Mwanakijiji, hoja za Maalim Seif na Union of treaties

Foum Jnr

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
272
132
Nianze kwanza katika hoja ya Mwanakijiji juu ya statement yake ya kumtaka Muheshimiwa Hamad kujiuzulu na kuwataka wale wazanzibari waliopo ndani ya bunge kuwacha nafasi zao ili kurudi kudai uhuru wao.

Katika Ministerial code of conduct, logic ya kuwa ndani ya goverment ni kukubaliana na kauli ya serikali au kujiondoa katika nafasi ikiwa unakwenda opposite na tamko la serikali. SMT na SMZ zote hazina kauli moja juu ya muungano na zimetoa uhuru wa kila mmoja kuchangia kwa namna anavyoamini mabadiliko yawe vipi katika katiba mpya. Kwa hili si Mheshimiwa Hamad wala mawaziri wengine waliokwenda kinyume na ministerial code of conduct inayowafanya kuachia nafasi zao. Serikali za coalition ziko nyingi sasa kutokana na result za uchaguzi ambapo majority ya kweli haipatikani, na kuungana kwa vyama kuunda serikali ya kitaifa haifuti maudhui ya vyama vyao bali ni kukaa na ku-comproise na kuangalia priority.

Natoa mfano wa stormont kule Northern Ireland ambapo Sin Fein na wale loyalist wameungana kuunda seriali ya umoja huku bado kila mmoja akilinda azimio kuu lake, angalia zaidi yule Martin Mcguines ambaye ni former commender wa IRA lakini yumo katika serikali ya sasa huku akijulikana kabisa kama ni republican anaeamini na kulenga maazimio ya united ireland against UK. Angalia pia serikali za namna hio kuanzia Israel, Ujarumani hata Uk ambapo tumeona watu wenye malengo tafauti kuungana na hata kutafautiana hadharani pale andapo agenda zao kuenda parallel. Kwa maoni yangu Mwanakijiji ni against serikali ya namna hii lakini hii ni haki yake ya kuamini na kuzungumzia kwa upeo wake anachokiamini sawa na haki ya wananchi wa asilimia 65% waliopiga kura ya yes vote kukubali mabadiliko ya katiba yaliotoa ruhusa hio na pia 49% ya kura ziliopigwa juu ya Mheshimiwa Hamad ambayo kiukweli ushindi wa chama chochote cha asilimia 51% hauwezwi kukubalishwa kama ndio majority ya kweli. Hivi Mheshimiwa Hamad yuko accountable kwa rai ya Mwanakijiji au kwa wananchi waliompigia kura? Kwa nini asimshauri Mheshimiwa Shein kuufuta uteuzi wake kwa kuenda kinyume nae?

Kuhusu wazanzibari walioko ndani ya bunge, njia moja ya wananchi wa kawaida wanaotaka kubadili upepo wa sera za nchi jambo la mwanzo linaloweza kufanikisha hilo ni kuingia katika vyombo vya kubadilisha sheria, mfano UKIP ni anti EU party, ambacho kinaongoza kwa popular vote katika EU elections UK na kikiwa na wabunge ambao lao kubwa ni kupeleka hoja yao ya anti EU, hebu mtafuteni Nogel Farage kiongozi mkuu wa UKIp na umsikilize kwa nini akiwa against EU lakini akawa ni member wa EU parliment? hizo ndizo taratibu za siasa za heshima. Katika dunia ya sasa ya kuwataka kuachana na siasa na kurudi kudai uhuru kwa njia za misituni hazina nafasi, upo uwezekana wa kubadili direction ya nchi kwa wapinzani kuwamo ndani ya chombo cha sheria kuliko ukiwa nje kupiga kelele barabarani. Lakini ni juu yake mwenyewe mwanna kijiji kutumia wabunge wake kupeleka hoja hio ya kuwaondoa wabunge wazanzibar katika bunge, naona ingelikuwa rahisi zaidi.

Tumalize kwenye suala la union ya mkataba na wale wanaouelezea kama kwamba ndio chanzo cha kuvunja muungano, kwanza na tujadili maudhui yaliomo ndani ya mabadiliko ya katiba ya zanzibar ya 2010 na tuwe wa kweli kama tungekuwa na mahakama ya katiba jee SMT na SMZ hawajakiuka katiba ya muungano? Hebu tuangalie ile statement ya Mheshimiwa Lisu bungeni juu ya mabadiliko yale na kutathmini alichokisema, utakuta hao walioapa kuilinda katiba ya muungano ndio hao hao walioadhimisha mabadiliko ya zanzibar ya 2010. Mheshimiwa Nahoda akiwa ndie waziri kiongozi Zanzibar, ambaye sasa ndie 'hero' wa muungano na tumuulize yeye akiwa kiongozi wa SMZ hakuona yale mabadiliko ya katiba yalipinga katiba ya muungano na in theory kuhatarisha kuvunja muungano huu anaoupigia debe? Je, watukufu wa nchi hii nao hawaku-initiate uvunjaji wa muungano kwa kuachia bila ya kukemea au kwa lugha nyengine kubariki mabadiliko yale yalioipa mamlaka rais wa zanzibar wa kubadili wakuu wa mikoa, border, na hata kuondoa mahakama ya rufaa tanzania katika ushiriki wake ndani ya zanzibar? Hivi badala ya kuwasakama hawa wanaotaka muungano wa mkataba kwa kisingizio cha kuvunja muungano kwa nini hamuanzi na hawa waliovunja kabisa maazimio ya katiba ya muungano na mukawaacha kuendelea kujigamba ati ndio waumini wa kweli wa muungano huku mukijuwa wazi ndio chanzo cha mkanganyiko wa katiba ya muungano? kwa nini tuwape CCM wachache license ya kutufanya tukubali kama huu ndio mfumo bora na kuwakandamiza wenye muamko wa maoni tafauti?

Tafauti gani ya muungano wa mkataba against katiba ikiwa katiba yenyewe imewezwa kuchezewa na kuvurugwa na sehemu moja tu kubadili maazimio makuu ya muungano? Ukweli mchungu nchi hizi hazijawahi kuwa moja, inakuwaje ikiwa ziko moja ikawa hata chombo kikuu cha sheria kama mahakama kuwa na limitation katika part moja ya nchi? au kukawa na mabunge mawili, rais wa wawili na mengi tu? Hivi tutacha lini kuhadaiwa na siasa za viongozi wa sasa hasa wa CCM wasioweza kutambua kama nchi hii ni moja au mbili? Inakuwaje kwa mfano wabunge wa Zanzibar kuchangia na kupigia kura maazimisho ya department zisizo za muungano au kuchanguliwa kushika nafasi kuu za wizara zisizo za muungano wakati ni vise verse kule visiwani?

Wenye kuupinga mfumo wa union of treaties waje na solid arguments zinazoonyesha kwamba huu wa katiba umeweza kuulinda muungano wa sasa hasa baada ya marekebisho ya katiba parallel ya Zanzibar ya 2010. Ninnaamini muungano ukivunjika usivunjike hatuwezi kuondosha ukweli wa historia ya miaka 48 ya kuwa wamoja, hichi kigugumizi cha muungano lazima kipatiwe ufafanuzi na ufumbuzi utakaopata nguvu ya wananchi wote ili mfumo ujao uwe na mandate ya wadau wakuu ie wananchi.

Tusikubali kuingizwa katika dimbwi la maji machafu kwa hadaa za kina AIR HEAD na CCM za kututia khofu zisizo na msingi. Tujiepushe na kauli za kuwatia chuki wananchi wa sehemu hizi mbili na kuwapa nafasi watukufu kuendelea na uhadaifu wao huku wakijifaidia nafasi kuu za muungano.
 
Foum Jnr,

..je, unapendekeza mambo gani yawe ktk treaty/mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar?

..kuna maoni kwamba hakuna haja ya kuwa na mkataba[treaty] kati ya Tanganyika na Zanzibar, bali nchi hizo zishirikiane kupitia EAC, au SADC. nini mtizamo wako kuhusu hoja hiyo.

..je, ni faida gani za kiuchumi, kisiasa, na kijamii, zitakazopatikana kwa upande wa Tanganyika?

..pia naomba utueleze faida za kiuchumi, kijamii, na kisiasa, kwa upande wa Zanzibar zitakazotokana na mfumo huo mpya.
 
Last edited by a moderator:
Maandishi ya MM Mwanakijiji huwa si mepesi kuyaelewa. Ninachoona ni mtu kulia baada ya jiwe kurushwa gizani!

Taabu kujua nani analia?
 
Jokakuu,
Suala lako nilianze kwa kusema mimi ni muumini wa muungano wenye lengo la kutarget maendeleo kwa wadau, kuimarisha sheria na uhuru wa mahakama na kutafutia ufumbuzi wa mambo muhimu yanayoleta challenge kwa wananchi ie, elimu, maji, umeme na makaazi. Katika muungano wa sasa wa katiba naona umejaa na migongano isio ya lazima, ni hadaa kwa wananchi katiba moja kusema ni nchi moja na nyengine kusema ni nchi nyengine. Mifano ya miungano ya namna hii ni mengi ilio fail.

miungano ya sadc au EAU haiwezi kufananishwa na muunggano wa Tanzania, kutokana na uasili wake wa miaka 48, binafsi sioni kama EAC itakuwa na future kubwa siku za mbele, sina imani na EAC hasa kwa kuwa sioni katika EAC kama Tanzania itafaidika sana hasa walengwa wananchi. Unapotoa mwanya wa union yenye integration ya borderless au sarafu moja ni kuanzisha vita dhidi yako mwenyewe, natoa mfano wa malawi na ziwa nyasa/tanganyika, hivi unafikiri katika future burundi nayo haitakuja kuidai part ya tanzania jirani kwamba ni yake historical na traditional hasa ikiwa tutafungua border kwa kiini macho cha EAC? au sarafu nani atakem-bail mwenziwe pindipi hali itageuka ya kiuchumi? Mungano wa Tanganyika zanzibar utaweza kuzaa matunda zaidi ikiwa tutayashughulikia mabadiliko ya kweli.

Faida zipo nyingi tu, bila ya kuwa offend yoyote humu tuje la mwanzo, udugu. vita vyovtote baina yetu vitatuhukumu kwa familia zetu zilioana na kuzaa pamoja. mfano mdogo angalia south na north korea na kuwa kattika day and age familia hazijaweza kuonana kwa muda sababu ya confrontation za kipuuzi za nationalism movement.

Uchumi, wafanya biashara wa zanzibar na uchumi wa zanzibar na tuwe wakweli unafaidika na kuwepo kwa muungano, na sawa pia kwa tanganyika ilivyofaidika na enterprenuership ya wazazibari kuanzia mwanza, tanga, daresalam etc wapo wanaoweza kubeza kwa kufananisha na arusha lakini tuangalie somo muhimu katika EA pale Mr Amin alipowafukuza wahindi na namna gani uchumi wa Uganda uliyumba. hivi serikali zote hazifaidiki na transaction hizi?

Kisiasa mfano mdogo ni upinzani wa sasa wa CHADEMA, hivi tuseme huu ufisadi umeanza juzi? Au kuwapo na serikali ya chama kimoja umeisadia tanzania? kwa nini zanzibar imekuwa na ngome kubwa ya opposition utakuta historical wazanzibar wakipingana wenyewe kwa wenyewe kutokana na ubepari vrs socialiism na usawa, mfanano na south africa hivi wale wazungu raia wa south afrika utawaita ni wageni kwa kuwa na asili ya europe? changamooto ya zanzibar katika chaguzi zake zimeinduced muamko wa demokrasia bara na nndio tunaona now nnamna upinzani unavyopanda chart. Na kwa zanzibar, kiasiasa yako mengi bara yalioisaida zanzibar, mfano leo tungekuwa na rais wa maisha kama sio CCM ya Mkapa kuzuia mabadiliko ya katiba yaliolengwa kuongeza muda wa urais kwa candidates, vipi wale wafunggwa kiisiasa walioachiwa huru baada ya mahakama kusema zanzibar haiwezi kupinduliwa hivyo hakuna charges za uhaini..

Katika mfumo mpya, tutaweka solid foundation kwa yale yaliotufaidisha kwa miaka 48, na kuyaingiza masuala mapya yanayoonyesha maendeleo zaidi kwa upande mmoja hasa zikiwa tafauti mfano afya kwa upande wa bara amabayo ni better off kuliko zanzibar au suala la coalition goverment kwa zanzibar ambayo limeleta stability zaidi.

Tukiwa na nia za kweli za kuleta mabadiliko tunaweza kurejesha ile azma ya waazilishi wa muungano huu nao ni kulinda usawa baina yetu, kuondosha matabaka na kulenga maendleo kwa wananchi.
 
Foum Jnr,

..naomba nikushukuru kwa USTAARABU na UMAKINI wako ktk kujenga hoja yako.

..tatizo la mijadala ya muungano hapa JF ni kukosa wachangiaji wa aina yako.

..natumaini spirit hii uliyoanza nayo itaendelezwa na wachangiaji wengine.
 
Last edited by a moderator:
Natoa mfano wa stormont kule Northern Ireland ambapo Sin Fein na wale loyalist wameungana kuunda seriali ya umoja huku bado kila mmoja akilinda azimio kuu lake, angalia zaidi yule Martin Mcguines ambaye ni former commender wa IRA lakini yumo katika serikali ya sasa huku akijulikana kabisa kama ni republican anaeamini na kulenga maazimio ya united ireland against UK.

Tumalize kwenye suala la union ya mkataba na wale wanaouelezea kama kwamba ndio chanzo cha kuvunja muungano, kwanza na tujadili maudhui yaliomo ndani ya mabadiliko ya katiba ya zanzibar ya 2010 na tuwe wa kweli kama tungekuwa na mahakama ya katiba jee SMT na SMZ hawajakiuka katiba ya muungano? Hebu tuangalie ile statement ya Mheshimiwa Lisu bungeni juu ya mabadiliko yale na kutathmini alichokisema, utakuta hao walioapa kuilinda katiba ya muungano ndio hao hao walioadhimisha mabadiliko ya zanzibar ya 2010. Mheshimiwa Nahoda akiwa ndie waziri kiongozi Zanzibar, ambaye sasa ndie 'hero' wa muungano na tumuulize yeye akiwa kiongozi wa SMZ hakuona yale mabadiliko ya katiba yalipinga katiba ya muungano na in theory kuhatarisha kuvunja muungano huu anaoupigia debe? Je, watukufu wa nchi hii nao hawaku-initiate .

Foum Jnr,

Imekuwa vizuri sana umeleta mfano wa Northern Ireland na Sinn Fein, na ningetaka nianzie hapo. Sinn Fein -ambao ni wakatoliki - wanalenga kuwa na Ireland moja (Northern Ireland & Repulic of Ireland). Lakini Loyalists - ambao ni Protesants, wako upande wa United Kingdom na hivyo wanakula kiapo cha utii kwa Monarch, kwa maneno mengine United Kingdom.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu na hatimaye kuondoa tofauti zao (Good Friday 1998) mahasimu hawa ni kweli wamekuwa na serikali ya mseto (umoja wa kitaifa). Hata hivyo, Sinn Fein wamebaki na msimamo ule ule - hawali kiapo cha utii kwa Monarch. Labda nikufahamishe tu hakuna mbunge hata mmoja toka Sinn Fein anayehudhuria vikao kwenye bunge la Westminster (House of Common). Hili ndilo bunge la United Kingom kama ilivyo Dodoma. Hakuna hata mmoja! Na hawadhuhurii kwa sababu moja kubwa - wamekataa kata kata kula kiapo cha utii kwa Monarch. Wao ni United Ireland na sio United Kingdom.

Wabunge wa Sinn Feinn ambao kwa nafasi zao walitakiwa wahudhurie bunge la Westminster wamekuwa wanafanya safari toka Northern Ireland kuja London kwa 'maongezi' tu na wabunge wengine au wananchi wa kawaida kwenye grounds za Westiminster Palace, lakini hawadhurii vikao vya bunge. Mwezi September mwaka huu (2012) msemaji wa Sinn Fein alinukuliwa na vyombo vya habari akisema hivi kuhusu wabunge wao kuhudhuria bunge UK,
"There is absolutely no prospect of us taking our seats. Absolutely none."
http://www.belfasttelegraph.co.uk/news/politics/london-calling-sinn-fein-mps-to-up-presence-at-westminster-16216854.html#ixzz2ElOfmvny

Aliyekuwa President wa Sinn Fein - Gerry Adams alipochaguliwa kuwakilisha jimbo lake, watu walisubiri kwa hamu kuona kama atalegeza msimamo. It didnt happen, hata baada ya makubaliano ya Good Friday yaliyozaa serikali ya umoja, bado bwana huyu aliendelea na msimamo wake. Hakuhudhuria vikao Westmister.

Kwa kifupi huyo Martin
McGuinness na Sinn Fein wenziwe - regardless wako kwenye serikali ya mseto au la - are "walking the talk". Msimamo wao kuhusu One Ireland haujabilika - no Westminster kwenye equation yao.

Maalim Seif na Hatma ya Zanzibar

Inawezekana kuna watu wanajua Maalim Seif anataka nini kuhusu Zanzibar. Lakini kwa sababu wanazozijua wao na hata Maalim Seif wameamua kutoa tamthilia ndefu sana. Episode ya kwanza ilikuwa serikali 3, episode ya pili ikaja na Muungano wa mkataba! Kwenye hii episode ya pili kuna sehemu kadhaa - mfano, Muungano wa SeneGambia (failed), Muungano wa Swiss, na Muungano wa EU! Maalim Seif anataka nini?

Ukiwa kiongozi ni lazima uwe na clear picture unapeleka wapi wale unaoongoza. Unatakiwa ueleze - in details- jahazi linaenda upande gani, na maandalizi yako vipi?

Na moja ya shida iliyopo ni mtindo wa Maalim Seif kuongoza kutoka nyuma -Leading from behind. Imekuwa ni kawaida kusikia 'wapambe' wakija ni vibwagizo, na baadae ndio utamsikia Maalim Seif anaongea. Hata huu utitiri wa aina za Muungano umekuwa kwa mtindo huo huo. Martin McGuinness na Sinn Fein wamekuwa na clear picture ya aina ya Taifa wanalotaka (United Ireland). Na msimamo wao haujabadilika. Maalim Seif anataka Taifa la aina gani? Ndani ya huu mwaka peke yake tumeshasikia zaidi ya aina mbili za Muungano!

Tukiendelea na hii tamthilia ya Maalim Seif na Hatma ya Zanzibar, naomba sasa tugeukie kauli yake ya kutaka 'Zanzibar huru'. Maalim Seif anasema anataka Taifa la Zanzibar lenye mamlaka kamili ndani na nje ya nchi. Perfect! Anaendelea kwa kutoa vitu muhimu ambavyo ni lazima vipatikane ili Taifa huru la Zanzibar liwepo: Sarafu, kiti kwenye umoja wa mataifa, passport, etc. Sawa sawa! Huhitaji kuwa brain surgen kujua kuwa hivyo vitu anavyotaka Maalim Seif vinafanya Zanzibar kuwa Sovereign nation. (
mpaka hapo nakubaliana naye kabisa - hatma za Taifa lolote iko mikononi mwa wananchi wake). Na kwa maana hiyo Maalim Seif ametupa 'trailer' ya sehemu ya pili ya tamthlia yake inayohusu Muungano kwamba, in actual sens,e hicho anachokiita Muungano wa mkabata hauna tofauti na East Africa Community au AU.

Ukitafakari kwa makini, Maalim Seif anahuburi kuVunja Muungano, lakini kwa sababu anazojua yeye amekuwa anakwepa matumizi ya maneno 'vunja Muungano' badala yake anafunika na maneno 'Muungano wa Mkataba'. Nasema hivi kwa sababu ili kupata Taifa huru la Zanzibar ni lazima (msisitizo) kuindoa Zanzibar toka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkataba utakuwepo baada ya Taifa huru lakini hatua ya kwanza kupata hicho kinachoitwa 'Zanzibar huru'. Ukishakuwa na Zanzibar huru ndio unaanza kuongea mambo ya 'Muungano wa mkataba wa kuchanja kuku, wa kucheza mdunduko au hata wa kunywa maji, na nchi yoyote ile (sio lazima Tanganyika).

Sasa, kama msimamo wa Maalim Seif na chama anachokiwalisha ni kuwa na Taifa huru la Zanzibar, wabunge wa CUF wanafanya nini kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Kwanini wasifanye kama huyo Martin McGuinness na Sinn Feinn wa Ireland (mfano uliotupa)?

Maalim Seif ni mdau mkubwa sana kwenye uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa. Alifanya mazungumzo na mahasimu wake (CCM) na baadae akaongoza wanachama wake kwenye kura ya maoni, Katiba ya Zanzibar kubalishwa na hatimaye kuunda SUK. Na kama ilivyokuwa kwenye SUK, Muungano pia ni swala kikatiba, sasa, kwanini Maalim Seif hachukui hatua stahiki i.e kura ya maoni, muswada BLW na hatimaye Jamhuri ya watu wa Zanzibar? Na maadam tunaambiwa wanzibari 'wengi' wanataka taifa huru, ni dhahiri kura ya maoni itakwenda vizuri. Ni kwanini hili halifanyiki, badala ya malumbano na kauli za kuudhi?

Kwenye blue: Nakubaliana na wewe kabisa, na inashangaza watu wanakula kiapo cha utii kwa kitu wanachopinga!

Kwa upande mwingine kitendo cha Maalim Seif kukwepa kutamka 'vunja Muungano' na badala yake anasema 'Muungano wa Mkataba' ni kwamba anaimbia Tanganyika "I hate you son of a bitch, but I love your wallet". Let's sign a deal, I can put on a blindfold!
 
Nchi yetu imejaaliwa na wingi wa vijana ambao ima tumekuwa kimnya tukiwaacha wachache kutuburuza, au kujishughulisha na ufisadi pale tunapopata nafaasi ya kuleta mabadiliko. Katika JF tatizo kubwa ni wachache wanaochukulia kumbi hizi za matusi ya wenyewe kwa wenyewe na kutokuwa tayari kuwasikiliza wengine ikiwa wnaatafautiana ki-maoni. tutawezaje kubadilisha muelekeo wa nchi katika demokrasia ya kweli ikiwa wenyewe vijana tumekuwa na mitizamo ya uchagiaji wa uadui kwa wenye muoni tafauti?

Kama mzanzibari ninaamini muungano una nafasi kubwa katika maisha ya wananchi, zaidi linalonipa moyo ni wananchi wenyewe binafsi hawana khiyana baina yao na ndio maana ukakuta kule Kipumbwi Tanga kumejaa wazanzibari walioa na kuzaa na halkadhalika karibu mikoa yote ndani ya zanzibar. Tatizo kubwa ni wanasiasa husasan CCM na sera kandamizi ya kuzuia maoni ya wengine, hivi katika dunia ilioendelea hakuna opposition team ndani ya vyama? demokrasia inatoa wito wa kuwa na uwezo wa kujadili na kutoa hoja itakayopata popularity na kujizolea wajumbe watakaokuchagua kuleta mabadiliko, hakuna chama kinachoendelea kwa ukweli kikiwa statitic bila ya dynamism ya maoni ya mener wake.

Nasikitishwa kukuta wananchi baina yetu tulioamua kutukana asili za wengine na kuzibeza kwa sababu ya mambo machache ya katiba, katiba inavunjika lakini udugu haufi wala kuondoka, miaka 48 ya shida ya pamoja huku wachache wakijifaidia matunda halisi ya muungano na sisi kuwa kimnya au kujiingiza katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ndio dhambi kuu ninayoiona inainyemelea jamii zetu. Katika kuheshimu na kuamini demokrasia na tuwe tayari kuwasikiliza wananchi, kubadilika na kutafuta njia za uhakika bila ya kubabaisha na kuhadaa walengwa kusuluhisha matatizo yaliopo. hivi miaka 48 ya union hii haijawa nafasi nzuri kwa CCM na wengine kujua kwamba huu mfumo mzima hauna muelekeo mwema? Nimeona kuleta hoja kwa sababu wengi katika JF na sehemu nyengine ni rahisi kusahau adui mkuu wa muungano si wazanzibari wala watanganyika bali ni radical CCm wanaofikiri ni wao wenye license ya kutuburuza maisha. msemo wa zidumu hekima za mwenyekiti ni ukosefu wa nadharia ya moderation na ni agaisnt democratic move ya kusikiliza na kufuata maelekezo ya wananchi.

Tusikilizane na kutafauti kwa ihsani, tuwasikilze wananchi wa pande zote mbili wanasemaje, dhima ya wanasiasa ni kutafuta permanent solution kuondoa mashaka yaliopo. Kama umedumu kwa miaka 48 na tuendeeleze katika mfumo mpya wa kisasa ulio na lengo la kutuondolea umasikini sisi wenyewe sio kujenga umoja wa utaifa feki huku ndani ya nyumba zetu zikiwa na migawano na limitation.
 
Foum,
Kwanza nashukuru kwa maoni yako
Pili, bado hujasema nini kifanyike na kwa njia gani.
Tatu, nadhani usiogope kuwa mkweli kwa ku-balance mambo yasiyowiana.
 
Nashukuru kwa challenge ulionipa, katika picture ulioweka umesahau kitu kimoja, majuzi tu Martin Mcguiness alikuonekana wakipeana mikono na huyo adui wake mkuu Queen elizambeth alipotembbelea hapo Belfast, na la pili msimamo wa SinnFein unajulikana kabisa kwamba vunja muungano wakati msimamo wa CUF na Mheshimiwa Hamad uko wazi, muungano uwe wa mabadiliko, sasa cha kuangalia na kustaajabisha amekuwa akisakamwa yeye kwa kutaka mabadiliko na kuachwa waliovunja hasa muungano kwa kuleta katiba ya 2010 na sasa ndio mawaziri na hero wa union kwa nini tuwe na vipofu wa ukweli?

Katika mtazamo wako na wengine mkataba ni kuvunja muungano, kama ni sawa jee huu wa katiba uko activve kweli hasa zikiwa katiba mbili ziko parallel kama sasa? Kwa nini khofu hii haipelekwi kwa walioleta mabadiliko haya including rais, makamo wake, waziri mkuu walioridhia uvunjwaji wa katiba hii walioipia?

hoja ya kusema mheshimiwa Hamad ni mvunjaji wa muungano haina mashiko, alichotaka mabadiliko ya kweli yenye kuwasikiliza zaidi wananchi kelele zao hasa, ila kama kwako huo ndio uvunjaji wa muungano basi tukubali kutafautiana..
 
Jokakuu,
Suala lako nilianze kwa kusema mimi ni muumini wa muungano wenye lengo la kutarget maendeleo kwa wadau, kuimarisha sheria na uhuru wa mahakama na kutafutia ufumbuzi wa mambo muhimu yanayoleta challenge kwa wananchi ie, elimu, maji, umeme na makaazi. Katika muungano wa sasa wa katiba naona umejaa na migongano isio ya lazima, ni hadaa kwa wananchi katiba moja kusema ni nchi moja na nyengine kusema ni nchi nyengine. Mifano ya miungano ya namna hii ni mengi ilio fail.

miungano ya sadc au EAU haiwezi kufananishwa na muunggano wa Tanzania, kutokana na uasili wake wa miaka 48, binafsi sioni kama EAC itakuwa na future kubwa siku za mbele, sina imani na EAC hasa kwa kuwa sioni katika EAC kama Tanzania itafaidika sana hasa walengwa wananchi. Unapotoa mwanya wa union yenye integration ya borderless au sarafu moja ni kuanzisha vita dhidi yako mwenyewe, natoa mfano wa malawi na ziwa nyasa/tanganyika, hivi unafikiri katika future burundi nayo haitakuja kuidai part ya tanzania jirani kwamba ni yake historical na traditional hasa ikiwa tutafungua border kwa kiini macho cha EAC? au sarafu nani atakem-bail mwenziwe pindipi hali itageuka ya kiuchumi? Mungano wa Tanganyika zanzibar utaweza kuzaa matunda zaidi ikiwa tutayashughulikia mabadiliko ya kweli.

Faida zipo nyingi tu, bila ya kuwa offend yoyote humu tuje la mwanzo, udugu. vita vyovtote baina yetu vitatuhukumu kwa familia zetu zilioana na kuzaa pamoja. mfano mdogo angalia south na north korea na kuwa kattika day and age familia hazijaweza kuonana kwa muda sababu ya confrontation za kipuuzi za nationalism movement.

Uchumi, wafanya biashara wa zanzibar na uchumi wa zanzibar na tuwe wakweli unafaidika na kuwepo kwa muungano, na sawa pia kwa tanganyika ilivyofaidika na enterprenuership ya wazazibari kuanzia mwanza, tanga, daresalam etc wapo wanaoweza kubeza kwa kufananisha na arusha lakini tuangalie somo muhimu katika EA pale Mr Amin alipowafukuza wahindi na namna gani uchumi wa Uganda uliyumba. hivi serikali zote hazifaidiki na transaction hizi?

Kisiasa mfano mdogo ni upinzani wa sasa wa CHADEMA, hivi tuseme huu ufisadi umeanza juzi? Au kuwapo na serikali ya chama kimoja umeisadia tanzania? kwa nini zanzibar imekuwa na ngome kubwa ya opposition utakuta historical wazanzibar wakipingana wenyewe kwa wenyewe kutokana na ubepari vrs socialiism na usawa, mfanano na south africa hivi wale wazungu raia wa south afrika utawaita ni wageni kwa kuwa na asili ya europe? changamooto ya zanzibar katika chaguzi zake zimeinduced muamko wa demokrasia bara na nndio tunaona now nnamna upinzani unavyopanda chart. Na kwa zanzibar, kiasiasa yako mengi bara yalioisaida zanzibar, mfano leo tungekuwa na rais wa maisha kama sio CCM ya Mkapa kuzuia mabadiliko ya katiba yaliolengwa kuongeza muda wa urais kwa candidates, vipi wale wafunggwa kiisiasa walioachiwa huru baada ya mahakama kusema zanzibar haiwezi kupinduliwa hivyo hakuna charges za uhaini..

Katika mfumo mpya, tutaweka solid foundation kwa yale yaliotufaidisha kwa miaka 48, na kuyaingiza masuala mapya yanayoonyesha maendeleo zaidi kwa upande mmoja hasa zikiwa tafauti mfano afya kwa upande wa bara amabayo ni better off kuliko zanzibar au suala la coalition goverment kwa zanzibar ambayo limeleta stability zaidi.

Tukiwa na nia za kweli za kuleta mabadiliko tunaweza kurejesha ile azma ya waazilishi wa muungano huu nao ni kulinda usawa baina yetu, kuondosha matabaka na kulenga maendleo kwa wananchi.
Nakupa heko heko ,congratulation, wewe ni msomi wa kweli na unaeleza kitu ambacho hakina unafiki,na umenifurahisha zaidi pale ambapo umeweza kuelezea faida za muungano, lakini hukuweza kuelezea hasara za muungano ,lakini hasara za muungano ambazo wazanzibari wamekuwa mstari wa mbele kudai haki zao za muungano, na ndio ukaona wakati huu wamekuja na kitu kipya ambacho wazanzibari wamefikiria na kuchukulia mifano halisi kama vile muungano wa EAC ,OIC,EU CHINA na hongkong.

Hapo awali kwa mfano zanzibar chama cha cuf walikuwa na sera ya serikali tatu, lakini kutokana na vijana kuamka, kuelimika ,wameweza kutafakari mfumo mzuri zaidi ya serikalitatu na kuona mfumo wa serikali ya mkataba ndio mzuri zaidi, yule mtoto mdogo wa zanzibar sasa hivi ukimuuliza nini maana ya muungano wa mkataba atakueleza maana yake na mifano atakupa halisi, lakini kama utakutana na mkereketwa wa ccm atakuambia mfumo huu tulio nao ni bora zaidi lakini atakuwambia kuwa zanzibar iwe na huru na kujiamulia mambo yake,ukienda undani zaidi utagundua anarudi kule kule kwenye mkataba lakini kwa utashi wa vyama vya siasa vyao na kulinda maslahi yao ndio hutamka kuwa muumini wa serikali mbili,lakini cuf imelifikiria zaidi suala la mkataba na kuona ya kwamba wananchi asilimia zaidi ya 75 wanaunga mkono, na wao ndio sera yao sasa hivi muungano wa mkataba.

Kwa upande wa bara suala hili kwa baadhi ya watu wanaona ni kuvunja umoja wa watanzania na kuona ya kwamba wazanzibari ni wasaliti wakubwa, na kutoa vitisho vya aina mbali mbali kwa wazanzibari, hawafahamu kuwa kila raia ana haki ya kulinda identity yake, na ndio wazanzibari wanasimama kidete katika hilo,lakini bado tanzania bara wao wamejisahau hilo, kulinda identity yao,

Ukweli ni kwamba lazima tubadilike, kubadilika huku tukubali matakwa ya wananchi, na ndio ambao wenye dhima kubwa ya nchi, wao ndio wanao ongozwa na serikali, na viongozi hawa hawa wa serikali wanatokana na wananchi, ili tuweze kufika huko mbele tunakotaka lazima tufanye marekebisho makubwa sana ya muungano.

wakali uliasisiwa muungano,wasomi walikuwa ni wachache,muungano haukuwa wa kuridhiana wala haukuwa wa matakwa ya wananchi,na ndio tunaona leo hii muungano haupo katika nyoyo za wananchi ispokuwa upo katika mikono ya wanasiasa hawa wana ccm ambao wanaongoza nchi hii miaka 48, wengine hufika kusema muungano kama ungelikuwa mbaya usinge dumu maiaka 48 lakini hawakumbuki kuwa muungano huu ulilindwa na bunguki na ulipoteza maisha ya watu wengi sana, ukweli ni kwamba uli dumu kwa damu ya binadamu na bunduki.

Ukweli hauepukiki,

Jamuhuri ya watu wa zanzibar kwanza.
 
Nashukuru pia Nguruvi kwa maelezo, katika suala la kusema nini kifanyike nimeeleza kwa uwazi mabadiliko ya muungano katika treaties na kusema khofu inayojazwa na badhi yetu kwamba huo ni kuvunja muungano ni kutokuwa wakweli kwa sababu ukilingganisha na katiba ya sasa utakuta muungano umekiukwa na hasa rais wa tanzania kuvuliwa madaraka yake visiwani. Nimeeleza pia katika masuala kuwamo pamoja ni yale ayanayolenga maendeleo kwa wananchi, kuanzia elimu, afya, maji, umeme, makaazi na utawala wa sheria pamoja kulinda demokrasia.
Hujafafanua zaidi "kubalance yasiowiana" kwa vile nimeweka challenge kwa wale waiotaka huu mkuungano wa treaty waje nao na hizo hoja zao na watueleze ni kipi kipya katika treaty kitachoondosha khofu ya kuvunja muunggano ukilinganisha na katiba ya sasa hasa baada yya mabadiliko ya zanzibar ya 2010.
 
Foum stop contradicting thyself. if it integration and adaption of single currency worked wonders for Tanganyika and Zanzibar then same is true for the five east african countries. Whats good for the goose is good for the gander.
 
Ndugu Ghibu,
Nashukuru kwa kuchangia kwako, ila sijaona mantiki ya kuzungumzia hasara kwani zimeshaelezwa nyingi na kila upande, nimetaka kulenga zaidi katika faida ambazo pia zimekuwa underestimated na wengi wetu. Hoja yangu ni kujenga utamaduni wa hekima katika maoni na kulinda heshimana utamaduni katika majadiliano. Ninaamini muungano unaweza kuendelezwa na kuwa mzuri zaidi ikiwa mabadiliko ya kweli yatakuja hasa yakilenga zaidi katika direction ya maendeleo, integrity kwa wananchi, sheria na demokrasia ya kweli.
 
Simple mind,
Unachokiona contradiction ni kichekesho kwa sababu unalinganisha uzamaji wa meli na coin.. hivi unafikiri kijinchi kama zanzibar cha laki tisa na muungano wa watu milioni 200? sasa ikiwa tanzania itakuwa na shida na kushindwa kukopa kutokana na single currency nani atakem-bail mwenziwe? Burundi au kenya? Tafakari kwa nini ramani ya 1800 iliochorwa na wazungu iwe ndio chanzo cha kudai umiliki wa bahari wa malawi? unafikiri integration ya boderless kwa EAC haitakuja kuwa ndio chanzo cha bbaadhi ya nchi kudai chao kwa kisingizio kama hicho hasa ukizinggatia nchi zao ndogo na overpopulated? katika suala la single currency kama unaona tumefanikiwa hizi kkelele za zanzibar kwa nini ziiwe kero kubwa kwa sasa, fuatilia challenge za muungano waraka wa serikali unaposema single currency pia ni tatizo japo uchumi haumo katika muungano kutokana na fiscal policies kulenga zaidi priority ya watanzania milioni arobaini kuliko wazanzibar laki tisa utapata ufahamu wa ninachokieleza..
 
Nashukuru kwa challenge ulionipa, katika picture ulioweka umesahau kitu kimoja, majuzi tu Martin Mcguiness alikuonekana wakipeana mikono na huyo adui wake mkuu Queen elizambeth alipotembbelea hapo Belfast, na la pili msimamo wa SinnFein unajulikana kabisa kwamba vunja muungano wakati msimamo wa CUF na Mheshimiwa Hamad uko wazi, muungano uwe wa mabadiliko, sasa cha kuangalia na kustaajabisha amekuwa akisakamwa yeye kwa kutaka mabadiliko na kuachwa waliovunja hasa muungano kwa kuleta katiba ya 2010 na sasa ndio mawaziri na hero wa union kwa nini tuwe na vipofu wa ukweli?
..

Martin McGuiness hana chuki binafsi na Malkia kama malkia, ila anapinga Northern Ireland kuwa sehemu himaya anayoongoza Malkia. Na hata baada ya kupeana mikono, wabunge wa Sinn Fein wameendelea na msimamo wao wa kutohudhuria bunge la UK. Hiii ni tofauti kabisa na wabunge wa CUF ambao msimamo wao ni 'vuguvugu'. Wanataka kuwa huru lakini wanachukua posho! Wabunge wa Sinn Fein hawachukui allowances.

Kwenye blue: Msimamo wa CUF na Maalim Seif ni upi? Kama ni Muungano wa mkataba maana yake anataka kuvunja huu wa sasa. Na ni nani alimwambia Seif Tanganyika inataka kuungana na Zanzibar - tena- baada ya huu Muungano wa miaka 48 kusambaratika? Ni vizuri tukatafsiri hicho anachokiita Muungano wa Mkabata baina ya Tanganyika na Zanzibar 'huru'. Huru means to free or detached from...

Tukumbuke moja ya sababu anazotoa Maalim Seif ni kwamba Tanganyika inanyonya Zanzibar. Kwa maoni yake Seif, miaka 48 ya Muungano imeleta hasara sana kwa Zanzibar na watu wake. Hivyo anataka Mkataba! Sasa kama Tanganyika imeinyonya Zanzibar, kwanini anataka kuungana na mnyonyaji yule yule? Ni kitu gani kinamzuia Maalim Seif kudai uhuru kamili bila 'extension? Kwanini anaweka kupengele cha 'kuungana' wakati anajua anayeungana naye ni mnyonyaji?

Mwisho, ni vitu gani hasa Maalim Seif anataka viwe kwenye huo Muungano wa mkataba na 'mnyonyaji' Tanganyika?
 
Ndugu yangu,
Naona umekuwa msahaulifu wa beef iliopo kati ya Mcguiness na queen kwa sababu moja ya tukio la terrorist la IRA lilimuua mwanafamilia mmoja wa royal kwa Prince Philip na ndio maana tukio hilo la yeye kupeana mkono na queen lilisubiriwa sana na media hapa hasa wakitaka kujua kama atatoa mkono hasa kwa vile moja ya mikutano ya mcguiness huko nyuma alitamka hasa kutompokea queen wala kutomtambua. Hebu angalia statement yako ilivyo na wasi wasi akiwa mkuu wa nchi utasemaje hana matatizo naye wakati ndie mtawala wa united kingdom?

Ni sawa waliposema hawataingia katika parlimet ya Uk lakini ndio serikali hio hio inayotoa mishahara, mafao, na hata ulinzi wa polisi sasa kama hio sio political opportunism ni nini? Iweje umuone hero kwa hilo na umbeze mwengine?

Hebu tazama nini hasa IRA wamesema juu ya kina Mcguiness na Gerry Adams baada ya kuingia serikalini?hivi unafikiri wanarepresent IRA na agenda zao hasa kwa kumpokea na kumkubali queen kama kiongozi wa serikali wanaoipinga?

Hoja ya kuwa huru na kuwamo ndani ya muungano ina uharamu upi hata ubatizwe kama ni kuvunja muungano wakati tayari mabadiliko anayoyasema yashatamkwa na katiba ya smz ya 2010? Hoja za kusema watoke wabunge ni za kitoto kwa sababu katika dunia ya sasa hasa katika bara letu demokrasia hio ya kugoma haileti effect yoyote, maana chadema waligoma na mwishowe wanajuwa kabisa kuukabili changamoto ni kuwamo ndani ya kiungo muhimu cha taifa.

Tujiulize jee wale wapiga kura waliompitisha mbunge wakijuwa kwamba sera zake watakubali kupoteza representation kwa waliomtuma? Hivi mbunge anajiwakilisha binafsi au waliomtuma?

Nimetoa mfano thabit wa UKIP na Majibu ya Nigel Faraj alipoulizwa ya nini kuwamo katika bunge la EU wakati sera yake hawautaki muungano huo na akajibu ni rahisi kuukata wakiwamo ndani ya bunge au at least kuvunja nguvu yoyote itakayozidisha intergration ya nchi yao ndani ya EU.Na sio yeye tu kuna kina Le pen nao pia wamejitosa humo, anti EU kutoka kila nchi wakipigania agenda moja ya kuzima harakati za integration zaidi kwa nchi zao huku pia wakiendelea na local campain against EU.

Tusitoke katika mada, tujiulize kama CUF na wengine hakuna alietamka kutoutaka muungano, wala kuwa huru hakumaanishi katika miungano hakumaanishi kuvunja muungano ila ni mabadiliko ya mfumo unaoongoza muungano. Sawa na hawa waliobadilisha maudhui ya muungano na ikaenda kinyume na katiba huku tukiwashangilia kuwa ndio watakatifu wa muungano.

Katika majibu yako ya juu unasema kuna tetesi mimi si muumini wa conspiracy theories, kama hakutamka au chama chake kusema muungano basi hatuwezi just kuwa na blank blanket la kusema ni anti unionist unless ukiwa na definition yako mwenyewe ya nani anti unionist na kwa hilo tutatafautiana kwa maoni na hoja tuwaache wengine wajudge ukweli.

Lengo la link ya juu ni kuona bias kubwa kiongozi mmoja anaetamka kwa kujiamini maoni yake juu ya katiba huku wakiachwa hasa waliovunja makubaliano kuendelea kudanganya umma, hio ndio hoja. Na pili kuwafumba midomo wenye kutaka mabadiliko ya mktaba kwa kisingizio cha kuvunja muungano wakati hio katiba iliotakiwa kulindwa imeshachafuka.

Natoa mfano mmoja muhimu wa namna gani muungano unatakiwa uwe, katika UK serikali ilishindwa kumuondosha yule mr hook kwa sababu ya mahakama ya EU ambayo ndio ya juu kuliko hata bunge la wananchi lilizuia kwa sababu waliona kuvnjwa kwa haki ya mwanadamu, jee watu walio na muungano wa treaties kama huo ni dhaifu kuliko tulio na muungano wetu wa katiba ambayo tayari upande mmoja umeshazuia ushiriki wa mahakama ya upande wa pili kwa mambo ya visiwani?

Sipo katika kumtetea Mheshimiwa Hamad, nimejenga hoja juu ya maoni ya mwanakijiji anayotaka ajiuzulu nami nimeoka kwa sheria ipi, ethic ipi au logic gani? Na pia kueleza kwamba leo tutaanza kwa kusema wabunge wazanzibar watoke katika bunge la muungano jee tutaishia hapo tutaendeelea na wito wa kuwafukuza walio na asli ya visiwani? Na mwisho kuonyesha hakuna tafauti ya mkataba wala katiba kama yanaweza makubaliano kuvunjwa na upande mmoja kwa namna ya mabadiliko ya 2010 na khofu ya kitoto kuendeleza mijadala kwa namna hio kitachodumisha muungano na mfumo wake wowote ni kuwashirkisha wanannchi kwani ndio wadau wakuu. Ukivunjwa usivunjwe hakuna anaeweza kufuta historia ya udugu wa miaka 48, angalia republic ya ireland na uhusiano wake wa UK imefika hadi juzi pesa za walipa kodi wa UK ndizo zilizo bail bank zao zilizokuwa hatarini kufilisika wakati UK haimo katika sarafu moja ya EU na japo wakiwa na uhasimu wa miaka sence ndio iliofanya kazi sio ubishi wa kitaifa na utashi wa kukhofishana katika karne ya sasa.

Kuhusu nani kasema kama wanataka kuungana katika mkataba wa muungano baada ya kufa kwa sasa basi jibu zuri watakuwa nalo wananchi na tuwaachie wanasiasa wajigambe na mfumo upi wanautaka mwishowe tuwasikilize wanasemaje wananchi.
 
Ndugu yangu,
Naona umekuwa msahaulifu wa beef iliopo kati ya Mcguiness na queen kwa sababu moja ya tukio la terrorist la IRA lilimuua mwanafamilia mmoja wa royal kwa Prince Philip na ndio maana tukio hilo la yeye kupeana mkono na queen lilisubiriwa sana na media hapa hasa wakitaka kujua kama atatoa mkono hasa kwa vile moja ya mikutano ya mcguiness huko nyuma alitamka hasa kutompokea queen wala kutomtambua. Hebu angalia statement yako ilivyo na wasi wasi akiwa mkuu wa nchi utasemaje hana matatizo naye wakati ndie mtawala wa united kingdom?

Ni sawa waliposema hawataingia katika parlimet ya Uk lakini ndio serikali hio hio inayotoa mishahara, mafao, na hata ulinzi wa polisi sasa kama hio sio political opportunism ni nini? Iweje umuone hero kwa hilo na umbeze mwengine?

Hebu tazama nini hasa IRA wamesema juu ya kina Mcguiness na Gerry Adams baada ya kuingia serikalini?hivi unafikiri wanarepresent IRA na agenda zao hasa kwa kumpokea na kumkubali queen kama kiongozi wa serikali wanaoipinga?

.

Nafahamu 'historical' animosity kati ya The House of Windsor na IRA- specifically Gerry Adams & Martin McGuiness. Na huyo mwanafamilia ya royal aliyeuliwa na bomu la IRA ni Lord Mountbatten, ilikuwa mwaka 1979. Na pia nakumbuka vizuri mjadala kabla ya Malkia kukutana McGuness.

Re. mfano wa Republic of Ireland. Yes, walikuwa chini ya himaya hiyo ya UK lakini miaka 80 na ushee walijitoa. Sasa hivi wana mahusiano mazuri kabisa na UK. Hivyo sioni kwanini Tanganyika na Zanzibar wasiwe na mahusiano mazuri even if Muungano unavunjika?

Sina hakika unatafsiri vipi Muungano wa Mkataba baina ya Zanzibar huru na Tanganyika? Ili kupata Zanzibar huru, ni lazima utenganishe -uiondoe kwenye Jamhuri ya Muungano. Kumbuka Maalim Seif anata Zanzibar yenye sarafu yake, kiti kwenye umoja wa mataifa, na hata mahusiano na nchi za nje. Ni nchi huru. Huwezi kuwa na vyote hivi halafu ukasema Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano! Na mimi sina tatizo kama Zanzibar wanataka uhuru kamili. Ni haki yao kabisa.
 
Back
Top Bottom