Mwanafunzi Mtanzania kakutwa amekufa/ameuawa Bangalore India

Poleni wafiwa.
Kifo hakizoeleki. Tusubiri postmortem ili kujua yanayowezekana kuwa yalijili. Yaweza kuwa ajali au kuawa. Hili la ubaguzi wa rangi si hoja kubwa kwani wao kwa wao wanabaguana sana, ni sehemu ya utamaduni wao kutomjali mtu asiye wa 'caste' yako. Tuliokaa India tunajua hayo. Dawa na kuheshimu hiyo mipaka na kustick together hasa ukiwa na rafiki mwenye dada utachungwa kishenzi. Inaweza kuwa boring lakini ni kwa muda mfupi tu.
MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI
 
What a tragedy! Lazima Raj Patel (the usual suspect) atakuwa anahusika na hii murder.
 
Pia inapatikana Coast blogspoat:

SURA ZA HUZUNI NA MAJONZI - BANGALORE-INDIA.


Baadhi ya wanafunzi waliokusanyika katika msiba huo wakiwa na nyuso za huzuni.






Sura za Huzuni na Majonzi kwa wanafunzi wa India waliopo Bangalore na Wenzao wa Mysore baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Muwakilishi wa Ubalozi Mr. Amon Mwamunenge juu ya maendeleo ya uchunguzi na taratibu za kusafirisha mwili wa Marehemu Imran Mtui kurudi nyumbani kwa ajili ya mapumziko ya amani.








Mwanafunzi Mtanzania, Imran Mtui auawa India





Habari zilizopo katika blogu ya Watanzania waishio Bangalore (TASABA), pia katika mtandao wa Twitter zinathibitisha kuwa, mwanafunzi wa Kitanzania, Imran Mtui (31) aliyekuwa anasoma katika Chuo kishiriki Cha Chuo Kikuu cha Bangalore nchini India, amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa hauna kichwa.

Taarifa zinasema kuwa mwili huo ulikutwa kando kando ya reli katika eneo la Shivajinagar katika mji wa Bangalore ukiwa hauna kichwa huku mguu mmoja ukiwa umejeruhiwa vibaya.Balozi wa Tanzania nchini India, John Kijazi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

"Mimi nilipata taarifa hizo juzi jioni ambapo jana tulifanya kikao na wenzangu na kumtuma Ofisa wetu Mzee Amon Mwamanenge na mwanasheria wetu wamekwenda huko kupata undani wa tukio hilo," alisema Balozi Kijazi.

Alisema kuwa kwa sasa hawezi kutoa picha kamili lakini mwili wa kijana huyo umekutwa ukiwa hauna kichwa na mguu umebondeka. Kijana huyo aliyefariki alikuwa amemaliza Shahada ya Usimamizi wa Biashara (BBM) na alitambulika kwa jina la Imran Mtui. Aliwahi kuwa Mtunza Fedha wa Chama Cha Wanafunzi wa Kitanzania Waishio Bangalore (TASABA).

Habari hizi zimedhibitishwa na mdogo wa marehemu, Issa Mtui, kwa njia ya simu akiwa safarini kuelekea Marangu, Moshi. Alieleza kuwa mwili wa marehemu unategemewa kuwasili nchini Alhamisi ya wiki hii kwa ajili ya taratibu za mazishi ambayo yatafanyikia Marangu.


Imrani ni wa pili kuzaliwa kati ya watoto wanne kwenye familia hiyo. Inadaiwa kuwa kabla mauti haijamkuta alitarajiwa jana angekuwa amerejea nchini baada ya kuwa amechukua vyeti vyake vya masomo ambavyo alikuwa akivisubiri baada ya kuhitimu masomo yake.

Polisi nchini India wanaendelea na jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wa tukio hilo.
 
Wasichana wa JF bwana!! Ina maana asingekuwa hansome msingehuzunika? Better to be silent !!

Jamani kuna ubaya gani kusema kijana was good looking wengine si wasichana kama ufikiriavyo
 
Jamani kuna ubaya gani kusema kijana was good looking wengine si wasichana kama ufikiriavyo

hamna ubaya wowote ukweli, he was handsome yes na hiyo si sababu pekee iliyotufanya tusikitike. binafsi nimesikitishwa na such a young person kukatiliwa maisha tena ndo kwanza amemaliza masoma ready to contribute to the progress of his family and the nation at large!!!!
 
Maskini mtoto wa watu, Mungu aipokee roho ya marehemu Imran na apumzike kwa amani, Amin. Pole nyingi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Imran. Ni uchungu mkubwa kwa wazazi wa huyu kijana, Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
 
Hivi uongozi wa nchi yetu uko serious kwenye kitu gani???Maanake naona mambo yote iko hovyo hovyo tuu.I'm very sad.RIP IMRAN.
 
messed up shituation... wasiwasi umekuwa unanipanda vile wao wanavonyanyaswa kule Australia, nimehisi watatanyanyasa wanaosoma nchini mwao .... jus an observation. May he rest in peace.

ps: ka Bujibuji alivotuambia... askari wahindi ni wabaguzi... wenyewe tu wanaweza kutuchinja badala ya kutulinda

pps: tulivo na waHindi/waTanzania wengi, sirikali yetu inaweza kuwa na sauti kubwa kwa viongozi wa India... ama wananchi wakichoka wata-Idi Amin wahindi ... don't wanna see dat, but human nature goes crazy and often unjustly in fighting for justice... it happens.
 
RIP Imran Mtui... sasa huyo Askari wa kibongo akifika huko India si itakuwa YU NOOO... ZEEEE.... ZEEE .... MY NEMUUU... Duh lazima atadunda.... Wizara husika ipeleke team kubwa kama inavyopeleka Davos,Addis etc... kwa mara nyingine RIP Imran Mtui...
 
RIPOTI RASMI YA KIFO CHA BWANA "IMRAN MTUI"


Mnamo siku ya jumapili ya tarehe 31/01/2010, majira ya 9:30 alasiri uongozi wa wanafunzi waishio Bangalore India (TASABA) tulipokea taarifa ya kusikitisha kutoka kwa ndugu wa karibu wa marehemu kuwa kaka yetu mpendwa IMRAN MTUI kuwa tena duniani.
Mnamo majira ya saa tatu usiku mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi waishio Bangalore (TASABA) Mh. Fidelis Msomekela aliwasiliana na ubalozi wa Tanzania New Delhi kuwafahamisha juu ya msiba wa mpendwa kaka yetu marehemu IMRAN MTUI.
Tarehe 1/02/2010 ofisi ya Ubalozi ilituma mwakilishi wake anayesimamia maswala ya wanafunzi India ili kusaidiana na serikali ya wanafunzi waishio Bangalore kujua chanzo zaidi juu ya kifo cha marehemu Imran Mtui.
Tarehe 2/01/2010, Mwakilishi wa ubalozi pamoja a mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi Bangalore (TASABA) walifika katika kituo cha polisi kiitwacho ‘Cantonment Railway Police' ili kupata ripoti kamili juu ya chanzo cha kifo cha marehu Imran Mtui. Ripoti ya polisi ilieleza kuwa mnamo majira ya saa 3:35 asubuhi mkaguzi wa reli alitoa taarifa kwa msismamizi mkuu wa reli kuwa ameona mwili wa marehemu IMRAN MTUI pembeni ya reli K.M No. 339/700-800 karibu na KRISHNARAJAPURAM LOCO SHED (MAHADEVAPUR, BANGALORE).
Taarifa za awali za polisi zinaeleza kuwa chanzo cha kifo cha marehemu Imran Mtui ni Ajali ya kawaida, uchunguzi zaidi unaendelea ili kujua chanzo kamili cha kifo cha ndugu yetu marehemu IMRAN MTUI.
Taratibu zote za kusafirisha mwili wa marehemu IMRAN MTUI zimekamilika, kesho (3/01/2010) majira ya jioni, mwili wa marehemu IMRAN MTUI utasafirishwa kuelekea nyumbani Tanzania kupitia kampuni la shirika la ndege la Emirates mpaka Dar es Salaam na baadae kusfirishwa kuelekea Killimanjaro kwa mazishi.
Uongozi wa Jumuiya ya wanafunzi waishio Bangalore (TASABA) unatoa shukrani za dhati kwa ubalozi wa Tanzania New Delhi kwa ushirikiano na msaada mkubwa walioutoa ili kufanikisha taratibu zote za kisheria na kutoa usafiri wa kumsafirisha ndugu yetu maarehemu IMRAN MTUI mpaka nyumbani kwao Kilimanjaro. Pia uongozi wa Jumuiya ya wanafunzi waishio Bangalore (TASABA), unatoa shukrani za dhati kwa wale wote walioungana na familia ya ndugu yetu mpendwa marehemu IMRAN MTUI kwa hali na mali.
Jumuiya ya wanafunzi waishio Bangalore (TASABA),unaomba wanajumuiya wote kuwa watulivu na kuacha kutoa habari za kizushi juu ya kifo cha marehemu IMRAN MTUI kwa kuwa uchunguzi zaidi bado unaendelea na mpaka sasa hakuna mtuhumiwa yoyote Yule anaye shutumiwa au kushikiliwa na polisi juu ya kifo hicho.
Uongozi wa wanafunzi waishio Bangalore (TASABA) unatoa pole kwa familia ya marehemu IMRAN MTUI. Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya ndugu yetu mpendwa marehemu IMRAN MTUI. Amin
Fidelis Msomekela
President – TASABA
 
India: Hatumfahamu Mtanzania aliyechinjwa


na Sauli Giliard na Mariam Maregesi


amka2.gif

LICHA ya kuwapo taarifa za kuchinjwa kwa Mtanzania huko India, ubalozi wake nchini umesema haumtambui.
Taarifa zilizothibitishwa na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhandisi John Kijazi, zinasema Imran Mtui (31) aliyekuwa anasoma katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Bangalore alichinjwa na kiwiliwili kukutwa kando ya reli.
Tanzania Daima ilipokwenda jana hadi Ofisi za Ubalozi wa India hapa nchini ili kupata balozi wake alisema: "Sisi hatujui, hatuna habari hizo, wala hatuna la kufanya," alisema balozi huyo huku akikataa kutoa ushirikiano.
Taarifa ambazo zimethibitishwa zinaeleza Mtanzania huyo aliyekuwa nchini India alikuwa anasomea Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA).
Zilieleza kuwa kiwiliwili cha marehemu kilionekana kandokando ya reli katika eneo la Shivajinagar lililopo mjini Bangalore, huku mguu mmoja ukiwa umejeruhiwa vibaya.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema wizara yake inafuatilia suala hilo. Waziri Membe alilazimika kuzungumzia hilo baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari juu ya taarifa za kuwapo mauaji hayo. Waziri Membe ambaye hakutaka kuzungumzia zaidi juu ya tukio hilo alibainisha kwamba serikali inawasiliana na familia ya marehemu kubaini chanzo cha kifo hicho cha kusikitisha.
 
He's one of the coolest people i've ever met,alikuwa mtu fresh sana,pia mpenzi mkubwa sana wa Reggae na culture ya Rastafarianism....Nakumbuka alikuwa akipenda poem za Mutabaruka,aliniambia kuhusu kipande kimoja cha poem hiyo kinachokwenda hivi, "I am da black man coming from da black womb entering in da black world,doing everything in black" ....

That is "I Doh Ave a Color Problem", one of my favourite poems from Mutabaruka. Ironically, the poem ends with the words ..I just had a blackout...

Imran, I feel like I have met you...RIP
 
India: Hatumfahamu Mtanzania aliyechinjwa


na Sauli Giliard na Mariam Maregesi


amka2.gif

LICHA ya kuwapo taarifa za kuchinjwa kwa Mtanzania huko India, ubalozi wake nchini umesema haumtambui.
Taarifa zilizothibitishwa na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhandisi John Kijazi, zinasema Imran Mtui (31) aliyekuwa anasoma katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Bangalore alichinjwa na kiwiliwili kukutwa kando ya reli.
Tanzania Daima ilipokwenda jana hadi Ofisi za Ubalozi wa India hapa nchini ili kupata balozi wake alisema: “Sisi hatujui, hatuna habari hizo, wala hatuna la kufanya,” alisema balozi huyo huku akikataa kutoa ushirikiano.
Taarifa ambazo zimethibitishwa zinaeleza Mtanzania huyo aliyekuwa nchini India alikuwa anasomea Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA).
Zilieleza kuwa kiwiliwili cha marehemu kilionekana kandokando ya reli katika eneo la Shivajinagar lililopo mjini Bangalore, huku mguu mmoja ukiwa umejeruhiwa vibaya.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema wizara yake inafuatilia suala hilo. Waziri Membe alilazimika kuzungumzia hilo baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari juu ya taarifa za kuwapo mauaji hayo. Waziri Membe ambaye hakutaka kuzungumzia zaidi juu ya tukio hilo alibainisha kwamba serikali inawasiliana na familia ya marehemu kubaini chanzo cha kifo hicho cha kusikitisha.

Huyu balozi wa India anaonyesha dharau aina hiyo wakati yuko Tanzania....na uongozi wetu nao umekaa kimya....hii kazi kweli.

Kama hataki ushirikiano na Tanzania....hasa katika masuala kama hayo yanayoihusu nchi yake....Na Afukuzwe nchini.
Kwanini atuvunjie heshima namna hiyo....!!

Well....Lakini inaelekea oungozi wa Tanzania umeona hiyo dharau ni sawa tu.....kwasababu...wamekaa kimya.
Ingekuwa Kenya...wasingekaa kimya....lazima wange fanya kitu....Uongozi wa Tanzania umezubaa na pia viongozi wenyewe ni waoga.

Rest In Peace Imran.
 
Washikaji nimetafuta official report ya kifo chake kutoka kwa polisi india ktika magazetu ya india lakini hazipatikani online... je kuna mtu yeyote ameiona stori hii katika magazeti ya kihindi?

Ningependa kujua wanachokisema wahindi wenyewe
 
Back
Top Bottom