Redpanther
JF-Expert Member
- Feb 23, 2019
- 2,813
- 3,769
Habari za wakati huu wapendwa na wanajamvi wenzangu wa MMU. Poleni kwa kazi na kwa wale walioenda kusali hongereni kwa ibada.
Nianze mkasa wangu juu ya huyu Baby mama wangu, Hapa juzi kati (wiki iliyopita) mwanadada aliyedai kuwa anaujauzito wangu na kunikabidhi kulea, alijifungua salama na Mtoto wa Kiume Mungu akajalia.
Anaishi kwao na mimi naishi kwangu, mwanzo alitaka aje akae nami tulee mimba pamoja nilikataa kwa sababu zangu binafsi. So ikabidi akae kwao tu, sasa tangu amejifungua nimekuwa nikituma pesa kwa ajili ya mahitaji ya msingi kwaajili ya mtoto na mama mtoto ukizingatia mtoto bado anategemea kila kitu kutoka kwa mama yake.
Kuna baadhi ya mahitaji ananitajia kimsingi mimi nayaona kama sio sahihi mimi kuhudumia kwa maana mahusiano mimi na yeye yaliisha na mimi nikawa nime move on na yeye akawa ame move mwanzoni kabisa mwa ujauzito. Sasa wakati kuna majukumu mengine naona kama napewa mzigo usio wangu, kwa mfano ananiambia nimlipie kodi ya nyumba akaishi kwake, ikiharibika simu hela ya matengenezo anapiga simu kwangu na niliwahi mpatia mara moja akatengeneza ila naona kama anazidi kuleta mazoea anataka nimpatie mtaji au nimfungulie biashara ili asinisumbue ishu ya matumizi ya mtoto , nilikataa nikamwambia nitatoa hela ya matumizi kila mwisho wa mwezi ila sio kukufungulia biashara.
Tokea hapo, ikitokea amepiga simu na nikawa sijapokea labda ikawa iko mbali au sikusikia anatuma mimeseji ya ajabu... Mara naona unakatika mauno juu ya huyo malaya wako ila simu ya mwanamke anayekulelea mwanao hupokei” sikujibu lolote ni nyingi tu mara unatumia pesa na malaya wako ila hela ya mtoto hutoi.! Pesa natoa ila yeye anaiingiza kwenye matumizi yake binafsi so namimi nakaza.
Sasa nimekuja kwenu, wanaume wenzangu ambao tunaohudumia hawa akina mama mnafanyaje ili kufanya hili suala la malezi kuwa rahisi na kupunguza mivutano na huyu mwana mama (Baby mama)
Naomba kuwasilisha, naombeni michango yenu wakuu