kama ndugu wa damu although ni makabila tofauti.

Sasa kwa hili la chuki inayotokana na mwanamke silijui kwa kweli ila one thing I know ni kuwa JK ni mpenda wanawake sana! Once again mkuu tiririka hata kwa PM tu.

Safari ni Safari, hata ya kujua historia za watu mbalimbali ni safari tu!

Moderators, nashangaa kuona mmeitoa hii thread Jukwaa la Siasa. Hii inahusiana sana na suala la uraisi 2015. Na je, mmeitoa Jukwaa la Siasa kwa sababu zipi za msingi? Hii ni kauli iliyotolewa sasa, sio historia, na imetolewa katika nyanja za kisiasa. Msitukatishe tamaa wachangiaji wa JF. Tunaaamini kwamba mko hapa kuendesha JF without fear or favor. Kama sivyo basi kuweni wazi ili wengine tusipoteze muda wetu.


Na sasa kuhusu thread;

Nimekuwa katika mazingira ya karibu kuwafahamu sana Mwandosya na JK, na tatizo kati yao. Kabla sijasema mengi, nataka niweke wazi kwamba Mkuu Gwamahala amesema ukweli hapa kwa karibu 98%. Lakini sasa ngoja niwaeleze baadhi tu ya mambo kati ya JK na Mwandosya. Ila kwa kifupi nashangazwa sana kusikia JK akidokeza alifanyiwa ubaya na Mwandosya. Hiyo si kweli. JK hakupatana na Mwandosya kutokana na namna zao mbili tofauti kabisa kiutendaji.

Ugomvi wao

Kwa wanao mfahamu Mwandosya watasema yuko arrogant, lakini ukweli ni kwamba huyu jamaa ni mgumu sana wa kuvumilia kile nitakachoita "uswahili". Ukweli ni kwamba hamstahi mtu yeyote ambaye anafanya mambo kwa namna ya kiswahili swahili. JK alijua hili lakini hili si lililosababisha mambo kufikia mpasuko.

Kulikuwa na mambo madogo madogo yaliyochangia, mengi tu, na yalitokana na sytle ya uongozi wa JK na Mwandosya wakiwa Wizarani. Kwa mfano, kuna wakati tulikuwa Morogoro kwa ajili ya ufunguzi wa mradi wa wafadhili wa nje, JK akiwa mgeni rasmi kama Waziri wa Nishati. JK alichelewa kwa zaidi ya saa nzima bila kutoa taarifa, na Mwandosya akasema hatuwezi kumsubiri mtu ambaye hatujui amepatwa na nini. Kwa hiyo afafungua mradi kama kama mtendaji Mkuu wa Wizara. Baada ya masaa mawili hivi, JK aliwasili, wakati huo Mwandosya akiondoka. Mwandosya akamwambia JK hatukujua nini kimekupata hivyo nilifungua kama mtendaji mkuu wa serikali na sasa ndio naondoka. JK alitaka warudi tena, Mwandosya akamwambia haiwezekani, ni afadhali yeye JK asiende tena kule ukumbini, na kamwambia kama yeye JK anaenda ukumbini Mwandosya yeye asingerudi ukumbini. JK alikasirika sana, akiona Mwandosya anajifanya mjuaji.

Sasa huu hapa ni mfano wa mambo mengi madogo yaliyokuwa kati ya JK na Mwandosya.

Makubwa mawili yaliyosababisha wakorofishane kabisa ni yafuatayo;

Tuhuma magazetini dhidi ya Mwandosya

Hili lilikuwa mojawapo lililoua uhusiano wa JK na Mwandosya, kutokana na maudhi kati yao ya kila siku. Kipindi fulani, Mwandosya akiwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, alianza kutuhumiwa na magazeti fulani magazeti juu ya ubadhirifu wa fedha za TPDC. Kitu kilichomshangaza Mwandosya ni kwamba habari zilizoandikwa zilikaribia sana ukweli, yaani ukweli ulipindishwa ilikuufanya uwe uwongo. Sasa Mwandosya alikuwa na influence sana na TPDC na mara nyingi walifanya aliyowaagiza. Kwa mfano, inasemekana jengo la Mafuta Hose (ambalo sasa ni Mkapa House) ilikuwa ni bidii binafsi ya Mwandosya japo kwa kutafuta vifungu fulani fulani vya fedha ili kulijenga, japo halikuwa na bajeti halisi. Mwandosya alitaka TPDC liwe na jengo ambalo wangejivunia. Lakini alifanya hivi kupitia vikao halisi vya Board na kadhalika.

Basi magazeti yakawa yanatumia style ya namna hiyo ya utendaji wa Mwandosya kumchafua, na Mwandosya akawa anashangaa hizi habari nani anazitoa toka ndani? Kwa kuwa ni mtu aliyeheshimika pia ndani ya duruu za waandishi wengi, akawasihi wamtafutie chanzo cha habari zinazoandikwa dhidi yake, kwa kuwa zilionyesha kutolewa na mtu wa ndani mwenye madaraka.

Mwandosya alipata mshituko sana alipokuja kuambiwa na kuhakikishiwa ni nani alikuwa akiwa-feed waandishi wa habari habari zilizopikwa dhidi yake! Basi siku moja alikusanya magazeti kadhaa yenye habari za kumtuhumu, akaenda ofisini kwa JK. Huko tunaambiwa alimwekea JK magazeti yale mezani na kumuuliza kama alifurahishwa na zile habari, na kumwambia waziwazi amepewa ushahidi beyond doubt kwamba yeye ndiye chanzo cha habari kwa waandishi wa habari! JK alikuja juu lakini hakuchukua hatua, pengine akihofia ukweli ungejulikana zaidi yeye ndiye mambo yangemharibikia hata zaidi!

Mafuta machafu TIPER

Hiki ndicho kisa cha mwisho cha Mwandosya kuondoka Wizara ya Nishati. Kwa kipindi kirefu Tiper walikuwa wakilalamika chini chini kwamba walilazimishwa kukubali mafuta (crude oil) yasiyoendana na aina ya kiwanda cha kusafisha mafuta cha Tiper. Hatimaye hili suala lilifika kwa Mwandosya. Akawauliza kwa nini siku zote hawakumueleza, wakasema waliogopa. Akasema basi consignment itakapokuja nyingine, fanyeni tests zote, na mnipe taaarifa. Kama kawaida consignment ya crude ikafika, na ikaonekana kweli mafuta si ya kiwango cha crude iliyotakiwa Tiper. Mwandosya akajulishwa, na akamweleza JK kwamba alikuwa ametoa taarifa kwamba consignment isishushwe, na anatoa masaa 24 kwa meli iliyoleta hayo mafuta kuondoka mwambao wa Tanzania.

Sasa hapa ndipo ilipopendeza. JK akamwambia Mwandosya anamsihi aruhusu meli ipakue na kumpa onyo mwagizaji wa hayo mafuta machafu yasiyofaa Tiper. Mwandosya akamuuliza JK unafahamu ahali za Tpier kusafisha crude oil isiyofaa? JK akamwambia unajua kuna tatizo, maana mwagizaji wa hayo mafuta ni mtoto wa raisi!

Mwandosya alimjibu JK kwamba yeye JK ni Waziri, mtendaji katika sera za wizara, na yeye ni professional executive, wa utendaji wa kila siku, hivyo ni bora wakaheshimiana katika mipaka yao ya kazi ikiwa angetaka watende kazi pamoja. Mwandosya akaweka msimamo kwamba meli haitapakua na yeye kama katibu mkuu wa wizara anatoa agizo meli iondoke katika maji ya Tanzania!

Kilichofuata ni JK kwenda ikulu na kusema ana tatizo la kiutendaji na Mwandosya hawezi tena kufnya nae kazi! Mwandosya aliitwa ikulu, mbele ya raisi na Katibu Kiongozi akarudia kauli yake kwamba JK anaingilia maeneo yake kiutendaji. Kwa busara sana Mwandosya hakuzua suala la mtoto wa raisi kuwa ndio mwagizaji wa mafuta machafu!

Basi katibu mkuu kiongozi aliagizwa alipatie hilo suala ufumbuzi. Katibu mkuu akamwambia basi angemhamisha Mwandosya ampeleke Wizara ya Kazi au Utamaduni kama sikosei. Mwandosya akashanga sana, na akahisi kuna mchezo umefanyika kati ya Katibu kiongozi na JK ili kum-frustrate! Alimjibu Katibu kiongozi jibu ambalo hata yeye katibu kiongozi alibaki hoi. Alimwambia unajua katibu kiongozi, mimi profession yangu ni lecturer, na nilikuja serikalini nikiamini mchango wangu katika nyanja hii utathaminiwa. Ninaamini nimechangia kwa moyo kuiendeleza nchi yangu, lakini sasa kama mnaona mchango wangu hautakiwi tena ni bora mkawa wazi ili nirudi Chuoni UD. Mwandosya akasema yeye sio "career principal secretary", ambaye leo utamtoa Wizara ya Nishati, kesho umpeleke Wizara ya Utamaduni, na siku nyingine Wizara ya labda wanawake, na yeye akakubali tu! Akauliza leo hii ukinipeleka mie wizara ya kazi, nikafanye nini kule? Akasema yeye hatakuwa na mchango wa kutoa Wizara ya kazi, na ana uhakika wako watanzania wengine ambao watafaa zaidi yake kwenye nafasi kama hiyo, wapewe hiyo nafasi! Mwandosya akamwambia katibu kiongozi wala asihangaike kumtafutia wizara nyingine, yeye alikuwa anarudi chuoni kufundisha.

(Angalia hapa utasema Mwandosya ni arrogant - lakini huwa hakopeshi kukupa vidonge vyako!)

Basi katibu kiongozi akawa hana cha kufanya, maana raisi kamwambia ampelekee suluhisho! Basi akamwambia Mwandosya ukiondoka kwa namna hiyo kila mtu atajua kumekuwa na tatizo serikalini na kati yako na JK. Akamsihi Mwandosya na kusema kwa heshima yake yeye katibu kiongozi, basi anaomba achague wizara yeyote atakayo ili iwe ya kuondokea, akimaanisha uondoke taratibu sio ghafla.

Basi Mwandosya baadaye Mwandosya alimwambia katibu Mkuu Kiongozi ampeleke Wizara ya Viwanda na Biashara, ambako alikuwapo Msuya kama sikosei. Basi mabadiliko yakafanyika, katibu mkuu viwanda na biashara akahamishwa na Mwandosya akapelekwa pale. Mwandosya akawa pale nusu nusu, akiwa katibu mkuu na huku anafundisha UD, hadi alipoacha rasmi na kuwa full time UD.

Maisha nje ya serikalini

Akiwa UD, na kwa kushirikiana na Prof. Luhanga, Mwandosya alianzisha NGO iliyoshughulika na nishati na mazingira (CEEST). Katika Afrika Mwandosya akawa wanasayansi wa kwanza kushughulikia masula ya "climate change", na akawa anashiriki kama muwakilishi wa serikali katika mikutano ya kimataifa ya UN (inaitwa UNFCCC). Sasa huko Mwandosya akawa maarufu sana kwa uwezo wake wa kujenga hoja na kuchambua mambo. Akaheshimika sana katika duru za UN. Wakati wa mjadla wa Kyoto Protocol, Mwandosya akachaguliwa kuwa msemaji rasmi wa kambi ya "Group 77 and China" katika vikao vya UN. Basi ilikuwa kule Japan ambako Mwandosya akiliongoza kundi la G77 and China alikutana na Al Gore, ambaye alikuwa Vice President wa USA wakati huo. Al Gore alimzimia sana Mwandosya, akawa anasema Mwandosya ni moja wapo wa watu duniani wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kujadili hoja. Kuna wakati mazungumz ya Kyoto Protocol yalikwama, kutokana na msimamo ambao Mwandosya aliweka kwa ajili ya G77 and China. Al Gore akamwambia Mwandosya, "unajua Mwandosya, sasa haya makubaliano yanategemea wewe tu, kama ukikubaliana nasi basi tutakuwa tumelimaliza hili. Ni kama dunia nzima inakusubiri wewe ukubali". Mwandosya alikaa kimya kidogo, halafu akamjibu Al Gore, "nashukuru sana mheshimiwa makamu raisi kwa heshima uliyonitunuku. Unajua mwanzoni sikuelewa uzito wa sehemu yangu katika huu mjadala, na sasa wewe umenifungua macho, kamba dunia yote inaniangalia mimi. Kwa jinsi hiyo mheshimiwa raisi, basi inanibidi niwe mwangalifu hata zaidi ili dunia isije ikasema baadaye kwamba mimi ndiye niliyewauza katika makubaliano ya Kyoto!" Ali Gore akabaki kaduwaa!

Kurudi tena serikalini na siasa

Kutokana na umahili mkubwa alioonyesha katika mjadala wa Kyoto Protocol na UN kwa ujumla, Mwandosya alialikwa rasmi na US Department of State kwenda kutoa lecture katika vyuo vikuu maarufu kadhaa kule USA, kutia ndani Yale.

Kwa ufupi (muda unaisha) baadaye Clinton alikuja Tanzania, na inasemekana alimwambia Mkapa una mtu ambaye unapaswa kumtumia katika serkali yako - ni jembe la ajabu sana! Basi Mkapa alimwita Mwandosya akamwagiza anataka agombee ubunge. Mwanzoni Mwandosya alisita, na baadaye akakubali. Alipita bila kupingwa na moja kwa moja Mkapa akamfanya waziri - wakakutana tena na JK katika baraza la Mawaziri, safari hii wote wakiwa mawaziri!

Kwa kifupi, katika vikao vya baraza la mawaziri hata kuangaliana walikuwa hawaangaliani!

Uraisi

Ni kweli kwamba Mwandosya alionekana ndie kiongozi makini wa kuchukua uraisi baada ya Mkapa. Taarifa za Usalama wa Taifa zilimkandamiza sana JK, lakini JK aliweka wazi kwa Mkapa kwamba kama wangeondoa jina lake angegombea na chama cha upinzani - na akamwambia wazi Mkapa kwamba nakuhakiishia bwana Benjamini, nikigombea na upinzani nitashinda, hivyo chagua la kufanya!

Japo CCM hawakupendezwa kabisa na hili ikabidi tu wampitishe. Mengi haa yameshasemwa.

JK aomba kusuluhishwa na Mwandosya
Ukweli ni kwamba tangu mwanzo JK alijua wazi asingeweza kumtoa Mwandosya kwenyeBarza la Mawaziri, kwa sababu Mwandosya alishajenga sifa ya kuwa mchapa kazi sana, na hata mataifa ya nje yaliona hivyo. Na alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kupata misaada toka nje.

Basi JK aliwaona baadhi ya vigogo wazee wa CCM na kusema anaomba asuluhishwe na Mwandosya. Basi vigogo hao wazee wakaenda kwa Mwandosya na kusem raisi anaomba msuruhishwe. Sasa mwandosya akawauliza swali, JK amesema anaomba mie na yeye tusulruhishwe, amewaambia kwa ugomvi gani kati yetu? Mie wala sina habari kwamba nina ugomvi na JK, sasa yeye amewaambia tusuruhishwe kwa ugomvi upi? Wakamjibu nao hawajui ugomvi kati yao. Mwandosya akasema basi nashangaa, nyie mmekubalije kutusuruhisha ugomvi ambao hamjaambiwa? Sasa mtakuwa mnatusuruhisha kwa jambo gani? Akawaambia mie nawashauri rudini tena kwa JK, mkamuulize, eti, kwani wewe na Mwandosya mna ugomvi gani, maana yeye anasema hana tatizo kabisa na wewe!

Basi wale wazee walirudi kwa JK, wakamwambia, eti, mna ugomvi gani, maana Mwandosya amesema hana tatizo na wewe! JK akasema anakataa tu, anajua tuna tazizo. Wakasema basi wewe tuambie tatizo, JK hakueleza kitu!

Waze wakarudi kwa Mwandosya wakasema JK hajasema tatizo mlilo nalo. Mwandosya akasema, basi na mie siko tayari kururuhishwa na mtu amabaye hata hasemi tusuruhishwe kwa ajili ya tatizo gani!

Yakaishia hapo. Wakawa wanatenda kazi kama kawaida, hadi kufikia JK kutembelea kijiji cha Mwandosya kufungua NGO ya kulea watoto yatima iliyofunguliwa na mama Mwandosya.

Sasa leo hii ndio tunapata hii kauli ya JK!!!

Binafsi ninaamini kwamba kauli ya JK kuhusu Mwandosya, kama kweli JK kasema alichosema, inahusiana sana na mbio za 2015. Ila tatizo, ni kwamba JK hakufikiria kwa undani kabla hajaitoa. Kauli ya JK ina mambo makubwa nyuma yake.

Nimefupisha sana, manaona ni kisa kirefu. Nimewapa mambo ambayo ni rahisi sana kuthibitisha, kutia ndani na suala la mafuta ya TIPER, au waandishi wakongwe wa habari, au TPDC nk. Kazi kwenu.
 
Jamaa nasikia marafiki sana. Huwezi jua. Mmoja wa wahudumu wa JK wakati ni Waziri wa Nishati anasema walikuwa na utani sana mpaka wakati mwingine wakichukuliana ma-she wao wa mitaani.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom