Mwanaume tumia akili zaidi ya hisia ukiwa na mwanamke

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Hisia hazitabiriki. Hisia zinabadilika haraka sana. Hisia zinaweka kufanya uharibu mambo. Hisia zitakufanya uhisi huna maamuzi kwa muda huo lakini akili ni maamuzi ya muda mrefu. Maamuzi ambayo kwa muda huo unaona ni mazuri na yatakusaidia kwa kipindi fulani. Mara nyingi huwa na matokeo mazuri.

Akili inakufanya ufikirie na uone madhara na faida ya matendo yako.

Ni sawa na unapohisi uchovu kwenda kazini, lakini akilini unajua kabisa ni muhimu kwenda kazini ili utimize malengo yako, lakini ukifuata hisia zako utakua na rekodi mbaya kazini.

Mwanaume usifanye kitu kwa kusema "Nilihisi hivi/nahisi itakua hivi”. Fanya/ toa maamuzi kamili baada ya kufikiria. Usikimbilie kufanya maamuzi. Mambo ya hisia waachie wanawake.

Unapotumia akili unamfanya mwanamke ajiachie kihisia. Mana anajua unaweza kuzimudu, lakini akiona unaingia kwenye hisia zake, ataficha ficha mambo mengine kwa kukuonea huruma, lakini haina maana kwamba wanaume tusiwe na hisia. Ila tuzijue hisia zinazotusukuma kufanya jambo.

Kuna muda mwanamke atakuchokoza au kukuambia maneno ya kukufanya umuone hana shukurani lakini hio ni hisia yake ya muda huo.

We usiingie katika ushawishi wake, wala usitake kujitetea mana ana akili na anajua umemfanyia mazuri lakini ni hisia zake tu za muda huo. Njia nzuri ya kumfanya atoke kwenye hizo hisia ni kumchombeza. Unaweza muambia “Sasa kwa sababu huna shukurani basi sikufanyii xxx tena kwa miaka kumi ijayo”. Au mpotezee tu.

Mwanamke anakupotezea, lakini una hisia naye sana za mapenzi.
Hivyo unajisikia umshawishi zaidi kwa vyovyote/ umtext kila saa au kumpigia. Achana na hizo hisia. Tumia akili na kuona ukweli kuwa huyo mwanamke hana mpango nawe au wewe tabia zako hazimshawishi mwanamke kukaa nawe. Tumia akili kubadilika.

Umempeleka sehemu ya kula lakini amefika na hajisikii na amenuna kabisa ili mbadili sehemu. Usiingie katika hisia zake na kutaka kubadili sehemu ili umfurahishe hisia zake. Bali tumia akili. Mchombeze kwa kitendo chake. Mwambie kitu kama “yani ungejua nilikuja kusafisha meza zote apa ili tupakute pasafi, ebu niache kwanza” na mada itabadilika, kutoka kununia mahali na mtafurahia.

Kuna muda mwanamke atataka kukupanda kichwani. Atakuonesha kukasirika au kukunja sura huku anakutishia lolote, lakini usiingie kwenye hisia zake za hasira. Tumia akili na uweke mipaka.

Mwanamke analalamika hana hela, ukiingia kwenye hisia zake utamuonea huruma na kutuma ela bila mpango. Ila ukitumia akili utachambua kwamba kwa malalamishi yake anahitaji pesa au anataka kuongea tu.

Mwanamke anakuambia mwanaume mwenye pesa ndo anampenda. Angalia huo mtego, hisia zako za mapenzi zisikufanye uhonge kiwanja kwa mwanamke usiyemjua ili tu umpate. Bali tumia akili.

Kuna muda mwanamke atakuonesha ukaribu. Hisia zake ni kuwa nawe muda huo. Tumia muda huo kumfanya ajisikie raha kuwa nawe. Tengeneza mazingira ya kuwa wapenzi.
Badala ya kuingia kwenye hisia zake za upendo ukajikuta unapenda zaidi ya yeye anavyokupenda. Ukajikuta mnapoteza muda kuongea vitu visivyoeleweka na umbea kwa kuwa mmeishiwa mada na kuishia kuwa marafiki.

Mwanamke ana huzuni/ analia, ni hisia ambazo sio lazima uingie umo. Nawe ukaanza kulia nae au nawe ukajaa huzuni nyumba ikakosa furaha. Bali tumia akili, kuna muda muache mwenyewe, kuna muda unamkumbatia tu na kuna muda unamwelewesha au mnaongea tu. Yote hayo bila kuingia kwenye huzuni yake.

Una hisia za mapenzi juu ya mwanamke. Sawa, lakini hilo jambo lisikufanye umfanye mwanamke malkia wako kabla hajathibitisha anastahili. Bali, tumia akili kuchambua matendo yake na sio maneno yake. Maneno yake yatakufanya uone mambo ni mazuri au usione mabaya.

Upo na mwanamke anakuumiza, lakini we ndo ushapenda.
Tumia akili kutambua kuwa wanawake ni wengi, unastahili furaha na una maamuzi juu ya maisha yako.

Ili kutumia akili, usijali sana hisia zako. Bali jua unachohitaji, unachokifanya na amini nafsi yako. Ukitumia akili kuliko hisia utapata urahisi kumuongoza mwanamke.
 
Upuuzi tu..yote hayo kusudi umfurahishe mwanamke!!!? Utapata pressure siku si nyingi.

Wanaume mm nawashauri usipoteze hata sekunde kumsoma mwanamke anataka nn sijui yupo na Hali Gani, utaishia kuwa mtumwa wake,. so ww ishi maisha Yako kuwa wewe kama wewe na mwanamke ndio ajipange kama anaweza ishi na ww ama la..akiweza abaki asipoweza apoteee..

Acheni kuabudu wanawake hao ni watawaliwa wa mwanaume Kwa mujibu wa maandiko.uliona wap boss anajifunza kuish na mfanyakaz wake na badala ya mfanyakaz kujifunza kuish na boss wake.😂😂😂
 
Wee Ishi Maisha Yako Yeye Ndo atafata Maisha Yako Na Taratibu zako ndo Maana Ya Mwanaume Kuwa Kichwa Cha Familia Sasa wee ukitaka Kujifanya LOVE BOY Kichwa kitauma huku uwaze Kutafuta Pesa huku uwaze Mwenzio Sijui Nini kanuna Bila Sababu za Msingi utkufa Siku zi zako Usitie Watu Ujinga
 
Naungana na wenzangu hapo juu..yeye ndo anatakiwa aingie kweny mfumo wako...ikishindikana achape lapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom