Hahahaha...simba makini mpo?Mimi ni Mwanasimba mwenye matarajio ya kuongoza timu , wala sina kolabo yoyote na Yanga , lakini nimesononeka sana kwa huyu shujaa wa timu yenu kumuona mara nyingi akila uswahilini , kama shida ni hela basi alipwe malimbikizo yake , hawa makocha wa yanga na simba wanavumilia mengi sana ambayo wewe huyajui .
Vile analipa mwenyewe basi aachwe aishi maisha yake.Alipiwe na nani ? Analipa mwenyewe tu , tatizo mwambusi ni mgeni D,salaam inawezekana hajui hotel zenye hadhi yake , hata Jamhuri kiweru sijawahi kumuona eneo hilo .
Nimekuona si mara moja ukipata lunch kwenye kihoteli cha wasomali mtaa wa kongo , kariakoo .
Hiki kihoteli kisichokuwa hata na feni achilia mbali a/c si sawa kwa hadhi yako , hakuna haja ya wewe kocha msaidizi wa Yanga afrika kwenda kubanana na wamachinga kwenye foleni ya wali nyama wa 3500 /, pondamali atakupoteza , mbona yeye hali kwa wasomali ?
Ingekuwa simba tusingeshangaa lakini yanga mbona shida hizo hakuna ? Jiangalie mkuu na ikiwezekana jirekebishe .
.....Itaendelea ikibidi .
Aulizwe Hanspope .Hivi simba mmelipa malimbikizo ya mishahara ya wachezaji ya miezi minne mliyokuwa mnadaiwa?
Vipi lile deni la Msoti, au mpo tayari kushuka Daraja....mtukoseshe point sita zetu.?
Lengo ni kuwakumbusha viongozi wa yanga umuhimu wa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake .Sometimes vya kuandika huwa vinaisha nafikiri.Sadly watu wanataka waandike tu hata kama hawana cha kuandika.Ndo unajikuta unaandika hata kocha wa yanga amekula wapi
Hivi ukisikia Mwambusi amewekwa karantini Tandale kwenye kambi ya kipindupindu utajisikiaje ? Kinga ni bora kuliko tiba .Umefuatilia mafanikio yake weee umeona cha ku mkosoa huna
Umeamua kuongelea anapo kula
Duuh!!
Mwacheni ale anapo taka bhanaHivi ukisikia Mwambusi amewekwa karantini Tandale kwenye kambi ya kipindupindu utajisikiaje ? Kinga ni bora kuliko tiba .
Bunju utakuwa umewafananisha uwanja wa Simba haujanza kutumika, ungesema Yanga angalau maana kuna kipindi waliweka kambi yao Bagamoyo.Nilikuwa duka fulani la mpemba maeneo ya Bunju, Dar es Salaam.
Ghafla nikaona basi la Simba SC likisimama na wakashuka wachezaji wakaja dukani kununua Maji ya Kandoro.
Mmoja aliamua kununua maji 6, kaweka kwenye mfuko wa rambo.
Hata hivyo wapo wanaolala huko Mikoche B, Masaki, Mbezi beach, kwenye mazingira magumu sana. Kula mtu anaweza kula popote pale, Mwambusi kula hapo sioni ubaya wake, kulala ndipo penye matatizo ndio maana watu wanafanya kazi Dar usiku wanaenda kulala kwa Moro.Huyu mleta mada ndio wale wanaokula lunch pale samaki samaki samora then usiku anaenda kulala kwake maji matitu..