Mwandosya alimfanya Nini Kibaya Jk, Hatokisahau?

Status
Not open for further replies.
Nakumbuka humu JF ulitoka uzi ulioeleza jinsi Kingunge Ngombale Mwilu alivyowashawishi wajumbe wa NEC CCM wamchgue JK japo wote wlikubaliana kuwa hana uwezo wa uongozi.
Uzi ule ulisema kati ya watu watatu waliopendekezwa kupeperusha bendera ya CCM, JK hakuwemo. Katika majina yalioyopendekezwa Prof. Mark Mwandosya aliongoza kwa kupata kura nyingi. Kingunge alisimama akasema (nukuu isiyo rasmi) " Ni kweli JK hana uwezo wa uongozi, lakini anachagulika. Ana mvuto. Kama tukimuweka Prof. Mwandosya CCM iwe tayari kukipoteza kiti cha urais kwenda kwa chama cha upinzani. Ni bora kuwa na rais dhaifu lakini kiti kikabakia kuwa cha CCM kuliko kutaka rais hodari lakini tukakosa kiti".
Maelezo haya yanatupa tafsiri mbili kuu. Prof. Mark Mwandosya ni mshindani wake mkuu kisiasa ndani ya CCM kuliko mtu mwingine yeyote. Bila woga wa kuukosa urais jina la JK lilitupwa katika kinyang'anyiro cha urais na la Prof. liling'ara.
Haijulikani mpaka leo kama hofu za Kingunge zinaweza kuthibitika kisayansi.
Jambo la pili ni kuwa uwezo mdogo wa kufikiri na kuongoza wa JK sio ajali ni jambo linalojulikana tangu hajaingia kwenye urais. Kilichomwingiza ikulu JK ni mvuto tu na sio sifa za uongozi. Mvuto hadi leo bado anao na udhaifu anao pia. Anaye sema leo kwamba uwezo wake wa kuchambua mambo ni mdogo, hatuambii kitu kipya, HE IS INVERTING A WHEEL WHILE DRIVERS ARE DRIVING CARS. Kwa maoni ya Kingunge yaliyoungwa mkono na wajumbe wa NEC ya CCM, ni afadhali kiti cha urais kikaliwe na picha nzuri kuliko kukikosa.
Kwa mtazamo wa Rais JK ( akitafuta legitimacy) hana jambo jingine zito alilolifanya kuthibitisha uwezo wake katika upongozi bali ni kumteua mpinzani wake ambaye ameshindwa kumsamehe dhambi ambyo hawezi kuitaja hadharani. Ikiwa dhambi hiyo hawezi kuitaja hadharani, watu wakaichambua, inatoa nafasi kwa wanajamii kujaza ombwe aliyoiacha. Yawezekana yeye JK ndiye mkosaji na amekwisha jihukumu mwenyewe.

I agree with you
 
Kabla hajaondoka madarakani ataongea Mengi bila kuujiijuwa....mabaya aliyowwafanyia...Kighoma Malima,amiri Jamal, hassy Kittine,Iddi Simba,Frederick Sumaye,.,Mwandsya,Salim Ahmed Salim na kumjeuka Lowwassa .....yeye anaona ni Sawa ....?

Huyo kwenye bold bado analia mpaka leo. Nadhani akipata nafasi huenda akalipiza. Time will tell
 
59841_466001220117572_4690602_n.jpg

Katika hii picha ,Kikwete anaogopa kumuangalia Mwandosya usoni; could it be a sign of guilty consciousness?
 
ASUNGILE MWAIFUNGA sikubaliani na wewe asilani, kwani Uchaguzi wa wagombea tokea CC kwenda NEC
  1. JK
  2. Salim A. Salim
  3. Tuluwaye Sumaye
  4. Prof Mwandosya
  5. na Abdallah Kigoda
NEC ndipo makundi ya yakashamiri kati ya CCM asili na CCM mtandao wakatoa majina matatu kwenda M/Mkuu
  1. JK
  2. S.A. Salim
  3. Prof Mwandosya
Hapo makundi yakafa yakaja Zone / Corridor za South, Central, Lake na ile North ilikufa baada ya Sumaye
Nataka kukwambia Kingunge hakubadili chochote hadi usiku wa manane wajumbe wanaitwa kuja chukua majina ma5 yatakayoingia NEC na mpaka yanatolewa JK hakuja kuchukua Matokeo

mm naona Vita hii isingekuwepo km Mwandosya asingechapisha Kitabu UOZA WA CCM wakati akijua JK ni Mwenyekiti wake BOFYA HAPA UOZA WA CCM

Nakumbuka humu JF ulitoka uzi ulioeleza jinsi Kingunge Ngombale Mwilu alivyowashawishi wajumbe wa NEC CCM wamchgue JK japo wote wlikubaliana kuwa hana uwezo wa uongozi.
Uzi ule ulisema kati ya watu watatu waliopendekezwa kupeperusha bendera ya CCM, JK hakuwemo. Katika majina yalioyopendekezwa Prof. Mark Mwandosya aliongoza kwa kupata kura nyingi. Kingunge alisimama akasema (nukuu isiyo rasmi) " Ni kweli JK hana uwezo wa uongozi, lakini anachagulika. Ana mvuto. Kama tukimuweka Prof. Mwandosya CCM iwe tayari kukipoteza kiti cha urais kwenda kwa chama cha upinzani. Ni bora kuwa na rais dhaifu lakini kiti kikabakia kuwa cha CCM kuliko kutaka rais hodari lakini tukakosa kiti".
Maelezo haya yanatupa tafsiri mbili kuu. Prof. Mark Mwandosya ni mshindani wake mkuu kisiasa ndani ya CCM kuliko mtu mwingine yeyote. Bila woga wa kuukosa urais jina la JK lilitupwa katika kinyang'anyiro cha urais na la Prof. liling'ara.
Haijulikani mpaka leo kama hofu za Kingunge zinaweza kuthibitika kisayansi.
HE IS INVERTING A WHEEL WHILE DRIVERS ARE DRIVING CARS. Kwa maoni ya Kingunge yaliyoungwa mkono na wajumbe wa NEC ya CCM, ni afadhali kiti cha urais kikaliwe na picha nzuri kuliko kukikosa.
Ikiwa dhambi hiyo hawezi kuitaja hadharani, watu wakaichambua, inatoa nafasi kwa wanajamii kujaza ombwe aliyoiacha. Yawezekana yeye JK ndiye mkosaji na amekwisha jihukumu mwenyewe.
 
' .....itakuwa ni aibu sana na ajabu pia utakuwa hujatenda haki kwa kumbagua ambaye hakukuchagua natolea mfano wangu katika uchaguzi uliopita,Prof Mark Mwandosya HAKUSHINDA LAKINI KWENYE SERIKALI YANGU NILIMUWEKA LICHA YA KUWA NILIFANYIWA MAMBO YA AJABU SANA AMBAYO NI VIGUMU KUYAVUMILIA LAKINI KAMA MWANASIASA LAZIMA UWE MKOMAVU....." Jakaya Kikwete ,DODOMA,22nd october 2012.

NOTE :- JK Tunayemjuwa na visasi kweli atakuwa alifanyiwa jambo baya ...hadi "alie" na mwandosya amsamehe hivi hivi kweli.......kwenye nchi nyingine angetakiwa kutoa maelezo aeleweke ...ili kama jambo alilofanya mwandosya lilikuwa baya watu wapime..
ISIJE IKAFIKIA MAHALI WATU WAKAMUHISI VIBAYA NA MASAHIBU YANAYOMKUTA MWANDOSYA..



- INTERGRITY YA MWANDOSYA IPO MAJARIBUNI KUWA MIAKA YOTE HII KIKWETE ANAMPA KAZI SIO KWA AJILI YA UWEZO WAKE WA KIUTENDAJI BALI KWA KUHOFIA MANENO YA WATU .....WANAOJUWA UGOMVI WAO...AU ULE MSEMO WA KUMUWEKA ADUI KARIBU UMMALIZE AU UMLAINISHE.....MWANDOSYA AFIKIRIE MARA MBILI...NDIO MAANA AMEPEWA KAZI JAPO NI MGONJWA???

NINAPATA MASHAKA MAKUBWA SANA NA UWEZO WA RAIS KIKWETE WA KU REASON HADI KUFIKIA KUTAMKA HAYA MANENO HADHARANI....BILA KUFIKIRIA MADHARA YAKE KWAKE KISIASA NA MAHUSIANO...AU NDIO KUTUBU?


Wekeni hiyo speech tuisikie kama ya Mulongo kwa youtube, naisi kama wahandishi makanjanja wamepika hii story. Me ni tomaso.
 
Mkuu Ukwaju, umeeleza vizuri unavyofahamu wewe. Maelezo unayotoa yanapingana na uzi aliotoa Zubedayo _Michuzi ya tarehe 27 July 2012 humuhumu JF wenye kichwa cha habari " Mh. Kingunge Ngombale Mwiru, Ushauri wako pale Chimwaga Pale Dodoma Umetufikisha hapa....."
Nakuomba mkuu, kwa ufahamu na maarifa yako pitia ukurasa huo. Watu wengi wanaoujua undani wameeleza baya hapa JF WHERE WE DARE TO SPEAK OPENLY
 
Wekeni hiyo speech tuisikie kama ya Mulongo kwa youtube, naisi kama wahandishi makanjanja wamepika hii story. Me ni tomaso.

Magazeti ya jana yote yalibeba hii habari ...akihutubia mkutano wa UWT....INGIA ONLINE . ..Tafuta..

IN Short nafikiri Kikwete akitoa hotuba bila kusoma huwa anaongea vitu ambavyo haviko coordinated kabisa....mnakumbuka alishawahi kuhutubia Nyerere squre akasema kuwa ....kwa namna wananchi wa Arusha wanavyomkera ...anatamani kuhamisha ofisi za kimataifa pale....na ni wakati huo ambao mikutano yote ilikuwa haifanyiki arusha ......akihutubia mkutano wa AfDB PALE AICC ...Akasema kuwa ...."...two years ago Arusha could not have hosted a meeting of this status"...just imagine mbele ya wageni wa dunia nzima ...sijui walimuelewaje ...na tishio lilikuwa nini kama Kampala yenye fujo iliandaa mkutano wa commonwealth....Je usalama wa Kampala unafika wa Arusha??? lakini tukagundua kuwa hayo maneno aliongea free style hayakuwa yameandikwa..

NAFIKIRI KIKWETE AWE ANASOMA TU HOTUBA ALIZOANDIKIWA KAMA ANAONA KICHWA KIMESHAANZA KULIWA...
 
Phillemon Mikael,

..unakumbuka alikwenda Mwanga, Kilimanjaro, akaanza kuwaambia wananchi kwamba wasiende mkoa wa Pwani kwasababu hakuna ardhi.

..bila kusahau ile hotuba yake kwa UWT alipotoa kauli ya matiti kuchirizika maziwa, na kuwaambia wanawake wa Tanzania waendelee kuzaa wasichana wazuri!!
 
Natamani siku moja kikwete aende BBC kwa hardtalk akutane na Stephen sackur!
 
Phillemon Mikael,

..unakumbuka alikwenda Mwanga, Kilimanjaro, akaanza kuwaambia wananchi kwamba wasiende mkoa wa Pwani kwasababu hakuna ardhi.

..bila kusahau ile hotuba yake kwa UWT alipotoa kauli ya matiti kuchirizika maziwa, na kuwaambia wanawake wa Tanzania waendelee kuzaa wasichana wazuri!!


Joka Kuu nakumbuka hii hotuba...ndio maana nafikiri stage aliyofikia kikwete....kuna kitu kina kula ubongo..!! Haiwezekani rais aongee jambo ambalo linavunja kabisa misingi ya katiba ya nchi inayosema,,"kila mtu anao uhuru wa kwenda mahala popote ilimradi asivunje sheria".........MANENO KAMA HAYO ANGALAU ANGEYATAMKA DIWANI WA MSOGA NINGEELEWA ...but kwa level ya rais kuongea vile ni kama kusahau kuwa wewe ndio rais wa wote ....hadi watu wanaoishi kwenye ukame na milima ya mawe kama WAPARE..............tena alitegemewa awaambie wapare wenye tabu ya ardhi waende Pwani kwenye ardhi tele!!
Miaka ya mwanzo ya 80' ,Mwalimu Nyerere alifanya ziara Kilimanjaro ...na katika kuhitimisha ..kama rais alionesha kusikitiswa na tatizo la uhaba wa ardhi Kilimanjaro ....kwani ardhi nyingi yenye rotuba ipo kwenye miteremko ya mlima kilimanjaro ...na kulikobakia kuna tatizo sugu la ukame na maji......yeye alitoa changamoto....kwa kuwaomba wataalamu wa JICA wakajenga mradi wa umwagiliaji wa LOWER MOSHI .....na vile vile ..akaagiza vijana wa Kilimanjaro wanaotaka wakajiandikisha majina wakapelekwa MOROGORO wakapewa ardhi.............
Hilo ndio suluhisho analotegemea kutoa mkuu wa nchi ...sio unaenda kuwahutubia watu wenye tatizo la maji na ardhi na kuwaambia ni marufuku kwenda PWANI...
Sio siri kuwa Pwani kuna mkakati wa dhati anaouratibu wa kuwashawi wageni [watanzania]wasipewe ardhi
......
 
Huwa siamini uwepo wa wachawi lakini kwa vimbwanga vinavyomiminwa kwenye uzi huu naanza kukubali taratiibu kuwa huenda wadudu hao wakawepo na kwamba hatima yao ikikaribia basi ni kama vile breki zinaachia; wanafunguka bila hiyana! Haya si mambo tuliyotegemea kuyasikia katika nchi yetu; Nadhani nimekuwa naïve kwa kiasi kikubwa kuhusu wanasiasa. Kama ni kweli, basi hawa watu ni balaa.
 
Mkuu siasa za Tanzania katika kipindi cha 2005 zilikuwa chafu sana, na ndio ulikuwa mwanzo wa chama na Tanzania kuporomoka na kuparaganyika. Kinyang'anyiro ndani ya CCM kiliendeshwa kwa njia za ajabu, kwa hiyo hadi kufikia 2010 hakukuwa na kazi yoyote ya kuendesha nchi isipokuwa kujilinda na kuwaangalia wengine. Tatizo ni kuwa watu wanamnyooshea JK vidole as if ni yeye peke yake alikuwa na harakati za kugombea urais, kulikuwa na wengine na wao harakati zao hazikuwa safi as they try to have us believe.

Si siri kuwa Prof Mwandosya (as arrogant as other people of his type) alikuwa na kauli za dhihaka sana dhidi ya JK alipokuwa Waziri, wakati yeye ni PS, hasa baada ya kile alichodhani kuwa waziri wake haenendi in a way that a minister shouldn't. Na ile kujiona kuwa yeye ni msomi na kusikitika kuwa na boss ambaye si msomi [Pamoja na kuwa prof alisahau kuwa we have a system ambayo mbunge yeyote anaweza kuwa waziri]The story of some girl, ni ndogo sana ambayo haiwezi kuwafanya wanaume na akili zai kuwa na ugomvi wa maisha kutokana na some girl, tena kimada sio mke. Sidhani kama hilo lina maana kujadiliwa.

Issue ilikuwa ni kwamba kutokana na u-arrogant wake he thought that JK did not have the education, character, personality to be president, lakini kutokana na kupenyezwa kwa rupia na zengwe, ikaonekana kuwa money talks, and money did talk. Kwa hiyo mtandao wakashinda na Asili waliodhani kuwa wanaweza kuongoza kutokana na sifa wakapigwa chini. Lakini kampeni aliyofanya na CCM asli Mark included ilimwaga sumu sana, na karibu yote aliyosema tunayaona sasa. JK ambaye ni mshindi katika mpambano pamoja na wanamtandao wengine kwa kawaida hawezi kuwa happy, nadhani kwa vyovyote unvayoweza kutafsiri, kumuweka Mwandosya kwenye cabinet, iwe ni kutokana na kum-comtain au vyovyote vile, ni uvumilivu.

Siasa za Mbeya zilikuwa simple, ilikuwa ni kama extension ya mpambano kati ya CCM mtandao na CCM asili. Lakini in the end swali lilikuwa nini kilikuwa na maslahi kwa Mkoa, kijana mdogo ambaye hajui lolote kuwa mbunge eti kwa sababu baba yake alikuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa ambaye hata uwaziri asingefikiriwa, au kumchagua Mwandosya aliyekuwa close kuwa rais, veteran mwenye elimu, personality, na rekondi nzuri kimkoa na kitaifa, ambaye ni manufaa kwa chama mkoa na mkoa in general. Pamoja na kuwa watu walihongwa baadhi ya watu waliona ni busara kumchangua Mwandosya anayefaa, na si kutumiwa kama uwanja wa mapambanao ya Mtandao na Asili.

Mwakyembe kila mtu anajua.

hapo kwenye red, mwandosya aliona mbali sana..ukiangalia hii nchi ilipo na kiongozi wetu wa nchi anavyoipelekesha tanzania sasa hivi na kwa vile alimjua jk toka wakiwa vijana alijua kua huyu jamaa asingeweza kuiongoza hii nchi so hili ni la ukweli na tumekuja kulidhibitisha wenyewe kwa macho yetu

hapo kwenye blue hizo tetesi ni kweli, mwandosya ana support kubwa sana mbeya so jk pamoja na kwamba anamjua mwandosya ni mbaya wake lakini bado kampa uwaziri ili kuwaweka watu wa mbeya kimya na wasupport ccm na ndio maana hata mwakyembe nae wamem contain...leo hii mwakyembe na mwandosya wakisema wahamie cdm basi mbeya nzima inaangukia cdm...so unaweza kusema JK hata juzi alivosema ni kwamba kaisema kwa uchungu kua mbaya wake ambaye mpaka leo hii si ajabu anamdharau lakini inabidi ampe uwaziri amuweke kapuni in the best interest ya ccm. kikwete sio mtu wa kutaja watu hadharani so mpaka kamtaja mwandosya ujue yamemfika mpaka shingoni inaelekea ana usongo nae.
 
Ninacokijua ni kuwa mwandosya na JK walikorofishana kipindi ambacho walikuwa wanahudumu wizara ya maji kwa pamoja,kipindi hicho JK alikuwa ni waziri mwenye dhamana na Mwandosya alikuwa akihudumu kama Katibu mkuu wa wizara,seke seke ilikuwa pale ambapo Mwandosya alikuwa 'hakubali' kuongozwa na asiye na elimu tena dhaifu(ikumbukwe huu udhaifu unaosemwa leo haukuanza hapa,hii ni asili ya JK) .Ndipo siku moja katika kutofautiana kwao Mwandosya alishindwa kuvumilia na kuamua kumzabua makofi JK,NA HAPO NDIO ULIKUWA MWANZO WA KUWA PAKA NA CHUI NA SIO KWA SABABU YA USHINDANI WA URAISI KAMA WENGI WAZANIVYO
 
Ninacokijua ni kuwa mwandosya na JK walikorofishana kipindi ambacho walikuwa wanahudumu wizara ya maji kwa pamoja,kipindi hicho JK alikuwa ni waziri mwenye dhamana na Mwandosya alikuwa akihudumu kama Katibu mkuu wa wizara,seke seke ilikuwa pale ambapo Mwandosya alikuwa 'hakubali' kuongozwa na asiye na elimu tena dhaifu(ikumbukwe huu udhaifu unaosemwa leo haukuanza hapa,hii ni asili ya JK) .Ndipo siku moja katika kutofautiana kwao Mwandosya alishindwa kuvumilia na kuamua kumzabua makofi JK,NA HAPO NDIO ULIKUWA MWANZO WA KUWA PAKA NA CHUI NA SIO KWA SABABU YA USHINDANI WA URAISI KAMA WENGI WAZANIVYO
 
Not that one......she was a toddler by then.......its a daughter of this man............for those who went for JKT in the 1980s will understand.......now don't ask me more questions it ends here..since it involves THREE armed men

Mkisi(2).jpg




Is this man not N. M....si??? Sitaki kumung'unya maneno huyu ni Afande Nelson Mkisi (Marehemu) Ana watoto kila mkoa ambako kuna makambi ya jeshi.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom