Mwanamke anayetuhumiwa kuhusika na mauaji adaiwa kuuwawa akiwa mahabusu

Kesho tr.24 Feb wanapelekwa tena mahakamani ngoja tusubili endapo wataendelea kubaki kimya kuthibitisha hizi habari kesho kitaeleweka lakini wanaweza kutuzuga anaumwa amebaki gerezani hii inawezekana ngoja tusubili ni masaa tu.
 
toka lini mahabusu akahojiwa na askari magereza? kuna ukweli gani hapo?
 
Mtuhumiwa wa mauaji adaiwa kufa gerezani
Ni mke wa mhindi anayedaiwa kuua

Waandishi Wetu

UTATA umetawala kuhusu maisha ya mke wa mfanyabiashara Vinoth Praven (23) raia wa India aitwae Komal Katakia (22), ambaye anashikiliwa na Jeshi la Magereza katika gereza moja jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara Abdulbasiti Abdallah (21), huku taarifa za awali zikieleza amefariki dunia na zingine zikisema kuwa yu hai gerezani.

Habari za kifo cha Komal zilianza kuenea jijini hapa kuanzia juzi Ijumaa huku baadhi ya watu wakidai kuwa ameuawa na wengine wakidai kuwa amejinyonga, lakini msemaji wa Jeshi la Magereza, Omari Mtiga alikanusha taarifa hizo akidai kuwa amewasiliana na maafisa wa magereza ambao wamemuhakikishia kuwa hawana taarifa hizo.

Habari kutoka kwa jamaa wa karibu wa Komal zinadai kuwa amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kitambaa cha kichwa (mtandio).

"Komal amekufa tangu juzi (Ijumaa) lakini tunashangaa mpaka sasa serikali haijataka kutoa taarifa za kifo chake na hata magazeti hayajaandika" alisema mmoja wa jamaa hao na kuongeza.

"Mimi nilidhania kuwa magazeti ya leo (jana) yangeandika taarifa za kifo hiki, lakini nimeangalia hakuna gazeti hata moja lililoandika, sijui tatizo nini".

Alipoulizwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema hawezi kuzungumzia kifo hicho kwani mtuhumiwa huyo hakuwa mikononi mwao.

"Siwezi kuzungumzia habari za kifo cha mtuhumiwa huyo, waulizeni magereza kwani hizi ni mamlaka mbili tofauti" alisema Kamanda Kova na kuongeza:

"Ok, sisi tukisema amekufa halafu magereza wakikanusha kuwa hajafa? Lakini pia mpaka sasa hatujaletewa barua kuwa amekufa au la, kwa hiyo hatuna ushahidi".

Juhudi za kuwapata maofisa wa magereza kuthibitisha kifo hicho hazikufanikiwa baada ya ofisa mmoja kupigiwa simu, ambapo mara baada ya kuulizwa swali alikata simu hiyo na kukataa kupokea tena kila alipopigiwa na mwandishi.

Hata hivyo baadhi ya vyanzo vya habari hii vimedokeza kuwa mtuhumiwa huyo amekufa na maiti yake imepelekwa Hospitali ya Rufaa Muhimbili ikiwa na makovu.

"Inadaiwa kuwa amekufa kwa mateso, kwa sababu mwili wake umeharibika kwa mateso na una makovu mengi," kilidokeza chanzo cha habari.

Febuari 8 mwaka huu Polisi jijini Dar es Salaam walimtia mbaroni raia wa India, Vinoth Praven (23) na watu wengine wanne akiwamo mke wa raia huyo, Komal Katakia (22), kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara Abdulbasiti Abdallah (21), ambaye mwili wake ulikutwa ndani ya begi la nguo katika Jengo la Harbour View, Mtaa wa Samora.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka Emma Mkonyi mbele ya Hakimu Mkazi Eva Nkya kuwa, Februari 2 mwaka huu saa 3:15 usiku katika mtaa wa Kipata Kariakoo, washitakiwa walimuua Abdallah.

Hata hivyo washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji hadi mahakama kuu.

Mwendesha mashitaka alisema kuwa upelelezi bado haujakamilika na Hakimu Nkya aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 24 mwaka huu itakapotajwa tena.

Wahindi hao ambao walirudishwa rumande, wanadaiwa kumuua Abdallah kwa kumkatakata vipande na mwili wake kuuweka kwenye begi la nguo.

Baada ya kuuweka mwili huo kwenye begi la nguo, washitakiwa hao wanadaiwa kuutelekeza kwenye gari dogo na kisha kulipaki katika Jengo la Harbour View (zamani J Mall) ghorofa ya pili.

Katika gari hilo pia kulikutwa na mfuko mdogo wa Rambo uliokuwa na kandambili zinazodaiwa kuwa ni za marehemu, nguo, kisu na bomba la sindano.

Mwili huo uligunduliwa na walinzi waliokuwa lindoni katika jengo hilo baada ya kusikikia harufu kali na kuanza kufuatilia kisha kutoa taarifa polisi.
 
Kama hayo yanayosemwa ni kweli, basi jeshi la polisi linajidhihirisha kuwa halina wataalamu wa upelelezi katika mashitaka ya jinai, kuna habari kuwa wanaopelekwa masomoni nje ni wale wenye vyeo vya juu na wanaporudi wanaishia maofisini bila ya kufanya kazi walizosomea.
 
Back
Top Bottom