Mwandishi ashindwa kumhoji Mzee Arsene Wenger

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,722
3,366
Kuna video inamuonesha mwandishi wa habari akihaha kumkimbilia Kocha wa zamani wa Arsenal ya Jijini London, Mzee Arsene Wenger kwa ajili ya kupata mahojiano mara baada ya nguli huyo kutua Airport ya JK Nyerere kwa ajili ya michezo ya African football league (afL).

Kichekesho ni pale Mzee Wenger amekaa anamsikiliza ndugu Mwandishi. Yule mwandishi ameishia kujikanyagakanyaga mwenyewe na kuchekacheka huku akimwamkia Wenger kwa lugha ya Kifaransa cha kuchapia! Sasa nikajiuliza kulikuwa na ulazima gani wa yule mwandishi kutumia kifaransa wakati hata yeye mwenyewe hakijui swsw zaidi ya salamu. Au sijui alifikiri Wenger hajui kiingereza? Mzee wa watu akaona isiwe taabu akafunga mlango wa gari na kujiondokea!

Hivi hizi aibu za waandishi kwenye mahojiano zitaisha lini jamani? wanatutia aibu hawa watu.

20231021_171709.jpg
 
Kuna video inamuonesha mwandishi wa habari akihaha kumkimbilia Kocha wa zamani wa Arsenal ya Jijini London, Mzee Arsene Wenger kwa ajili ya kupata mahojiano mara baada ya nguli huyo kutua Airport ya JK Nyerere kwa ajili ya michezo ya African football league (afL)...
Acha hizo Dogo kaongea kifaransa vizuri tu, ule muda alliibia tu wageni walikuwa bize sana kuwahi hotelini, nampongeza sana yule Dogo Kwa ujasiri, angalieni kwenye content za kusema uzushi
 
Kwa muda mdogo aliokuwa nao mwandishi alijitahidi kutoonekana mbumbumbu.

Japo sijui kifaransa lakini maongezi yao yalianza na kuisha vizuri tu. Hakuna alieduawaa wala kuonekana kupotea kimaongezi baina ya muulizaji na mjibuji.

Kukosoa ni sawa ila tujifunze kutoa credit pale inapostahiki.
 
Acha hizo Dogo kaongea kifaransa vizuri tu, ule muda alliibia tu wageni walikuwa bize sana kuwahi hotelini, nampongeza sana yule Dogo Kwa ujasiri, angalieni kwenye content za kusema uzushi
Ni hawa wa TV online ambazo kila nyumba kuna ''mwandishi wa habari?'' Hili nalo ni janga na aibu nyingine kwa nchi yetu. Hawa watu wanaleta madhara kwenye akili za watu badala ya habari.
 
Kuna video inamuonesha mwandishi wa habari akihaha kumkimbilia Kocha wa zamani wa Arsenal ya Jijini London, Mzee Arsene Wenger kwa ajili ya kupata mahojiano mara baada ya nguli huyo kutua Airport ya JK Nyerere kwa ajili ya michezo ya African football league (afL).

Kichekesho ni pale Mzee Wenger amekaa anamsikiliza ndugu Mwandishi. Yule mwandishi ameishia kujikanyagakanyaga mwenyewe na kuchekacheka huku akimwamkia Wenger kwa lugha ya Kifaransa cha kuchapia! Sasa nikajiuliza kulikuwa na ulazima gani wa yule mwandishi kutumia kifaransa wakati hata yeye mwenyewe hakijui swsw zaidi ya salamu. Au sijui alifikiri Wenger hajui kiingereza? Mzee wa watu akaona isiwe taabu akafunga mlango wa gari na kujiondokea!

Hivi hizi aibu za waandishi kwenye mahojiano zitaisha lini jamani? wanatutia aibu hawa watu.

View attachment 2788337
mzee anajua kiingereza, ameishi uingereza sana, angeongea kimombo tu angeelewana naye. sio lazima kifaransa.
 
Kuna video inamuonesha mwandishi wa habari akihaha kumkimbilia Kocha wa zamani wa Arsenal ya Jijini London, Mzee Arsene Wenger kwa ajili ya kupata mahojiano mara baada ya nguli huyo kutua Airport ya JK Nyerere kwa ajili ya michezo ya African football league (afL).

Kichekesho ni pale Mzee Wenger amekaa anamsikiliza ndugu Mwandishi. Yule mwandishi ameishia kujikanyagakanyaga mwenyewe na kuchekacheka huku akimwamkia Wenger kwa lugha ya Kifaransa cha kuchapia! Sasa nikajiuliza kulikuwa na ulazima gani wa yule mwandishi kutumia kifaransa wakati hata yeye mwenyewe hakijui swsw zaidi ya salamu. Au sijui alifikiri Wenger hajui kiingereza? Mzee wa watu akaona isiwe taabu akafunga mlango wa gari na kujiondokea!

Hivi hizi aibu za waandishi kwenye mahojiano zitaisha lini jamani? wanatutia aibu hawa watu.

View attachment 2788337
Angemuuliza kama amekuja kumuona mama Samia.
 
wajifunze
na hilo ndo tatizo hawataki kujifunza.

kwa muda mdogo aliopata kama angemakinika na kazi angeshajaza kurasa za magazeti hapa bongo na hata nje ya nchi maana watu wanafatilia sana.

iyo nafasi ni adimu inaweza isijirudie maishani.
 
Mimi nimeweza kuona na kuisikiza hiyo video clip, lakini kwa bahati mbaya kwa kuwa sifahamu lugha ya Kifaransa sikuambulia kitu zaidi ya "bienvenue en Tanzanie"...

Sasa kwako mleta uzi, je wewe unakimudu Kifaransa?

Je, walipokuwa wanajibizana pale walikuwa wanaongea nini labda?

Ungetuwekea tafsiri ya walichokuwa wanaongea...

Back
Top Bottom