Mwanakijiji, huu ni UDINI pia...

Status
Not open for further replies.
The Boss,kwa nini hautaki pengo ajishughulishe na hili swala,au hauelewi mahusiano yake ya kikazi na huyo padri aliyeuwawa? Na mbona sijawahi kukusoma ukipinga maelekezo ya viongozi wa serikali kuwaomba viongozi wa dini kuhakikisha amani na upendo vinadumu katika nchi yetu? Au hapa huwa hauoni kama wanaamishia majukumu yao kwa watu wasio husika?

Na mwisho,nje ya mada kidogo.mamlaka ya viongozi wa dini hayaishii kwa waumini wao pekee bali kwa jamii nzima,hasa ukizingatia wanawajibika kuhakikisha jamii nzima inafuata imani zao kutoka na ubora na ukweli wake kulinganisha na imani zingine.
 
Kwa kuwa tukio la Sheikh Soraga liko Pending na haijulikani ni nani muhusika, na Paroko wa mpendae Fr Mkenda tukio la kujeruhiwa kwake nalo liko Pending then kuuawa kwa huyu Faza kutaliingiza taifa katika majaribu makubwa. Mchungaji wa Buseresere tunaweza kusema ugomvi wa kuchinja, lakini kwa hawa mapadri wawili tutasemaje?? Kama polisi wangefikia suluhu za high profile incidences za kidini watu wangeweza kutulia na kusubiri, sasa tusubiri nini wakati jeshi letu haliwezi kuwapata hawa wauaji, mtu atawaza ni heri kuchukua sheria mkononi.

Tabia ya kushindwa kutatua matatizo na kero ndio alama ya utendaji wa serikali ya awamu ya nne. Ikumbukwe hata bungeni kuna kesi na miongozo kibao imekaliwa na spika wa bunge bila kutolewa uamuzi ambazo zimesababisha vurugu bungeni,,, huu ni mfano tu wa madhara yanayoweza kutokea kama matatizo hawafikiwi suluhu kwenye jamii
 
Perseption kama hizi ndo zinafanya daily watu wanachinjwa...we try too hard kujifanya hatuoni tatizo
Sio kwamba napinga kwamba kuna tatizo la udini,ila is vyema kulikuza namna hii,kwa nini naona kila mtu anakimbilia conclusion kwamba waislamu wanahusika na hayo mauaji? Jakaya aliishawahi kusema kuna viongozi wa dini wanashiriki biashara ya madawa ya kulevya,what if this could be a reason? Nachoomba mimi ni uthibitisho tu basi,lakini sijasema kwamba hayajasababishwa na msukumo wa kidini.
 
uhalifu na vurugu zinazojitokeza ni zao la serikali dhaifu,sasa kila mtu akianza kuomba muongozo wa Viongozi wa DINI yake,unafikiri hii nchi itakalika?
Ni ukweli ulio dhahiri kwamba nchi haina serikali, inajiongoza yenyewe. Na kama kuna serikali basi ni hiyo dhaifu uliyoitaja The Boss, na kwa uelewa wangu serikali dhaifu katu haiwezi kuchukua hatua.

Hebu tujikumbushe matukio ya huko nyuma halafu tuseme ni hatua gani zilichukuliwa na serikali. Yalichomwa maduka ya wakristo huko Zanzibar, zikachomwa bar na bucha za nguruwe, bucha zikachomwa pia Songea, wakaanza kuchoma makanisa huko Zanzibar, wakachoma makanisa mbagala, wakafanya jaribio lakumuua kwa risasi father Ambrose, wakaua mchungaji huko Geita na sasa wameua Padri huko Zanzibar.

The boss, unaweza kutaja hata mtu mmoja aliyeshitakiwa au kufungwa kutokana na matukio haya? Baada ya kuchomwa kwa makanisa Mbagala tulitarajia wale wahuni wote walioshiriki katika uchomaji ule wangekamatwa na kushitakiwa, cha ajabu ukisoma mashitaka yanayomkabili shehe Ponda si ya uchomaji wa makanisa bali ni ya uchochezi uliopelekea uvamizi wa kiwanja cha Manji kule Chang'ombe. Yaliyofanywa dhidi ya wakristo yameachwa yaendelee. Vyombo vya habari vya kiislam na mihadhara inayoendeshwa ya kuwashambulia na kuwakashifu wakristo vimeachwa viendelee.

Shehe Ilunga hivi sasa amewatangazia waislam wawaue viongozi wa wakristo. UShahidi wa video upo, hajawahi kukamatwa. Sasa wakristo waende wapi kwa mtizamo wako? Maana hiyo serikali dhaifu ina polisi wa kukamata na kuwaua waandamanaji wa chadema lakini haina polisi wa kuwakamata kuwashitaki waislam wanaochochea vita nchini.

Unafikiri wakristo wafanye nini? Je waendelee kuvumilia kuona viongozi wao wakiuawa tena kwa maagizo ya shehe wao ambayo yapo dhahiri hadi kwenye youtube na hachukuliwi hatua? Unadhani uvumilivu wa wakristo utakuwa na matunda gani bora katika miaka mitatu ilyobakia ya utawala dhaifu uliopo madarakani? Sioni msaada wowote unaoweza kutolewa na viongozi wa serikali wasio na hata tone la hekima wala busara ya kuongoza nchi.

Yafaa turudi kwa viongozi wetu wa dini tuwatake nao watoe matamko sawasawa na hayo yanayotolewa na akina shehe Illunga. Enzi za Petro rudisha upanga wako alani, nafikiri zifike mwisho sasa.
 
Last edited by a moderator:
Naomba tusianze kutafuta wauwaji kwa kuhisi tu,
hivi nani anajua ikiwa padri hakuwa na maadui
hivi ikiwa yule mtawa aliyefumaniwa angeuwawa na mfumanizi wake,
si mngekuja na maneno haya haya kwamba waisilamu wamuua mtawa kwa chuki
sasa msihukumu, padri mushi nae alikuwa ni binadmu kama wengine,
huenda ni maadui zake wame mmaliza kwa sababu zao binafsi tusizozijua.
tuiache serikali ifanye kazi yake
 
The Boss,kwa nini hautaki pengo ajishughulishe na hili swala,au hauelewi mahusiano yake ya kikazi na huyo padri aliyeuwawa? Na mbona sijawahi kukusoma ukipinga maelekezo ya viongozi wa serikali kuwaomba viongozi wa dini kuhakikisha amani na upendo vinadumu katika nchi yetu? Au hapa huwa hauoni kama wanaamishia majukumu yao kwa watu wasio husika?

Na mwisho,nje ya mada kidogo.mamlaka ya viongozi wa dini hayaishii kwa waumini wao pekee bali kwa jamii nzima,hasa ukizingatia wanawajibika kuhakikisha jamii nzima inafuata imani zao kutoka na ubora na ukweli wake kulinganisha na imani zingine.

Kuaminika na kuheshimika kwa Viongozi wa DINI kuko kwenye wafuasi wao tu.
Ili Waislam wasiopenda vurugu washiriki kikamilifu na wakristo kupambana na wahuni wachache
ni bora kuwepo na Kiongozi wa KITAIFA anaeongoza haya na sio kiongozi wa wakatoliki
 
The Boss umekuja ku-water down thread ya Mwanakijiji? Kwa nini usingemfata kule kule kwenye thread yake? Unaongeza risk ya wengine kula ban manake tangu yale mashetani ya kiislam yamuue padri huko znz wengine tumejitahidi kunyamaza...
 
Naomba tusianze kutafuta wauwaji kwa kuhisi tu,
hivi nani anajua ikiwa padri hakuwa na maadui
hivi ikiwa yule mtawa aliyefumaniwa angeuwawa na mfumanizi wake,
si mngekuja na maneno haya haya kwamba waisilamu wamuua mtawa kwa chuki
sasa msihukumu, padri mushi nae alikuwa ni binadmu kama wengine,
huenda ni maadui zake wame mmaliza kwa sababu zao binafsi tusizozijua.
tuiache serikali ifanye kazi yake

iwapo serikali imeonekana kushindwa kufanya kazi yake ......way foward ni nini?
 
Yafaa turudi kwa viongozi wetu wa dini tuwatake nao watoe matamko sawasawa na hayo yanayotolewa na akina shehe Illunga. Enzi za Petro rudisha upanga wako alani, nafikiri zifike mwisho sasa.

Hesabu za Kikristu hazikokotolewi kwa njia za kiislamu. Upanga urudishwe alani kwake. na viongozi wetu hawahitaji kukurupuka na matamko. Wanachukua hatuahili stahili kulingana na mazingira na ukubwa wa tatizo. Kwa mbinu na njia za Kikristu zenye kulenga kudumisha amani.
 
Aliyesema kwamba wauaji wa padre Mushi ni waislam ni nani?
Chochote wakachosema
bado jukumu la kukamata wahalifu na kuwapeleka mahakamani lipo kwa serikali....

Pengo sio Nyerere,yes ni sad Padri kauwawa but si kwamba waluiomuua huyo Padri wana
baraka za waislam wote wa TZ....sioni umuhimu wa Kauli za viongozi wa dini kwenye 'POLICE CASE'
 
Hali siyo swari tena, nchi haitawaliki kabisa The Boss ni kama viongozi wote wako honey moon inafika wakati wa watu kwenda kwenye nyumba za Ibada huku wameweka silaha kibindoni, Nchi ingekabidhiwa jeshi tu tujue moja.
 
Last edited by a moderator:
iwapo serikali imeonekana kushindwa kufanya kazi yake ......way foward ni nini?

Way forward ni njia yeyote ile inclusive
ambayo waislam wengi na wakristo wengi wataiunga mkono
na sio kumuomba Pengo atoe muongozo...Pengo ni kiongozi wa wakatoliki
waislam wanaopinga UDINI huu na vurugu hizi utawatenga ukimleta Pengo kwenye picture
Bora Pengo ajilete mwenyewe na sio kuombwa na Influential Writer kama Mwanakijiji
NI HATARI MNO,na ni udini pia
 
Umefanya kosa kubwa sana kuongelea maneno ya mwanakijiji bila kuya quote wengine hatujui pa kuyapata ili tuweze kumhukumu. Kutokana na upungufu huo niacheni nidai tu hapa yawezekana mwanakijiji anamtaka Pengo aseme kitu ili kutuliza hali ya joto isipande kwa waumini wake. Viongozi wa dini wanasikilizwa sana kuliko mtu yoyote katika jamii kuliko hata raisi wa nchi.
 
Pengo hata awe na busara za aina gani ni kiongozi wa DINI ,na 1.UHALALI wa Pengo unaishia kwa wafuasi wa dini yake tu......hata kama viongozi wa KITAIFA hawafanyi wanayotakiwa kufanya, bado 2. Pengo Hawezi ku Play role ya Kiongozi wa Taifa hasa kwenye vurugu za kidini kama hizi...

kwa hizi comment 2 sioni tofauti kati yako na mwanakijiji
 
Infact kuna baadhi ya hoja uko sawa kama kuendelea kwa vitendo hivi bila serikali kuchukua hatua ni uzembe wa serikali,hoja ya mwanakiji ni kwamba wakati serikali imekaa kimya na baadhi ya viongozi wa muslim wanaendelea na uchochezi pengo yuko kimya hali ilipofikia zisipochukuliwa hatua za dharura watu watashinikiza viongozi wao deni watoe tamko ili kulipiza kisasi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom