Mwanachama wa ACT Wazalendo: Tunawahofia zaidi NCCR Mageuzi bara kuliko Chadema

Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
6,923
8,314
Leo nimekuwa na mazungumzo na kaada wa ACT Wazalendo

Amenifurahisha sana baada ya kuniambia tunawashukuru CCM kwa kuwafutilia mbali hawa mabwana. Anasema walikuwa hawalali wakiwaza namna ya kuifuta chadomo

Amemshukuru sana Comrade Polepole kwa kuisambaratisha Chadema. Anasema wapinzani wao wakuu wanabaki NCCR-Mageuzi kwani ni kama kimezaliwa upya.

Anasema ana uhakika Chadema haiwezi kupata wabunge zaidi ya watatu huku akisema NCCR Mageuzi ndio itakuwa tishio kwao.

Kwa wale vijana wageni kwenye siasa ambao bado wana mihemuko nawajulisha NCCR- Mageuzi ndio chama kikubwa zaidi cha upinzani kuwahi kutokea nchini. Walivuna Wabunge mafuriko hata Mtoto wa Nyerere Baba wa Taifa alikuwa kule.

Ni NCCR pekee imewahi kuwa na wabunge kila kona ya Tanzania.

Yanayotokea Chadema yalishatokea miaka 30 iliyopita kwa vijana waliozaliwa 90 walijue hili waache mihemuko.

Basi kaada huyu wa ACT Wazalendo anasema wana hofu kubwa kwani NCCR Mageuzi ndio itakayounda Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Nimemwacha kwa kumwambia CCM haibakishi jimbo safari hii amekuwa mpole sana,amesema akikosa bara, Zanzibar hawakosi viti hata viwili.

Mimi nawashauri ACT Wazalendo washirikiane na NCCR Mageuzi kuunda kambi ya Upinzani waachane na makanjanja wa siasa Chadema.

Poleni Chadema mmekufa kifo cha aibu mno. NCCR Mageuzi wamewazidi kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini nioge Matusi? Kwanini nipigwe ban? Au unasononeka Chadema inavyojifia kifo cha aibu?
Aisee kwaiyo content yako Ni nini

Kuifuta chadema
Kupata wabunge watatu
Nncr kuwa chama kikuu cha upinzani

Ukiandika Uzi wowote Jf hakikisha unacheza na maudhui yenye kuakisi jamii .... La sivyo Uzi wako utafutwa achilia mbali kuoga ndoo za matusi na ban juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ACT =CUF ,kwa hiyo ungesema kwa Zanzibar ungeeleweka zaidi, CUF japo imejigeuza na kuwa ACT haijawahi kuwa na wabunge wengi Tanganyika licha ya kuongoza kambi Rasimi bungeni.kwa hiyo tusubili muda ndiyo utaongea na WANYONGE watakachoamua kwani wapiga kura wengi hawamo kwenye Maana hata mleta uzi inaonekana hata umri wa kupiga kura hujafikisha,hata kwenye jukwaa hili la JF umeingia jana.
 
Act na cuf ni tofauti

Cuf ni ngangari
ACT =CUF ,kwa hiyo ungesema kwa Zanzibar ungeeleweka zaidi, CUF japo imejigeuza na kuwa ACT haijawahi kuwa na wabunge wengi Tanganyika licha ya kuongoza kambi Rasimi bungeni.kwa hiyo tusubili muda ndiyo utaongea na WANYONGE watakachoamua kwani wapiga kura wengi hawamo kwenye Maana hata mleta uzi inaonekana hata umri wa kupiga kura hujafikisha,hata kwenye jukwaa hili la JF umeingia jana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo nimekuwa na mazungumzo na kaada wa ACT Wazalendo

Amenifurahisha sana baada ya kuniambia tunawashukuru CCM kwa kuwafutilia mbali hawa mabwana. Anasema walikuwa hawalali wakiwaza namna ya kuifuta chadomo

Amemshukuru sana Comrade Polepole kwa kuisambaratisha Chadema. Anasema wapinzani wao wakuu wanabaki NCCR-Mageuzi kwani ni kama kimezaliwa upya.

Anasema ana uhakika Chadema haiwezi kupata wabunge zaidi ya watatu huku akisema NCCR Mageuzi ndio itakuwa tishio kwao.

Kwa wale vijana wageni kwenye siasa ambao bado wana mihemuko nawajulisha NCCR- Mageuzi ndio chama kikubwa zaidi cha upinzani kuwahi kutokea nchini. Walivuna Wabunge mafuriko hata Mtoto wa Nyerere Baba wa Taifa alikuwa kule.

Ni NCCR pekee imewahi kuwa na wabunge kila kona ya Tanzania.

Yanayotokea Chadema yalishatokea miaka 30 iliyopita kwa vijana waliozaliwa 90 walijue hili waache mihemuko.

Basi kaada huyu wa ACT Wazalendo anasema wana hofu kubwa kwani NCCR Mageuzi ndio itakayounda Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Nimemwacha kwa kumwambia CCM haibakishi jimbo safari hii amekuwa mpole sana,amesema akikosa bara, Zanzibar hawakosi viti hata viwili.

Mimi nawashauri ACT Wazalendo washirikiane na NCCR Mageuzi kuunda kambi ya Upinzani waachane na makanjanja wa siasa Chadema.

Poleni Chadema mmekufa kifo cha aibu mno. NCCR Mageuzi wamewazidi kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu mwandiko umekaa kimwitamwita!
 
Back
Top Bottom