Mwanahamisi Singano: Ndoa hazina maana tena

Ameandika Mwanahamisi Singano.

Labda wewe ni mmoja wa wengi ambao baada tu ya kusoma kichwa cha habari na jina la mwandishi, tayari hasira zimekupanda. Pengine unasoma haya makala siyo kwa sababu ya kutaka kujua kilichoandikwa, bali unasoma ili upate cha kukosoa na kunidogosha. Nikuombe ushushe pumzi! Kuwa mpole kidogo, ni vizuri kwa afya yako.

Alright! Najua wajua kuwa mijadala ya migogoro ya ndoa na ongezeko la talaka imeshika hatamu, huku waliojibatiza utaalam wa ndoa wakiwa busy kutoa uchambuzi na masomo kwa wanandoa hasa wanawake, na serikali ikianza kuhamasisha midahalo ya ndoa.

Kwa baadhi yetu tunaona jambo hili linafanywa kuwa jipya ila si jipya. Labda ukubwa umeongezeka. Pengine watu wamekuwa wepesi kulizungumzia kuliko ilivyokuwa awali, lakini migogoro na kuvunjika kwa ndoa ilikuwepo na ipo.

Tuseme tu ukweli. Watu wanaumia kwenye ndoa jamani. Wanawake kwa wanaume.

Mpaka leo kuna familia kama mume mtarajiwa hana nyumba, hana gari, hana kazi nzuri, hawakubali aoe binti yao, hata kama wanapendana kiasi gani. Kaka zangu walio kwenye ndoa wanajua jinsi matarajio yalivyo makubwa. Kuwa mume bora ni kuwa na kipato kikubwa kuliko mume wa rafiki wa mke wako na kumpa mkeo, mashemeji na wakwe, kila wanachotaka hata kama hakipo kwenye uwezo wako.

Shida ya afya ya akili ni kubwa mno kwa ‘wakaka’. Hawasemi tu. Wanalazimika kufanya dili hatari. Wanaumizana kenye kutafuta kipato na ‘wanasnichiana’, ili mradi ‘makasiriko’ kama yote ili ndoa iende. Kimsingi, tumevurugwa.

Huku kwa dada zangu ndio mtume salale. Hakuliki wala hakulaliki. Tunastiriwa na make-up tu.

Ila kila mtu analia na lake. Huyu analia mume hana muda naye, kama hayuko safari kikazi, yuko baa na marafiki, akiuliza, anajibiwa, kwani umekosa nini? Yule analia mume hajigusi kwenye majukumu ya kifamilia kwa kuwa mke ana kipato kikubwa.

Mke hakumbuki mara ya mwisho lini mume kumnunulia hata upande wa kanga, achia mbali kulipa ada au kununua bidhaa za nyumbani. Na akifungua mdomo kumuuliza anaambulia kipigo au matusi, eti anataka kumpanda kichwani mume kwa kuwa yeye ana hela kuliko mume.

Shangazi yangu mie analia machozi yasiyokauka. Kuamua kwake kuukimbia upweke na kuogopa dhambi ya kuzini kukamfanya akubali kuolewa mke mdogo, sasa anafanywa mwizi wa penzi la Bi Mkubwa. Anajiona hana thamani na hastahili mapenzi wala faraja ya mume. Huo uadilifu unaosemwa haujui unafananaje.

2-1.jpg

Na jirani yangu anasema japo anafanya kazi ngumu na anachoka kama punda mbeba mizigo jangwani, inabidi akirudi apike, afue n.k maana alishamfumania mumewe na mdada wa kazi. Tena mume akamkanya eti kama hatatimiza majukumu yake, ataoa dada wa kazi. Aibu ya kuolelewa dada kazi bora akomae na kufua majeans.

Halafu kuna wakina sie – Wasimbe.

Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa shida zote hizi zinakuja kwa sababu tumekataa kabisa kubadilisha taasisi ya ndoa, mfumo na matarajio ya wanandoa. Mpaka leo tunataka kuishi, kama wahenga walivyoishi kwenye zama za mawe za kale. Tunakwama. Ndoa zinakosa maana.

Zama hizo walizoishi wao waliyofanya yali-make sense. Kwa mfano, japokuwa wanadini wanaamini ndoa ilianza na Adam na Hawa/Eva, wataalam wa historia na sayansi ya jamii watakwambia ndoa kama taasisi ilianza pale ambapo jamii zilianza kukaa pamoja na kumiliki Rasilimali. Kabla ya hapo, kwa mujibu wa wataalam hao, watu walikuwa wanajamiiana ila si kwa taratibu za kindoa kama tunavyozijua sasa.

Enzi zile upatikanaji wa mali ulitokana na uwezo wa watu kutumia nguvu, iwe kuwinda, kutengeneza zana (za mawe au chuma), kulima, kuvua n.k. Wanafamilia wenye nguvu kazi kubwa (watu wengi) walikuwa na uwezo mkubwa wa kufanikiwa zaidi.

Kutokuwepo na mbinu za uzazi wa mpango kuliwafanya wanawake wengi, wawe aidha wana mimba au mtoto mchanga muda wote. Si mnaujua ule msemo wa ‘masika mimba, kiangazi mtoto’? Ewaaa, ndivyo ilivyokuwa!

Na hapo ndipo mgawanyo wa majukumu ulipotokea na shughuli na tamaduni za kuozeshana zilipoanza. Wanawake wakitolewa mahari ili wawe wazalishaji wa nguvukazi (watoto). Nguvukazi hiyo ilipewa ubini wa baba au wajomba kama alama ya umiliki. Pale ambapo walizaliwa watoto wa kike, basi baba au mjomba alipokea ‘mali’ (mahari) na kuwatoa mabinti zake wakazalishe nguvukazi kwenye jamii nyingine.

Uhitaji wa nguvukazi kubwa kwa haraka ulilazimisha wanaume waoe wake wengi. Ndoa za mitala zilikuwa ni jambo la kawaida kabisa. Kabla ya ujio wa dini zilizokataza au kuweka ukomo ya idadi ya wanawake wa kuoa, kwenye jamii nyingi za kale ukomo wa idadi ya wake ilitegemea ukomo wako wa kulipa mahari.

Katika jamii hizi, ndoa zilikuwa na kazi maalum, kuzalisha nguvu kazi, kuwa sehemu ya utambulisho wa mtu, kuwa taasisi ambayo mali na rasilimali zinamilika na kusaidia jamii kuendelea kwa maana ya mgawanyo wa kazi.

Pale ambapo wanaume walitoka kwenda kutafuta rizki, muda mwingine iliwachukua siku kadhaa, wanawake walibaki kijijini na kwa umoja wao wakilea nguvukazi na kufanya kazi za nyumbani ikiwa ni pamoja na kuzalisha chakula. Ndoa hazikuwa kuhusu mapenzi na mahaba, bali kutimiza mahitaji ya jamii (practical purposes).

3.jpg

Leo tuko mwaka 2022, tunausogelea mwaka 2023, rizIki na mali kwa sehemu kubwa hasa huku mijini, hazitafutwi tena kwa kutumia nguvu na misuli, bali akili na maarifa. Maboresho katika sekta ya elimu na kupanuka kwa huduma za uzazi wa mpango kumeongeza ushiriki wa wanawake kwenye shughuli za kiuchumi. Maendeleo ya teknolojia yameleta matarajio tofauti hasa kwenye sekta ya mahaba.

Ukuaji wa uchumi na kukua kwa miji kumevunja mshikamano wa Kijamii. Ubepari umeleta umimi na ubinafsishaji wa mali. Sasa mafanikio ya familia yanategemea zaidi ubora na si wingi wa wanafamilia. Katika muktadha huu tulitarajia kama jamii tuanze mchakato wa kubadilisha matarajio na labda mfumo wa ndoa.

Niliwahi kuongea na rafiki yangu mwanaume na kumuuliza kwa nini hataki kuoa tena baada ya kuachana na mtalaka wake? Jibu lake lilikuwa, “Naogopa mgogoro wa mali, hiki nilichokichuma nataka kirithiwe na wanangu, ndoa zetu ni ‘all inclusive’, chake changu na changu chake, sasa kwa sisi ambao tuna watoto ukioa tena unatafuta majanga kuliko furaha.”

Majibu yake yalinifanya nimvutie waya swahiba wangu, msimbe mwenzangu, nimpe hizi habari njema kuwa kuna wakaka ambao wanataka kuwa na mahusiano/ndoa ila wanaogopa migogoro ya mali, mana huyu swahiba wangu kila siku alikuwa anasema, yeye hafuati mali kwenye ndoa, ana zake.

Kiherehere changu kilizimishwa na majibu yake mafupi ila mazito, aliniambia, “Mishy, wakaka wengi kama hao wako emotionally unavailable, wanataka tu kuwa na independent women but they have no idea, what to do with them.” Hapa alikuwa anamaanisha kuwa wanaume wa aina hiyo hawana muda wa kuwa pamoja na wewe vilivyo kihisia, wanataka tu kuwa na wanawake walio huru na wanaojitegemea lakini hawajui wafanye nini na wanawake hao wanapokuwa nao.

Kimsingi, alinieleza yeye anataka kuwa na mwenza atakayekuwa mwandani, msiri, na mfariji wake. Mwenza wa kumuonea ruhuma, wa kumtia moyo, wa kufurahi na kuhuzinika nae. Kwa kizungu tungesema soulmate maana kwa mujibu wake, japo anaweza kukimbizana na maisha, na anajua kuitafuta pesa haswa, ila kuna hitaji la moyo la kupendwa na kujaliwa.

Shida ni pale huyo mwenza, na jamii inayomzunguka, bado wanapokuwa na matarajio yaleyale ya mke wa zama za mawe za kale. Ndoa haitakuwa ‘yeye (mke) anataka nini’ bali ‘mume anataka nini’. Hakuna hata kauchochoro ka kusema, basi tupange wote tunataka nini – utaambiwa wewe sio wife material, sio kama bibi zetu. Hawakumbuki kuwa bibi zetu hawaishi maisha yetu. Kigumu ni kipi hapo kuelewa?

Anyways, kwa hapa tulipofika, ndoa siyo tena sehemu ya kuanza au kupata maisha. Siku hizi wadada na wakaka wote wanaweza kuyatafuta maisha nje ya ndoa na wakafanikiwa. Siyo tena sehemu pekee ya kupata watoto maana zamani kuzaa nje ya ndoa dunia ingeweza kukumeza mzimamzima. Ila siku hizi wala. Mpaka baadhi ya makanisa yana utaratibu wa kurejesha watu kundini japo sijawahi kuona wakaka wanarejeshwa kundini kwa kuzaa nje.

4.jpg

Ndoa sasa zinaacha kuwa kipimo pekee cha mafanikio na heshima, japo ka-pressure bado kapo hasa kwa wadada. Ila nawajua wadada na wakaka wengi wanaoana ili ‘watoe nuksi’ basi ‘waridhishe wazazi’ na maisha yanaendelea kuwa bukheri baada ya talaka. Mjini wanasema heshima pesa, mengine yanaongeleka.

Maana pekee iliyobaki ni ya kiimani. Katika jamii zetu ambazo dhambi haziogopwi kivile tena, siku si nyingi maana hii nayo itapotea. Kama alivyoniambia kaka yangu senior bachela, kuliko kujibebesha stress za kuandaa harusi za gharama, kuishi maisha ya kuwafurahisha wakwe na kudeal na mke na shida zake, bora aendelee kuwa na rafiki tu, atatubu.

Kama kweli, tunataka ndoa ziendelee kuwepo, basi tuzitafutie maana mpya na mifumo mipya inayoakisi mahitaji wa wanandoa wa karne hii ya ishirini na moja. La sivyo tutaendelea kuhesabu talaka, single mothers and fathers na ongezeko la kutisha la ukatili wa kijinsi(a) pamoja na mauaji baina ya wenza. Ni muda sasa wataalam wa sayansi wa jamii kuanzia wanasosholojia hadi wanasaikolojia kufanya kazi yao ipasavyo au tuendelee kutia ndoa doa.
kauli mbiu ni ile ile " HAKUNA KUOA " 😁😁
 
Wakati wew na wanasosholojia wako mkiandaa reforms kwa ajili ya ndoa, nakukumbusha tu kwamba kwa sisi waislam al maaruf kam wavaa kobadh kwa hapa jukwaani.

Sisi kwetu ndoa ni ibada yenye hadhi ya nusu ya dini, na kama ni ibada basi kitabu chetu kitukufu kimeshaelekeza taratibu za ibada zote.

Sasa kubadili sheria za kiibada ni sawa na kumchokoza alieziweka, na aliziweka akijua kuwa itakuja karne ya ishin na moja na alijua itakuwaje sas kwa vile anaifaham karne hii kama itampendeza atatoa maelekezo yeye mwenyewe ya kubadili au kumantain, manake sie tumekatazwa kupunguza wala kuongeza doctrines katika mambo ya kidini ikiwemo ndoa. So kwa niaba ya wavaa kobadh acces denied.

Me niseme tu kwa dhati kwamba ninyi wanawake wa kisomi mkijihic mmeota mapembe kwa taaluma za mlimani bas mna hiari ya kukataa kuolewa.

Mama na dada mliopo hapa: hakunaga viongozi wawili wanaolingana mamlaka sehemu moja, ni lazma mmoja awe juu na wa chini areceiv orders ama nyie elimu yenu inasema vp? Mnadanganywa na Marekani? Taasisi ni ileile ambae hataki akumbatie mto.
Ukweli kabisa hata wazungu walitumia logic sana katika vipando vyetu kama gari pawe na dereva mmoja hata ndege wapo kibao ila Kuna capten mkuu mmoja kama meli katika uendeshaji.
 
Hakuna maisha yasiyokua na mfumo. Na kitu chochote kinachofanyika bila kuzingatia mfumo lazima kiyumbe.

Kuna mfumo unaoendesha maisha ya ndoa. Huu mfumo usipozingatiwa lazima ndoa iyumbe.

Anachozungumza mwandishi ni kwamba hii mifumo inayoendesha maisha ya ndoa inabidi iendane na wakati kwasababu bila kuendana na wakati ni lazima ilete confusion kwa wanandoa.

Mtu yoyote mwenye akili timamu anaelewa umuhimu wa ndoa.
Na ukitaka kuthibitisha kwamba ndoa ina umuhimu mkubwa, ndugu Maxence Melo mwenyewe ana ndoa.

Tunaohangaika ni sisi wenye uelewa finyu kuhusu ndoa. Na wewe kujeruhika na mahusiano hapaondoi umuhimu wa ndoa.

HEAL YOUR WOUNDS THEN FIND LOVE AGAIN. Hakuna kitu kinasononesha kama kuzeeka mwenyewe.
nahc kama sijaelewa maana ya wakati katika hii mada ! Viburi vya wanawake wasomi ndo vinaitwa wakati? Kama ni hivyo wacha wazeeke wakiwa wapweke..na kinachonikera ni kuwalisha matangopori wanawake ambao hawakwenda vyuoni huko kwenye vikundi vyao..kwa maoni yangu wote watakumbatia mito katk karne hii.
 
Tukatae Ndoa, Ndoa inamnufaisha KE huku ME akiteketea

Kataa Ndoa
Pale utakapoanza kuzeeka, ukalazwa chini na madhaifu pamoja na magonjwa ya uzee, ukakosa mtu wa kutuma hata maji ya kunywa au pharmacy, wakati huo pisi wote wame-block cm yako na ndugu wamekutelekeza, ndo utajua hujui na itakuwa ushachelewa..

Hekima ni kujitahidi kutafuta na kuoa mwenza mwenye afadhali, siyo kukataa Ndoa!
 
haha endelea kuota
 
nahc kama sijaelewa maana ya wakati katika hii mada ! Viburi vya wanawake wasomi ndo vinaitwa wakati? Kama ni hivyo wacha wazeeke wakiwa wapweke..na kinachonikera ni kuwalisha matangopori wanawake ambao hawakwenda vyuoni huko kwenye vikundi vyao..kwa maoni yangu wote watakumbatia mito katk karne hii.
Umeuliza swali zuri mkuu kwamba viburi vya wanawake wasomi ndo vinaitwa wakati?

Zamani wanawake walikua wanabanwa kupata elimu ila siku hizi wana uwezo wa kusoma mpka levo za juu. Sasa mzungu anasema KNOWLEDGE IS POWER. Usitarajie mwanamke wa sasa mwenye elimu yake na mihela yake akawa mnyonge kama hawa bibi zetu.

Tunapokwama sisi wanaume ni kushindwa kujiadjust namna ya kuishi na huyu mwanamke mwenye elimu na mwenye nguvu ya kiuchumi ambae huwezi ukamtisha kwa kutumia hivyo vitu kwa sababu yeye mwenyewe anauwezo wa kuvitafuta na kuvipata.

Elimu na ajira kwa wanawake vimempa mwanamke wa leo uwezo mkubwa wa kuhudumia familia na kuwa na opinion katika family matters.

Sisi wanaume nguvu zetu kwenye ndoa zimelalia kwenye kuwa na uwezo wa kuilisha na kuihudumia familia na kutoa maamuzi. Sasa huyu mwanamke wa kileo mwenye elimu na nguvu ya kiuchumi ana uwezo sawasawa na sisi ndo mana tunaogopa kuwa nao tukihisi uanaume wetu utakuwa CHALLENGED kwenye ndoa.

Mimi nadhani tusitake wanawake zetu wa leo wawe kama bibi zetu sababu hata sisi hatupo kama babu zetu.

tukiweza kuji-tune na hii dunia ya sasa na mwanamke wa kisasa ndoa zitaweza kusavaiv.
 
Ameandika Mwanahamisi Singano.

Labda wewe ni mmoja wa wengi ambao baada tu ya kusoma kichwa cha habari na jina la mwandishi, tayari hasira zimekupanda. Pengine unasoma haya makala siyo kwa sababu ya kutaka kujua kilichoandikwa, bali unasoma ili upate cha kukosoa na kunidogosha. Nikuombe ushushe pumzi! Kuwa mpole kidogo, ni vizuri kwa afya yako.

Alright! Najua wajua kuwa mijadala ya migogoro ya ndoa na ongezeko la talaka imeshika hatamu, huku waliojibatiza utaalam wa ndoa wakiwa busy kutoa uchambuzi na masomo kwa wanandoa hasa wanawake, na serikali ikianza kuhamasisha midahalo ya ndoa.

Kwa baadhi yetu tunaona jambo hili linafanywa kuwa jipya ila si jipya. Labda ukubwa umeongezeka. Pengine watu wamekuwa wepesi kulizungumzia kuliko ilivyokuwa awali, lakini migogoro na kuvunjika kwa ndoa ilikuwepo na ipo.

Tuseme tu ukweli. Watu wanaumia kwenye ndoa jamani. Wanawake kwa wanaume.

Mpaka leo kuna familia kama mume mtarajiwa hana nyumba, hana gari, hana kazi nzuri, hawakubali aoe binti yao, hata kama wanapendana kiasi gani. Kaka zangu walio kwenye ndoa wanajua jinsi matarajio yalivyo makubwa. Kuwa mume bora ni kuwa na kipato kikubwa kuliko mume wa rafiki wa mke wako na kumpa mkeo, mashemeji na wakwe, kila wanachotaka hata kama hakipo kwenye uwezo wako.

Shida ya afya ya akili ni kubwa mno kwa ‘wakaka’. Hawasemi tu. Wanalazimika kufanya dili hatari. Wanaumizana kenye kutafuta kipato na ‘wanasnichiana’, ili mradi ‘makasiriko’ kama yote ili ndoa iende. Kimsingi, tumevurugwa.

Huku kwa dada zangu ndio mtume salale. Hakuliki wala hakulaliki. Tunastiriwa na make-up tu.

Ila kila mtu analia na lake. Huyu analia mume hana muda naye, kama hayuko safari kikazi, yuko baa na marafiki, akiuliza, anajibiwa, kwani umekosa nini? Yule analia mume hajigusi kwenye majukumu ya kifamilia kwa kuwa mke ana kipato kikubwa.

Mke hakumbuki mara ya mwisho lini mume kumnunulia hata upande wa kanga, achia mbali kulipa ada au kununua bidhaa za nyumbani. Na akifungua mdomo kumuuliza anaambulia kipigo au matusi, eti anataka kumpanda kichwani mume kwa kuwa yeye ana hela kuliko mume.

Shangazi yangu mie analia machozi yasiyokauka. Kuamua kwake kuukimbia upweke na kuogopa dhambi ya kuzini kukamfanya akubali kuolewa mke mdogo, sasa anafanywa mwizi wa penzi la Bi Mkubwa. Anajiona hana thamani na hastahili mapenzi wala faraja ya mume. Huo uadilifu unaosemwa haujui unafananaje.

2-1.jpg

Na jirani yangu anasema japo anafanya kazi ngumu na anachoka kama punda mbeba mizigo jangwani, inabidi akirudi apike, afue n.k maana alishamfumania mumewe na mdada wa kazi. Tena mume akamkanya eti kama hatatimiza majukumu yake, ataoa dada wa kazi. Aibu ya kuolelewa dada kazi bora akomae na kufua majeans.

Halafu kuna wakina sie – Wasimbe.

Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa shida zote hizi zinakuja kwa sababu tumekataa kabisa kubadilisha taasisi ya ndoa, mfumo na matarajio ya wanandoa. Mpaka leo tunataka kuishi, kama wahenga walivyoishi kwenye zama za mawe za kale. Tunakwama. Ndoa zinakosa maana.

Zama hizo walizoishi wao waliyofanya yali-make sense. Kwa mfano, japokuwa wanadini wanaamini ndoa ilianza na Adam na Hawa/Eva, wataalam wa historia na sayansi ya jamii watakwambia ndoa kama taasisi ilianza pale ambapo jamii zilianza kukaa pamoja na kumiliki Rasilimali. Kabla ya hapo, kwa mujibu wa wataalam hao, watu walikuwa wanajamiiana ila si kwa taratibu za kindoa kama tunavyozijua sasa.

Enzi zile upatikanaji wa mali ulitokana na uwezo wa watu kutumia nguvu, iwe kuwinda, kutengeneza zana (za mawe au chuma), kulima, kuvua n.k. Wanafamilia wenye nguvu kazi kubwa (watu wengi) walikuwa na uwezo mkubwa wa kufanikiwa zaidi.

Kutokuwepo na mbinu za uzazi wa mpango kuliwafanya wanawake wengi, wawe aidha wana mimba au mtoto mchanga muda wote. Si mnaujua ule msemo wa ‘masika mimba, kiangazi mtoto’? Ewaaa, ndivyo ilivyokuwa!

Na hapo ndipo mgawanyo wa majukumu ulipotokea na shughuli na tamaduni za kuozeshana zilipoanza. Wanawake wakitolewa mahari ili wawe wazalishaji wa nguvukazi (watoto). Nguvukazi hiyo ilipewa ubini wa baba au wajomba kama alama ya umiliki. Pale ambapo walizaliwa watoto wa kike, basi baba au mjomba alipokea ‘mali’ (mahari) na kuwatoa mabinti zake wakazalishe nguvukazi kwenye jamii nyingine.

Uhitaji wa nguvukazi kubwa kwa haraka ulilazimisha wanaume waoe wake wengi. Ndoa za mitala zilikuwa ni jambo la kawaida kabisa. Kabla ya ujio wa dini zilizokataza au kuweka ukomo ya idadi ya wanawake wa kuoa, kwenye jamii nyingi za kale ukomo wa idadi ya wake ilitegemea ukomo wako wa kulipa mahari.

Katika jamii hizi, ndoa zilikuwa na kazi maalum, kuzalisha nguvu kazi, kuwa sehemu ya utambulisho wa mtu, kuwa taasisi ambayo mali na rasilimali zinamilika na kusaidia jamii kuendelea kwa maana ya mgawanyo wa kazi.

Pale ambapo wanaume walitoka kwenda kutafuta rizki, muda mwingine iliwachukua siku kadhaa, wanawake walibaki kijijini na kwa umoja wao wakilea nguvukazi na kufanya kazi za nyumbani ikiwa ni pamoja na kuzalisha chakula. Ndoa hazikuwa kuhusu mapenzi na mahaba, bali kutimiza mahitaji ya jamii (practical purposes).

3.jpg

Leo tuko mwaka 2022, tunausogelea mwaka 2023, rizIki na mali kwa sehemu kubwa hasa huku mijini, hazitafutwi tena kwa kutumia nguvu na misuli, bali akili na maarifa. Maboresho katika sekta ya elimu na kupanuka kwa huduma za uzazi wa mpango kumeongeza ushiriki wa wanawake kwenye shughuli za kiuchumi. Maendeleo ya teknolojia yameleta matarajio tofauti hasa kwenye sekta ya mahaba.

Ukuaji wa uchumi na kukua kwa miji kumevunja mshikamano wa Kijamii. Ubepari umeleta umimi na ubinafsishaji wa mali. Sasa mafanikio ya familia yanategemea zaidi ubora na si wingi wa wanafamilia. Katika muktadha huu tulitarajia kama jamii tuanze mchakato wa kubadilisha matarajio na labda mfumo wa ndoa.

Niliwahi kuongea na rafiki yangu mwanaume na kumuuliza kwa nini hataki kuoa tena baada ya kuachana na mtalaka wake? Jibu lake lilikuwa, “Naogopa mgogoro wa mali, hiki nilichokichuma nataka kirithiwe na wanangu, ndoa zetu ni ‘all inclusive’, chake changu na changu chake, sasa kwa sisi ambao tuna watoto ukioa tena unatafuta majanga kuliko furaha.”

Majibu yake yalinifanya nimvutie waya swahiba wangu, msimbe mwenzangu, nimpe hizi habari njema kuwa kuna wakaka ambao wanataka kuwa na mahusiano/ndoa ila wanaogopa migogoro ya mali, mana huyu swahiba wangu kila siku alikuwa anasema, yeye hafuati mali kwenye ndoa, ana zake.

Kiherehere changu kilizimishwa na majibu yake mafupi ila mazito, aliniambia, “Mishy, wakaka wengi kama hao wako emotionally unavailable, wanataka tu kuwa na independent women but they have no idea, what to do with them.” Hapa alikuwa anamaanisha kuwa wanaume wa aina hiyo hawana muda wa kuwa pamoja na wewe vilivyo kihisia, wanataka tu kuwa na wanawake walio huru na wanaojitegemea lakini hawajui wafanye nini na wanawake hao wanapokuwa nao.

Kimsingi, alinieleza yeye anataka kuwa na mwenza atakayekuwa mwandani, msiri, na mfariji wake. Mwenza wa kumuonea ruhuma, wa kumtia moyo, wa kufurahi na kuhuzinika nae. Kwa kizungu tungesema soulmate maana kwa mujibu wake, japo anaweza kukimbizana na maisha, na anajua kuitafuta pesa haswa, ila kuna hitaji la moyo la kupendwa na kujaliwa.

Shida ni pale huyo mwenza, na jamii inayomzunguka, bado wanapokuwa na matarajio yaleyale ya mke wa zama za mawe za kale. Ndoa haitakuwa ‘yeye (mke) anataka nini’ bali ‘mume anataka nini’. Hakuna hata kauchochoro ka kusema, basi tupange wote tunataka nini – utaambiwa wewe sio wife material, sio kama bibi zetu. Hawakumbuki kuwa bibi zetu hawaishi maisha yetu. Kigumu ni kipi hapo kuelewa?

Anyways, kwa hapa tulipofika, ndoa siyo tena sehemu ya kuanza au kupata maisha. Siku hizi wadada na wakaka wote wanaweza kuyatafuta maisha nje ya ndoa na wakafanikiwa. Siyo tena sehemu pekee ya kupata watoto maana zamani kuzaa nje ya ndoa dunia ingeweza kukumeza mzimamzima. Ila siku hizi wala. Mpaka baadhi ya makanisa yana utaratibu wa kurejesha watu kundini japo sijawahi kuona wakaka wanarejeshwa kundini kwa kuzaa nje.

4.jpg

Ndoa sasa zinaacha kuwa kipimo pekee cha mafanikio na heshima, japo ka-pressure bado kapo hasa kwa wadada. Ila nawajua wadada na wakaka wengi wanaoana ili ‘watoe nuksi’ basi ‘waridhishe wazazi’ na maisha yanaendelea kuwa bukheri baada ya talaka. Mjini wanasema heshima pesa, mengine yanaongeleka.

Maana pekee iliyobaki ni ya kiimani. Katika jamii zetu ambazo dhambi haziogopwi kivile tena, siku si nyingi maana hii nayo itapotea. Kama alivyoniambia kaka yangu senior bachela, kuliko kujibebesha stress za kuandaa harusi za gharama, kuishi maisha ya kuwafurahisha wakwe na kudeal na mke na shida zake, bora aendelee kuwa na rafiki tu, atatubu.

Kama kweli, tunataka ndoa ziendelee kuwepo, basi tuzitafutie maana mpya na mifumo mipya inayoakisi mahitaji wa wanandoa wa karne hii ya ishirini na moja. La sivyo tutaendelea kuhesabu talaka, single mothers and fathers na ongezeko la kutisha la ukatili wa kijinsi(a) pamoja na mauaji baina ya wenza. Ni muda sasa wataalam wa sayansi wa jamii kuanzia wanasosholojia hadi wanasaikolojia kufanya kazi yao ipasavyo au tuendelee kutia ndoa doa.
Hili lipo wazi kabisa na uliyo yaandika ndio yanayotokea saa hii, ndio mana waoaji wamepungua sana.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Inasaidia. Waislam wana furaha na ndoa zao ukilinganisha Wakristo.

Wakristo wanaume wanakufa haraka kuliko Waislamu.

Waislamu wanzidi kuwa vijana huku Wakristo wakizeeeka mapema zaidi.

Na hili ni kutokana na uhuru walionao Waislamu huku Wakristo wakifungwa na sheria za Kanisa na ile ya Ndoa katika suala zima la kufunga ndoa na malezi
Acha uongo hakuna ndoa za kikafiri kama za waislam walahi ni wapumbavu sana wanaume tena ndio mpangwe weh no shida kubwa bora mtu anajua anamke mmoja

Maana ngoja nikupashe watu wakishapendana wakajuana vyema na kuwekeana mipaka ndoa itadumu muislamu gani amweshimu mkewe sindoto .
Walahi hawaeshimu wake zao wanawaweka kama products zao za madukani upendo zero , wao nimaonyesho tu mwislamu huwa anavisasi
 
Umeuliza swali zuri mkuu kwamba viburi vya wanawake wasomi ndo vinaitwa wakati?

Zamani wanawake walikua wanabanwa kupata elimu ila siku hizi wana uwezo wa kusoma mpka levo za juu. Sasa mzungu anasema KNOWLEDGE IS POWER. Usitarajie mwanamke wa sasa mwenye elimu yake na mihela yake akawa mnyonge kama hawa bibi zetu.

Tunapokwama sisi wanaume ni kushindwa kujiadjust namna ya kuishi na huyu mwanamke mwenye elimu na mwenye nguvu ya kiuchumi ambae huwezi ukamtisha kwa kutumia hivyo vitu kwa sababu yeye mwenyewe anauwezo wa kuvitafuta na kuvipata.

Elimu na ajira kwa wanawake vimempa mwanamke wa leo uwezo mkubwa wa kuhudumia familia na kuwa na opinion katika family matters.

Sisi wanaume nguvu zetu kwenye ndoa zimelalia kwenye kuwa na uwezo wa kuilisha na kuihudumia familia na kutoa maamuzi. Sasa huyu mwanamke wa kileo mwenye elimu na nguvu ya kiuchumi ana uwezo sawasawa na sisi ndo mana tunaogopa kuwa nao tukihisi uanaume wetu utakuwa CHALLENGED kwenye ndoa.

Mimi nadhani tusitake wanawake zetu wa leo wawe kama bibi zetu sababu hata sisi hatupo kama babu zetu.

tukiweza kuji-tune na hii dunia ya sasa na mwanamke wa kisasa ndoa zitaweza kusavaiv.
Mwanamke yeyote atakudharau sana hata kama hana elimu usipojitambua
 
Sheria iruhusu Wakristo huoa wake wengi ili kuondoa dhana ya michepuko. Case ya Elizabeth Mohamed vs John Magesa, Mahakama Kuu ilitoa msimamo mzuri sana wa sheria, kwamba, Mahakama inatambua kuwa Wakristo wanaweza kuwa na mke zaidi ya mmoja, na kwamba watoto wote ni sawa, haijalishi wamezaliwa na mke yupi.

Pia mahakama iliamua kwamba whether Mkristo katenda kosa kwa kuwa na wake wengi, hilo ni suala la kuamuliwa na sheria za kanisa (Canon Laws) na siyo suala la mahakama maana mahakama haina dini.

Huu ni msimamo wa mahakama japo upo Sheria ya Ndoa inasema vingijevyo
Wanaume hata mpewe dunia hamridhiki mf. Sulemani
 
Hao wataalamu wenyewe sasa ambao wapo serikalini mtihani mkubwa. Ila nikupongeze kwa andiko zuri. Kwa kifupi umeandika hoja nzito sana.

Nimekuelewa zaidi hasa katika eneo la kuitafutia ndoa maana mpya badala ya kushika maana au mahitaji ya ndoa kwa sababu za kikale.

Ila sasa nilikuwa nataka kuhoji jambo, haiwezekani kuwa tuna changamoto ya kutoa mafunzo ya ndoa kama taasisi kuu kijamii na kitaifa na kuiwekea misingi ya kuhehsimiwa ikiwamo kuwa na kanuni na sheria za kuisimamia kiserikali na pia kuwa na mifumo ya kijamii kama Jando na Unyago?

Maana kwa nilichokiona sasa ni kwamba ukiacha haya mafunzo ya juu juu ya ndoa kama kitchen party, semina za makanisani na taasisi za kiimani, ambayo hayalengi kutrain watu seriously na kuwaandaa kwaajiri ya NDOA bali ni kama kupiga soga tu juu ya changamoto za kindoa, hakuna platforms kama zilizokuwapo miaka hiyo ambapo mtoto wa kike alikuwa anakalishwa chini anafunzwa na akina mama wanaoitumikia ndoa na kuitambua kama taasisi muhimu katika jamii kiasi kwamba akitoka hapo hata akakutane na mwanaume wa aina gani atajua kumudu kuishi nae kama mume na kuweza kufika mbali nae.

Pia watoto wa kiume walikuwa wakipewa mafunzo yao ya Jandoni kuwajenga kuwa na kaliba ya kiume na kujua wajibu na majukumu yao kifamilia na sio kutangatanga na kuzaa hovyo kama mbwa koko.

Kimsingi nadhani tunahitaji haya mafunzo yarejee kwenye jamii na kuaddress hili uliloliandika. Kimsingi mahitaji ya ndoa ni yake yale ila Shughuli za kiuchumi na kiasiasa ndizo zimeingilia masilahi ya ndoa.

Ndoa ikiheshimiwa kama taasisi namba moja katika taifa na Serikali ikaacha kiherehere cha kuingilia maswala ya Ndoa na kuwa muamuzi pekee wa nini kifanyike katika Ndoa huku ikipuuza asili ya jamii husika, tamaduni, maadili, na nguvu ya wanafamilia katika kusimamia haya mambo tutafeli mchana kweupe.

Nishauri tu kwa sasa tuanze kuchukua hatua sababu madhara yanayokuja kutokea miaka 100 kutoka sasa kwa namna hali jinsi ilivyo sidhani kama tutakuwa na salama ya kizazi chetu. Na yote ni matokeo ya kupuuza misingi au kutokutazama upya misingi ili jamii iweze kushikiria ndoa na kuiheshimu.
 
We ni mfano wa kuigwa. Ulichokiongelea unakifahamu vizuri. Nimemiss thread kama hizi hapa JF, za kutufunza mambo ya maisha.. sio kushabikia vita ya urusi na ukrein kwa milengo ya kidini.

Naungana na wew, kuna haja ya kufanya reform namna ya ndoa inavyopaswa kuendeshwa haswa tuanzie kwenye vitabu vya dini na hii fifte fifte inayo trend huku mjini.
Reform gani? Ndoa ni ibada.full stop
Ndoa angalia hata kina princess diana ziliwashinda haya wao nao kigezo ni nini ? Mali zipo.madaraka yapo kola kitu cha fahari walichotaka duniani walipata,nenda kwa mstaa duniani wana kila aina ya ufahari vop nao.huwez kuwa na reform.reform unauosema wewe watu wabakane majiani humo.huyu akimuona yule amkimbize kama kuku mana ndio unavotaka
 
Wakati wew na wanasosholojia wako mkiandaa reforms kwa ajili ya ndoa, nakukumbusha tu kwamba kwa sisi waislam al maaruf kam wavaa kobadh kwa hapa jukwaani.

Sisi kwetu ndoa ni ibada yenye hadhi ya nusu ya dini, na kama ni ibada basi kitabu chetu kitukufu kimeshaelekeza taratibu za ibada zote.

Sasa kubadili sheria za kiibada ni sawa na kumchokoza alieziweka, na aliziweka akijua kuwa itakuja karne ya ishin na moja na alijua itakuwaje sas kwa vile anaifaham karne hii kama itampendeza atatoa maelekezo yeye mwenyewe ya kubadili au kumantain, manake sie tumekatazwa kupunguza wala kuongeza doctrines katika mambo ya kidini ikiwemo ndoa. So kwa niaba ya wavaa kobadh acces denied.

Me niseme tu kwa dhati kwamba ninyi wanawake wa kisomi mkijihic mmeota mapembe kwa taaluma za mlimani bas mna hiari ya kukataa kuolewa.

Mama na dada mliopo hapa: hakunaga viongozi wawili wanaolingana mamlaka sehemu moja, ni lazma mmoja awe juu na wa chini areceiv orders ama nyie elimu yenu inasema vp? Mnadanganywa na Marekani? Taasisi ni ileile ambae hataki akumbatie mto.
Umenena vema.
 
Back
Top Bottom