Mwanariadha wa zamani wa Olimpiki Oscar Pistorius aachiliwa huru

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
232
650
Mwanariadha wa zamani wa Olimpiki Oscar Pistorius ameachiliwa kwa msamaha kutoka jela nchini Afrika Kusini, baada ya kuwa kifungoni kwa takriban miaka 11 baada ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Pistorius alihukumiwa kwenda jela baada ya kumpiga risasi nyingi mpenzi wake kupitia mlango wa bafuni mwaka wa 2013, ambapo alijitetea kwa kusema 'alikuwa amemdhania kuwa mwizi'.

Pistorius, ambaye sasa ana umri wa miaka 37, amekuwa gerezani tangu Oktoba 2014, alipohukumiwa kwa mara ya kwanza. Alipatikana na hatia ya mauaji mwaka 2015 baada ya mahakama ya rufaa kubatilisha hukumu ya awali ya mauaji ya bila kukusudia. Hata hivyo, bado ataendelea kuwa chini ya uangalizi maalum hadi kifungo chake kitakapomalizika mwaka wa 2029.

Oscar mwenye ulemavu wa miguu (pichani), miguu yake ilikatwa alipokuwa na umri wa mwaka mmoja. Baadaye Pistorius alitengenezewa vifaa bandia na vilimsaidia akawa mwanariadha mashuhuri duniani anayejulikana kama "blade runner".

Katika Michezo ya Olimpiki ya Walemavu, alishinda medali nyingi za dhahabu. Kama hiyo haitoshi Oscar alishindana na wanariadha wasio na ulemavu kwenye Michezo ya Olimpiki ya London mnamo 2012.

images (71).jpeg
images (72).jpeg
 
Ila huyu alimuua sema sheria Ndio hivyo mnakuwa wapenzi kisha mnauana lo aangalie wasije kumuua huko mtaani
Miaka ikiwa kwa mwingine inaenda haraka kweli
 
Back
Top Bottom