Mwanafunzi anadhalilishwa na vyombo vya habari Serikali na Wanaharakati mko kimya

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,591
38,040
Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, mbali na mambo mengine, inazuia utoaji wa taarifa zinazomuanika mtoto ambazo zinaweza kumletea madhara kisaikolojia, kijamii, au kimahusiano.

Mtoto Esther wa Pandahill Sekondari Mbeya sasa amekuwa kama banda la maonyesho viwanja vya Sabasaba. Ukiyasikiliza maneno anayosema, mengi yanamdhalilisha yeye mwenyewe na wazazi wake. Mtoto anasema amebakwa na mwalimu bwenini na alipotoka akaenda kujipoza kwa Baba Jose mwezi mzima. Serikali inaonekana kuchukulia hili kuwa jambo la kawaida, ingawa ndiyo hiyo hiyo iliyotunga sheria ya Mtoto mwaka 2009 na imekuwa ikiifanyia marekebisho mara kwa mara.

Kesi zote za udhalilishaji kingono kwa watoto siku hizi zinafanyika katika mahakama ya chumba maalum ili kulinda hadhi ya mtoto, na maelezo yao wakati wa upelelezi yanachukuliwa chini ya uangalizi wa mzazi/mlezi au afisa wa ustawi wa jamii. Wahanga wa vitendo vya ukatili wa kingono wanahudumiwa na madaktari maalum katika hospitali ambao wanashughulika na matukio ya ukatili wa kingono (GBV).

Labda wahusika wanaweza kutueleza ni nini kinaendelea nyuma ya sakata la mwanafunzi Esther kiasi cha kushughulikiwa tofauti na watoto wengine. Kwa nini kuna watu wanatendewa ukatili wa kingono lakini hatuoni wakiitishiwa vyombo vya habari kama inavyofanyika kwa Esther? Huyu amewakosea nini mpaka mnamtumia kama tangazo la biashara ya nguo za ndani?
===
Mwanafunzi Esther: Nilitoroka shuleni kwa sababu mwalimu alinibaka

Mwanafunzi kidato cha tano wa Shule ya Sekondari Panda hill, Esther Noah (18) amesema chanzo cha kutoroka shuleni ni kunyanyaswa kingono na mwalimu wa shule hiyo anayejulikana kwa jina la mwalimu Jimmy.
Akizungumza na Habari Digital, Esther amedai mwalimu huyo alikuwa akimtaka kimapenzi na baada ya kumkatalia ndipo alianza kumnyanyasa kwa vipigo, na kisha kumbaka bwenini huku akimziba kwa blanketi ili asitoe sauti za kuomba msaada.

“Tulipotoka kuchukua chakula tukawa tumefika bwenini kwa kuchelewa, tukala chakula kisha mimi nikaenda kuoga, wakati narudi bwenini walimu wakawa wamefukuza watu maana muda ulikuwa umekwisha. Nilipofika mimi nikawa napaka mafuta, ndipo mwalimu [Jimmy] akaingia akawa ananipiga nikamwambia nimechelewa kuchukua chakula, na ndipo akanibaka,” ameeleza.

Ameongeza kuwa kesho yake baada ya kutendewa tukio la ubakaji, wakati wakiendelea na mitihani alizushiwa kuwa ameingia na kitabu kwenye chumba cha mtihani ambacho kilikuwa chini ya dawati lake, na kisha akashambuliwa kwa kipigo na walimu na kuchaniwa mtihani licha ya kujitetea kuwa hakuhusika.
“Ilibidi niende zahanati [ya shule] na baada ya mtihani wa pili kuisha nikaenda kushinda kanisani, nilikuwa nalia sana kwamba kwanini nimetendewa kitendo kile jana yake na leo nasingiziwa? Nikaamua kutoroka shuleni. Niliandika barua nikiwa na hisia kali na maumivu na kwenda kusikojulikana,” amesema.

Aidha, kuhusu kijana muuza mkaa aliyejulikana kwa jina la ‘Baba Jose’ ambaye alimtambulisha kama mke wake kwa mwanamke ambaye Esther alikutwa akiishi nyumbani kwake, mwanafunzi huyo amedai kijana huyo alimpeleka kwa mwanamke huyo ili kumsaidia apate kazi, na baada ya hapo hawakuwahi kuonana tena.
Esther pamoja na familia yake wameiomba Serikali kumchukulia hatua mwalimu huyo ili vitendo vya unyanyasaji na ubakaji unaofanywa na baadhi ya walimu vikomeshwe.
Screenshot_2023-07-02-09-24-23-090_com.twitter.android.jpg
 
Mkuu, minaona tatizo limeanzia kwa wazazi na aina ya malezi aliyo yapata binti.
Kwanza haiwezekani mtoto kama yule awe na maneno magumu kiasi kile na asiwe na haya wala aibu.
Lakini pia haiwezekani mtoto kama yule atoroke shuleni kisha aende kwa baba Jose, badala ya kwenda nyumbani.

Mkuu.... kuna mambo mengine serikali inasingiziwa sana, na hata media zinayafanya haya kwa ajili ya pesa na bila kuangalia madhara na mustakabali wa binti.

By the way, kwanini wazazi wameruhusu mtoto wao kuongea kwenye media...???
 
Mkuu, minaona tatizo limeanzia kwa wazazi.
Uko sahihi, lakini wazazi wasio na uwezo unawajua. Ni rahisi kuvutwa na viongozi wasiojitambua na kumtumia Mtoto kisiasa. Watoto wa viongozi wanafanya madudu mengi lakini hatujawahi kuona wanapelekwa kwenye vyombo vya habari. Mwaka Jana tumeona Mtoto wa Simbachawene anataka kupiga makofi Polisi lakini Hakuna pengine tilipomuona akihojiwa mbali ya kwamba yule ni Mtu mzima. Wao wako mbele kuanika watoto wa wenzao lakini watoto wao wanawaficha.
 
Huyu mtoto na wazazi wake naona wamesahau kuwa kuna maisha baada ya Panda hill. Yawezekana kweli kuna udhalilishaji ambao mtoto amefanyiwa.
Jambo la kufanya mimi nafikiri ilikuwa ni kufuata taratibu za kiafya kwa maana ya vipimo vya daktari (japo hili sioni kama litaleta ushahidi makini kwa vile jambo la udhalilishaji inasemekana limefanyika muda mrefu umepita)
Wangeenda mahakamani tu ili kama kuna ushahidi mwingine uwasaidie. Kama kweli mtoto alidhalilishwa.

Ila hii kila siku kumuanika mtoto kwenye vyombo vya habari ni kumharibia future tu.....ebu niambie ni kijana gani baada ya miaka 6 au 10 atamshika huyu binti mkono ampeleke kwao kuwa "wazazi wangu huyu ndiye binti ninayetaka kumuoa" na familia ikaridhia....inawezekana lakini hili doa wanalikolezea wino mweusi sana kila mara kumpeleka huyu msichana kwenye media.
 
Sio serikali iliyompekeka kwenye hivyo vyombo vya habari.

Muda mwingine hebu tusiiingizie serikali kwenye upuuzi wa wajinga wachache na Mambo yao ya Kipuuzi puuzi.
 
Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 mbali ya Mambo mengine ya ulinzi wa Mtoto inazuia utoaji wa Taarifa zinazomuanika Mtoto zinazoweza kumletea madhara mbeleni kisaikolojia, kijamii au kimahusiano.
Mtoto Esther wa Pandahill Sekondari Mbeya Sasa amekuwa kama Banda la maonyesho viwanja vya Sabasaba. Ukisikiliza anayoongea mengi yanamdhalilisha yeye mwenyewe na wazazi wake. Mtoto anasema amebakwa na Mwalimu bwenini na alipotoka akaenda kujipoza Kwa Baba Jose mwezi mzima. Hili serikali inaliona la kawaida wakati ni serikali hiyo hiyo iliyotunga sheria ya Mtoto 2009 na imekuwa ikiifanyia marekebisho mara Kwa mara kiasi kwamba kesi zote za udhalilishaji kingono Kwa watoto siku hizi zinafanyika chamber court ili kulinda hadhi ya Mtoto na maelezo Yao wakati wa Upelelezi yanachukuliwa chini ya uangalizi wa mzazi/Mlezi au Afisa wa Ustawi wa Jamii. Hospitalini wahanga wanahudumiwa na madaktari maalum wanaoshughulika na matukio ya Ukatili wa kingono (GBV).
Labda wahusika watueleze kuna nini nyuma ya sakata la Mwanafunzi Ester kiasi cha kushughulikiwa tofauti na watoto wengine? Mbona kuna Mabaamedi wanatendekewa ukatili wa kingono lakini hatuoni wakiitishiwa vyombo vya habari watatangaza kama inavyofanyika Kwa Ester? Huyu amewakosea nini mpaka mnamtumia kama tangazo la Biashara ya nguo za ndani?

View attachment 2675914
Kuna Habari zimekaa kiakili zaidi kuliko tukio. Nimatukio yakinadharia kama like la popobawa Zanzibar. Huyu aweza kuwa sio mtoto ila kiumbe toka sayari ya tatu kutupumbaza kwa yake yanaendelea ktk Taifa...... Jicho la Tatu
 
Sio serikali iliyompekeka kwenye hivyo vyombo vya habari.

Muda mwingine hebu tusiiingizie serikali kwenye upuuzi wa wajinga wachache na Mambo yao ya Kipuuzi puuzi.
Mkuu wa mkoa siyo serikali? Aliyekwenda naye siku ya Kwanza alijitambulisha kama RC Mbeya au alikuwa anadanganya?
 
Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 mbali ya Mambo mengine ya ulinzi wa Mtoto inazuia utoaji wa Taarifa zinazomuanika Mtoto zinazoweza kumletea madhara mbeleni kisaikolojia, kijamii au kimahusiano.
Mtoto Esther wa Pandahill Sekondari Mbeya Sasa amekuwa kama Banda la maonyesho viwanja vya Sabasaba. Ukisikiliza anayoongea mengi yanamdhalilisha yeye mwenyewe na wazazi wake. Mtoto anasema amebakwa na Mwalimu bwenini na alipotoka akaenda kujipoza Kwa Baba Jose mwezi mzima. Hili serikali inaliona la kawaida wakati ni serikali hiyo hiyo iliyotunga sheria ya Mtoto 2009 na imekuwa ikiifanyia marekebisho mara Kwa mara kiasi kwamba kesi zote za udhalilishaji kingono Kwa watoto siku hizi zinafanyika chamber court ili kulinda hadhi ya Mtoto na maelezo Yao wakati wa Upelelezi yanachukuliwa chini ya uangalizi wa mzazi/Mlezi au Afisa wa Ustawi wa Jamii. Hospitalini wahanga wanahudumiwa na madaktari maalum wanaoshughulika na matukio ya Ukatili wa kingono (GBV).
Labda wahusika watueleze kuna nini nyuma ya sakata la Mwanafunzi Ester kiasi cha kushughulikiwa tofauti na watoto wengine? Mbona kuna Mabaamedi wanatendekewa ukatili wa kingono lakini hatuoni wakiitishiwa vyombo vya habari watatangaza kama inavyofanyika Kwa Ester? Huyu amewakosea nini mpaka mnamtumia kama tangazo la Biashara ya nguo za ndani?

View attachment 2675914
jambo la kwanza; Huyo ni mwanafunzi na Wala si mtoto bali ni mtu mzima mwanafunzi, sas basi japokuwa ni mwanafunzi ana haki zote za kisheria na kulindwa kama mwanafunzi kama amebakwa ni Halali Shelia zifuatwe maana huyo ni mwanafunzi
Jambo la pili;

japokuwaa ni mwanafunzi Bado anamakosa makubwa kutoloka shule kabla ya kutoa taalifa kwenye UONGOzi WA shule hatimaye yake akaondoka Kwa maamzi yake mwenyew na kwenda kwa baba Jose kimy kimya bila ya kwenda nyumbani Moja Kwa Moja na kutoa taalifa Kwa wazazi ama ndugu zake, kwenye kipengele hiki Nina mashaka na huyu mwanafunzi

Jambo la tatU; serikali yetu iko wapi kukemea waandish WA habali WA michongo kwenda kumuhoji mwanafunzi ilihali alitakiwa ahojiwe na vyombo vya kiselikali Kwa sili na si kuanza kudhalilishana mitandaoni kinyemela hivyo

Mwisho kabisa Niseme malezi si mazuli Kwa upande mtoto

Mwmmmm
 
Back
Top Bottom