Mwanajeshi mstaafu ateka mzee wa miaka 80 Ifakara

Semahenge

Member
Apr 1, 2023
25
13
Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la EMMANUEL MKOMAWAGI ambaye alikuwa mwanajeshi Arusha Monduli akishirikiana na mwenyekiti wa kijiji cha Kaporo Ifakara anayeitwa SAIDINA FAYA kumteka mzee mstaafu anayekadiriwa kuwa na miaka 80(jina Kapuni!)ambaye anasumbuliwa na kisukari na presha.

Mzee huyo alichukùliwa kwa udhalilishaji mkubwa akiwa kwake mchana kweupe.

Alikodishiwa wahuni wakaja wakambeba mzobe mzobe wakamweka kwenye bajaji wakiwa wanampiga na kumkanyaga kanyaga (aliwekwa sehemu ya kukanyagia miguu kwenye Bajaji.

Watekaji hao walimsafirisha usiku mzima hadi wilaya nyingine hadi kijiji kinaitwa Ihowanja wilaya ya Malinyi akiwa amenyang'anywa simu pamoja na wallet yake

Tunashukuru Jeshi la Polisi Ifakara mjini kwa kushirikiana na wasamarian wema kumtrack mwanajeshi na kujua yuko huko vijijini kwa bibi mnyoa nywele kwa lengo la kwenda kumnyoa nywele(imani za kishirikina zilizopitwa na wakati)

Tunaomba vyombo vya sheria vimsaidie Mzee huyu kupata haki yake kwani Mwanajeshi anajitapa amestaafu amelipwa kiasi kizuri cha pesa anatamba atashinda hii kesi..

Huyu mzee mstaafu alipokonywa hela alizokua nazo, simu, pamoja na kadi zote za benki na kadi ya NHIF.

Naombeni msaada wa "kisheria" kuhusiana na hili suala la UTEKAJI NA UDHALILISHAJI Kwa huyu mzee .

Natanguliza shukrani

Cc;@Pascal Mayala
Petro E. Mselewa
 
SAIDINA FAYA huyu mwenyekiti ni njaa kali balaa. Aliwahi kuuza kiwanja mara mbili.
Na mimi nimeambiwa hizo habari..wanakijiji wanaomba wapaze sauti aondolewe uenyekiti .wengi mno wamelalamika hayo ..serikali ya ccm iliangalie hili kwa umakini...binafsi simfahamu natamani nimuone
 
Ndugu zangu wakazi wa wilaya ya Kilombero,Ulanga na Malinyi imani za kishirikina zimetanda kwenye akili zao.
Wanawaza uchawi + kupelekana kwa Kalembwana kunyoona nywele pamoja na mavyuzii ni ujinga sana ndio maana umasikini wa kipato hadi wa akili ni mkubwa sana kwa jamii ile.
 
Ndugu zangu wakazi wa wilaya ya Kilombero,Ulanga na Malinyi imani za kishirikina zimetanda kwenye akili zao.
Wanawaza uchawi + kupelekana kwa Kalembwana kunyoona nywele pamoja na mavyuzii ni ujinga sana ndio maana umasikini wa kipato hadi wa akili ni mkubwa sana kwa jamii ile.
Kabisa .na chanzo ni mgogoro wa ardhi..mipaka ya beacon..mjeshi akamwambia huyo mzee umepata wapi hela za kuwa na viwanja vingi hivi? Wewe ni mchawi twende kwa bibi kalembwana sijui ukanyolewe ndo kubebwa mzobe mzobe na wahuni na kipigo juu ajabu sana yaani
 
Back
Top Bottom