Wadau, nawasilisha kwenu; Jana mchana Januari 29, 2013 anayejiita mwandishi wa habari Joseph Ngilisho wa magazeti takribani yote ya UDAKU, ZANZIBAR LEO, DIRA YA MTANZANIA, SEMA USIKIKE, REDIO WAPO, REDIO SUNRISE N.K ambazo amekuwa akiziandikia kwa kutishia watu hatimaye amekamatwa na PCB kwa kuomba RUSHWA ya Sh. Milioni 2.
Hivi karibuni Ngilisho aliandika habari DIRA YA MTANZANIA akidai jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha linavuja kama mti wa muembe, kuta za kumbi mbalimbali zimechanika vibaya. Hata hivyo kabla ya hapo tayari alishaomba apewe Sh. Milioni 2 ili asiandike habari hizo.
Sasa jana ameweka mtego akanaswa hata hivyo alipojaribu kijinusuru na mikono ya DOLA alijikuta akikimbia na kutumbukia tena kwenye mikono ya DOLA yaani Ofisi za Usalama wa Taifa.
Hivi sasa amesomewa mashitaka yake na anatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni wafanyakazi wa Serikali.
Nawasilisha.