Mwanamke Anayewatesa Majirani Kwa Kelele za Ngono Ashindwa Kesi

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18
Wednesday, November 11, 2009

Mwanamke wa nchini Uingereza ambaye alikuwa akiwatesa majirani kwa sauti zake kali za kimahaba wakati akijamiiana na mumewe ameshindwa kesi ya rufaa kupinga kupigwa marufuku baada ya mahakama kusema sauti anazotoa si za kawaida ni kama sauti za mtu aliye kwenye maumivu makali sana ya kujeruhiwa au kuuliwa.

Mwanamke wa nchini Uingereza ambaye alipigwa marufuku na mahakama kuwasumbua majirani zake kwa kelele zake kali za kimahaba anazotoa kila anapofanya mapenzi na mumewe, ameshindwa kesi yake ya rufaa aliyofungua kupinga hukumu hiyo.

Mahakama ilisikilizishwa sauti anazotoa bi Caroline Cartwright wakati akifanya mapenzi na mumewe Steve Cartwright na kuungana na madai ya majirani wa mtaa wake ambao walisema kuwa kelele zake huwakosesha usingizi kwani ni sawa na za kelele za mtu aliyekuwa kwenye maumivu makali sana wakati akijeruhiwa au kutolewa roho.

Mahakama ilisikilizishwa dakika 10 za kaseti ya sauti iliyorekodiwa wakati bi Caroline na mumewe wakifanya mapenzi usiku na kuukosesha usingizi mtaa mzima.

Hata jirani yake mmoja ambaye ni nusu kiziwi hukosoka usingizi kelele hizo zinapoanza.

"Sauti anazotoa Caroline na miungurumo ya mumewe Steve si za asili ni kama vile wote wawili wapo kwenye maumivu makali sana", mahakama ya mjini Newcastle iliambiwa.

Majirani, wapita njia mpaka mfanyakazi wa posta walitoa malalamiko yao kuhusiana na kelele hizo.

Caroline na mumewe walipigwa marufuku na mahakama kupiga makelele au kuongea kwa sauti kubwa zinazotoka nje ya nyumba yao lakini Caroline Cartwright, mwenye umri wa miaka 48, alikata rufaa kwa misingi ya haki za binadamu baada ya kupandishwa tena kizimbani kwa kuivunja amri ya mahakama ya kutowasumbua majirani zake kwa kelele zake za kimahaba.

Akitoa hukumu jana jumanne, jaji wa kesi hiyo alisisitiza hukumu iliyotolewa mwanzo iendelee na Caroline ataendelea kupigwa marufuku kupiga kelele zake za kimahaba.

Caroline Cartwright aliiambia mahakama kuwa anashindwa kujizuia kutoa sauti anazotoa.

"Nimejaribu kujizuia sana nimeshindwa, nimejaribu hadi kuweka mto usoni kwangu kupunguza kelele bila mafanikio", alisema.

Hata hivyo jaji alitupilia mbali utetezi huo.

"Hatuna shaka kuwa kelele unazotoa zinaweza kusikika kwenye nyumba za jirani, mtaa wako na mitaa ya jirani", alisema jaji huyo.

Jaji huyo aliendelea kusema kuwa kelele hizo zinasababisha kero kwa majirani kwakuwa huendelea kwa masaa kadhaa.

"Hali hii inasababisha kero kubwa kwakuwa inatokea karibia kila usiku", alisema jaji huyo.

Mahakama iliambiwa kuwa kelele hizo huanza majira ya saa sita usiku na huendelea kwa masaa kadhaa wakati mwingine mpaka asubuhi.

Jirani yake wa mlango unaotizamana bi Rachel O'Connor aliiambia mahakama "Kelele wanazozitoa si za kawaida, siwezi kuzielezea, sijawahi kusikia kitu chenye mfano wake".

"Huwa naweka sauti ya TV yangu hadi mwisho chumbani kwangu lakini sauti zao huizidi sauti ya TV yangu na huwa nashindwa kusikia chochote toka kwenye TV", bi O'Connor aliiambia mahakama.

Mwanzoni mwa mwaka huu bi Caroline Cartwright alipewa onyo la miaka minne na mahakama kutowasumbua watu kwa kelele zake kokote kule nchini Uingereza.

Lakini alipandishwa kizimbani wiki chache baade baada ya kukiuka mara tatu maagizo aliyopewa na mahakama ndani ya siku kumi tangia alipoonywa.


Source: NIFAHAMISHE
 
DUh inaelekea huyo husband anatumbua vipele vyote na kukuna pande zote ndo maana huyu mama ana feeel kitu roho inapenda hahahaha
 
DUh inaelekea huyo husband anatumbua vipele vyote na kukuna pande zote ndo maana huyu mama ana feeel kitu roho inapenda hahahaha
Mkuu! yaani mama wa watu kajitahidi asizitoe hizo sauti ila imeshindikana kabisa.... Inaelekea kama unavyosema, jamaa anagawa dozi maridadi haswaaaa
 
DUh inaelekea huyo husband anatumbua vipele vyote na kukuna pande zote ndo maana huyu mama ana feeel kitu roho inapenda hahahaha

Husband is so strategic, he is touching every inch. Karibuni Bwawani Uporoto street Mwananyamala, kelele hizo tumezizoea.
 
A woman who was banned from making loud noises during sex has lost an appeal against her conviction. Caroline and Steve Cartwright's love-making was described as "murder" and "unnatural" at Newcastle Crown Court.
Neighbours, the local postman and a woman taking her child to school complained about the noise.
Mrs Cartwright, 48, from Washington on Wearside, lost the appeal against a conviction for breaching a noise abatement notice.
She argued she had a right to "respect for her private and family life" under Article 8 of the Human Rights Act.

o.gif
start_quote_rb.gif
We are in no doubt whatsoever about the level of noise that can be heard in neighbouring properties, in the street and in the back lane.
end_quote_rb.gif



Recorder Jeremy Freedman, Newcastle Crown Court


But Recorder Jeremy Freedman, sitting with two magistrates, rejected her claim that she could not help making the loud noise during sex.
He said: "We are in no doubt whatsoever about the level of noise that can be heard in neighbouring properties, in the street and in the back lane.
"It certainly was intrusive and constituted a statutory nuisance. It was clearly of a very disturbing nature and it was also compounded by the duration - this was not a one-off, it went on for hours at a time.
"It is further compounded by the frequency of the episode, virtually every night."
'Shouting and screaming'
Next door neighbour Rachel O'Connor told the court she was frequently late for work because she overslept having been awake most of the night because of the noise.
She said: "The noise sounds like they are both in considerable pain. I cannot describe the noise. I have never ever heard anything like it."
The court heard Sunderland City Council recorded levels of up 47 decibels.
Mrs Cartwright was appealing against the abatement notice, which was imposed in November 2007, and a subsequent Asbo, banning the couple from "shouting, screaming or vocalisation at such a level as to be a statutory nuisance".
She has since been accused of three counts of breaching the Asbo, but has denied the charges and will stand trial at Newcastle Crown Court on 14 December.
 
dah, uhuru wakousiwanyime wengine uhuru,,,kuna hsidasana hapo katika kutafsiri kati ya uhuru wake wa kufurahia maisha ikiwemo mapenzi na uhuru wa majirani kuwa na haki ya mazingira tulivu!

wakae kwenye nyumba sound proof?
 
aliyerekodi alikuwa wapi, alikuwa na hali gani ilihali alijua jamaa wanamegana.......!!!!!!!
majuu kweli hamnazo
 
Ah! watu na raha zao jamani nyie mpaka na vinasa sauti si ndio kukoseshana amani huko? Huenda mzee akimega mashine inakoleza ndio maana bi mkubwa anakosa uvumilivu. Walitakiwa wawashauri watengeneze nyumba yao iwe na sound proof kuepuka hiyo miguno kuliko kwenda kushitakiana. Duh! dunia iko mambo mingi sana..
 
Waliaji wenyewe ndiyo hawa hapa.

Ahhhh, Uhhhhh, ............... Mweeeeee!!!!! Hadi kiziwi anakosa usingizi? Ni kituko kama Goalkeeper wa Mozambique jana.
caroline-cartwright.jpg
 
kweli duniani kuna mambo hizo nyumba zimekaaje mpaka makelele yanawafikia?
Hapo sasa hata mimi sipati picha nijuavyo mimi nyumba za majuu zimetengana sio rahisi kusikia labda aache mlango wazi na wako uwe wazi unaweza sikia vinginevyo haiwezekani tena mtaa mzima labda kama wanafanyia nje
 
Ha ha ha Gollie wa Mozambique... angekua mzaliwa wa Uganda wangemnyonga... Duh ana-display U-gay wake hadharani...
 
Back
Top Bottom