Mwandishi kortini kwa kupokea rushwa

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Mwandishi kortini kwa kupokea rushwa


Na Muhidin Amri, Songea

MWANDISHI wa habari wa kujitegemea mkoani Ruvuma, Bw Kwirunus Mapunda, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Ruvuma kujibu kosa la kushawishi na kupokea rushwa ya sh. 200,000, Mwandesha Mashitaka wa
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa, Bi. Maria Mwakatobe alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Bi. Janeth Mtega kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Desemba 22, mwaka huu katika mji mdogo wa Peramiho.

Aliendelea kudai kuwa, mtuhumiwa alishawishi na kuomba rushwa ya sh. 500,000 na kupokea kiasi cha sh. 200,000
kutoka kwa Padri Fidelis Mligo wa Shirika la Wabenediktine, Peramiho Songea Vijijini, ikiwa ni malipo ya awali ili asiendelee kuandika habari za ushirikina zinazohiusu taasisi hiyo.

Bi. Mwakatobe aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo huku akijua ni kosa la jinai, kushawishi, kuomba na kupokea rushwa chini ya sheria na. 15(1) ya mwaka 2007.

Mtuhumiwa huyo alikana mashtaka yote na yupo nje kwa dhamana, na kesi hiyo itatajwa tena tarehe Februari 1, 2011.
 
Siku za mwizi ni 40. Huyu Kwirinus Mapunda alikuwa akiandikia katika gazeti la Mwananchi. Tabia ya ke ni ya kitapeli tapeli ndiyo maana hata kwenye Songea Press Club waligoma yeye kujiunga. Amekuwa akitapeli hata wazee wa kijijini kwao. Huyu hafai kuandikia gazeti lolote kwa sababu ni fisadi wa habari. Anatuharibia fani yetu mbele ya jamii. Aende akalime gerezani, kwani naye amewahi kuwa afisa magereza.Sasa ataenda kuishi gerezani kama mfungwa! Character asassination is very bad. If you want money, you better ask, instead of creating and writing fake stories so as to threaten people in order to get money. Hili ni fundisho kwa sisi waandishi wa habari hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom