Mwalimu: TANU iliwakuta na fedha zao tayari

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,922
30,271
JULIUS NYERERE ALISEMA TANU IMEUNDWA IMEWAKUTA NA FEDHA ZAO HAWAKUTAJIRIKA NDANI YA CHAMA

Historia ya wafadhili wa TANU na harakati za kupigaia uhuru wa Tanganyika bado haijaandikwa.

Mwalimu Nyerere katika miaka ya 1970 alipata kusema kuwa kuna watu TANU ilikuwakuta nafedha zao wazalendo kama John Rupia, Paul Bomani, Dossa Aziz, Abdul na Ally Sykes.

Walikuwapo pia wazalendo wengine waliokuwa na uwezo mkubwa wa fedha na fedha hizi walizitoa kusaidia harakati za kupigania uhuru kama Eikael Mbowe.

Nimeweka hapo chini picha za hawa wazalendo.

Picha ya kwanza Paul Bomani na Julius Nyerere, Ally Sykes na Julius Nyerere, Abdul Sykes na Julius Nyerere, John Rupia na Julius Nyerere.

Picha inayofuatia yenye wat wengi wa kwanza kushoto ni Dossa Aziz na nyuma yake aliyesimama ni Abbas Sykes na kutoka kwa Dossa mtu wasita kulia ni Julius Nyerere na picha ya mwisho ni Eikael Mbowe akisalimiana na Julius Nyerere.

Ningependa kuweka historia za wazalendo hawa kwa kifupi kama nilivyowasoma katika Nyaraka za Sykes wengine kama wao wenyewe walivyonihadithia maisha yao.

Paul Bomani nimemkuta katika Nyaraka za Sykes kama President wa TAA Kanda ya Ziwa 1953:

''Uongozi wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Japhet Kirilo UNO kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha za kupeleka msafara mwingine katika UNO kuueleza umoja huo kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao.

Kamati hii ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Saadan Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hiyo.

Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja kamati hii ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga.

Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa, Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote.

Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kusudio hilo.''

(Kutoka: Report ya Lake Province Kwa Kifupi Iliyotolewa na Bwana Abbas K. Sykes).

''Ally Sykes ndiye aliyechora kadi ya TANU na kuchagua rangi na nembo yake. Rangi alizochagua zilikuwa, nyeusi kuwakilisha taifa la Kiafrika na kijani ardhi ya Tanganyika. Mfano wa kadi ya TANU ulitokana na kadi yake ya Tanganyika Legion.

Baada ya kumaliza kuichora ile kadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie.

Kutoka mfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza.'' Aisha ''Daisy'' Sykes anamweleza baba yake Abdul Sykes:

''Nyumbani kwetu milango ilikuwa wazi siku zote kwa wageni.

Hivi ndivyo tulivyokuwa na wageni kutoka kila kabila, uwezo na hali tofauti. Lakini kile ambacho kimeathiri fikra zangu na kubakia na mimi katika kumbukumbu zangu ni kufika pale nyumbani kwa uongozi wa juu wa Waafrika kabla ya uhuru, machifu kutoka makabila mbalimbali ya Tanganyika na viongozi wa vyama vya wazalendo vilivyokuwa ndiyo vinainukia, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi Waafrika katika wa serikali ya kikoloni.

Kutokana na hadhi hii ya baba yangu na umaarufu wake na kule kupenda kukirimu watu, nikawa si mgeni kwa machifu mashuhuri na nikawa nawahudumia walipokuwa mara nyingi wakija nyumbani.

Wageni hawa mashuhuri waliokuwa wakija nyumbani ni pamoja na Mangi Mkuu Thomas Marealle, Machifu Abdiel Shangali, John Maruma kutoka Moshi, Adam Sapi Mkwawa kutoka Iringa, Kidaha Makwaia kutoka Usukuma, Abdallah Fundikira, Harun Lugusha kutoka Tabora, Humbi Ziota kutoka Nzega, Michael Lukumbuzya kutoka Ukerewe na Patrick Kunambi kutoka Morogoro na wengine wengi.''

Dossa Aziz walimpa jina la utani, ''The Bank.''

Hakuna siku mtu atakwenda benki aambiwe kuwa hakuna fedha.

John Rupia yeye haelezeki.

Hapakuwa na Mwafrika tajiri wakati ule wa kumshinda.

Eikaeli Mbowe yeye alitoa nyumba yake Uchaggani kuwa ofisi ya TANU. Sadik Patwa Muasia aliyekuwa na kiwanda cha soda Tanga.

Leo ukienda kwenye restaurant yake Tanga utakuta imepembwa na picha za kupigania uhuru, Patwa akiwa na Mwalimu Nyerere na Makatta Mwinyimtwana mmoja wa matajiri wakubwa Tanga nyakati hizo.

Hawa ndiyo wazalendo waliomzunguka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Iweje leo hatujui historia zao?

1658948665047.png
1658948698531.png
 
Hongera mzee said ... thread nzuri ... Naomba kujua kilichotokea 95 kumhusu Bomani.
 
Hongera mzee said ... thread nzuri ... Naomba kujua kilichotokea 95 kumhusu Bomani.
SMC...
Unakusudia tukio lipi?

Lile la mbunge kumwita kabaila katika Halmashauri Kuu ya CCM Diamonnd Jubilee Bomani alipokuwa anagombea nafasi Kamati Kuu?
 
Mi sikupenda NAMNA NYERERE ambavyo aliwatesa wafadhili wa chama cha TANU !yule mzee Bilali wa Tabora alisimulia KWENYE documentary Moja hi I! disappointed!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani sasa iwe Katiba mpya"!
 
SMC...
Unakusudia tukio lipi?

Lile la mbunge kumwita kabaila katika Halmashauri Kuu ya CCM Diamonnd Jubilee Bomani alipokuwa anagombea nafasi Kamati Kuu?
Ndio ... huku mtaani inasemekana hawa wafadhili wa chama baada ya uhuru kuna waliopitia magumu pia .
 
1659214818927.png


..Mwalimu Nyerere akisalimiana na Mzee Aikaeli Mbowe.

..upande wa kushoto kwa Mwalimu ni Meja Jenerali Silas Mayunga.

..nyuma ya Mwalimu Nyerere, ni mpambe wake Meja Makwaia.
 
Back
Top Bottom