Mwalimu Nyerere, sensa na udini

Anasema: "..hiyo ndiyo Tanzania tuliyokuwa tukiijenga (isiyo ya kidini) sasa watu wanazungumzia udini"

Ina maana ameshindwa kujenga Tanzania isiyo na udini! (the dude is a failure) sasa hao wanaotuambia kuwa tumeachiwa Tanzania na nyerere isiyo na udini wameyatoa wapi maneno haya!

Kiufupi nyerere hafai kuwa ni rejea katika namna ya kuufuta ubaguzi wa kidini.

Halafu anasema serikali haijali dini ya mtu na ni jambo ambalo haliihusu serikali?...huyu alikuwa akiishi dunia gani?
 
anasema: "..hiyo ndiyo tanzania tuliyokuwa tukiijenga (isiyo ya kidini) sasa watu wanazungumzia udini"

ina maana ameshindwa kujenga tanzania isiyo na udini! (the dude is a failure) sasa hao wanaotuambia kuwa tumeachiwa tanzania na nyerere isiyo na udini wameyatoa wapi maneno haya!

Kiufupi nyerere hafai kuwa ni rejea katika namna ya kuufuta ubaguzi wa kidini.

Halafu anasema serikali haijali dini ya mtu na ni jambo ambalo haliihusu serikali?...huyu alikuwa akiishi dunia gani?

una chuki tu na nyerere....udini gani ulikuwepo kipindi chake....?
 
Zamani sio sasa kwakua tumeyaacha ya Nyerere ndio maana kila kitu kinajifunua wazi UDINI Tanzania unatutafuna!! Hii ni laana ya kuona Nyerere hakufanya kitu!
 
una chuki tu na nyerere....udini gani ulikuwepo kipindi chake....?
Kama vile umesahau pale alipomchukua Mchungaji Mushendwa na kumpa nafasi ya juu katika TANU kwa ajili tu ya imani yake kubwa katika Ukristo?!
hili ni moja tu kati ya mengi.
 
Anasema: "..hiyo ndiyo Tanzania tuliyokuwa tukiijenga (isiyo ya kidini) sasa watu wanazungumzia udini"

Ina maana ameshindwa kujenga Tanzania isiyo na udini! (the dude is a failure) sasa hao wanaotuambia kuwa tumeachiwa Tanzania na nyerere isiyo na udini wameyatoa wapi maneno haya!

Kiufupi nyerere hafai kuwa ni rejea katika namna ya kuufuta ubaguzi wa kidini.

Halafu anasema serikali haijali dini ya mtu na ni jambo ambalo haliihusu serikali?...huyu alikuwa akiishi dunia gani?

Inaonye hukuwepo enzi ya nyerere,kwahiyo hufahamu unacho kiongea.
 
Kwanini watanzania tunapenda kuongele maswala ya udini na ukabila?
Kuna maswala mengi ya kimaendeleo ya kuongelea,tubadilike.
 
Anasema: "..hiyo ndiyo Tanzania tuliyokuwa tukiijenga (isiyo ya kidini) sasa watu wanazungumzia udini"

Ina maana ameshindwa kujenga Tanzania isiyo na udini! (the dude is a failure) sasa hao wanaotuambia kuwa tumeachiwa Tanzania na nyerere isiyo na udini wameyatoa wapi maneno haya!

Kiufupi nyerere hafai kuwa ni rejea katika namna ya kuufuta ubaguzi wa kidini.

Halafu anasema serikali haijali dini ya mtu na ni jambo ambalo haliihusu serikali?...huyu alikuwa akiishi dunia gani?

Mhitimu wa Radio Iman na shehe Illunga!
 
Mtu ukiwa na upendeleo huwezi kutoa hukumu ya haki. Waliokuwepo wakati wa utawala wa Nyerere wanaweza kukushuhudia kuwa wakati wa kupata uhuru watu walitaka watambulike kwa udini, ukabila na utajiri wao. Aliweza kulifanyia kazi hilompaka likafifia. Sababu mojawapo ya kutaifisha taasisi za elimu na afya zilizokuwa zinaongozwa na madhebu ya kidini ilikuwa ni kuondoa matabaka ya udini huu tunaouongelea hapa. Hata kama alishindwa (kulingana na baadhi ya mawazo ya wenzetu humu) lakini alijitahidi; kauli na dhamira yake ilikuwa wazi kwa kile alichokuwa anafanya na kuongea! Hakuweza kukaa kimya bila kuchukua hatua ya haraka yalipojitokeza haya; hakuogopa mtu.
 
Mwacheni nyerere apumnzike. Nyie hangaikeni na udini wenu IPO siku mutakuja pata malipo
 
tanzania hakuna udini bali ccm hao.uwezi kuniambia watu waliompiga ulimboka wasipatikane,waliochoma makanisa wasipatikane,waliompiga risasi nae asipatikane,mpaka walete fbi.baadae utasikia uchunguzi umegharimu trilioni kumi usishangae
 
Kwanini watanzania tunapenda kuongele maswala ya udini na ukabila?
Kuna maswala mengi ya kimaendeleo ya kuongelea,tubadilike.

udini na ukabila ndio sera ya ccm kutugawa na kututawala.sasa wanatapatapa.ukumbuki 2000 kwenye uchaguzi tuliambiwa cuf ni chama cha kidini,baadae tukaambiwa chadema ni chama cha ukabila.
 
Huu udini uliopo sasa ni wa upande mmoja tu. namaanisha hivi , kuna upande mmoja ndio una chuki na upande mwingine wakati upande huo unaochukiwa wala hauna muda wa kuwachukia wenzao.
 
Mtu ukiwa na upendeleo huwezi kutoa hukumu ya haki. Waliokuwepo wakati wa utawala wa Nyerere wanaweza kukushuhudia kuwa wakati wa kupata uhuru watu walitaka watambulike kwa udini, ukabila na utajiri wao. Aliweza kulifanyia kazi hilompaka likafifia. Sababu mojawapo ya kutaifisha taasisi za elimu na afya zilizokuwa zinaongozwa na madhebu ya kidini ilikuwa ni kuondoa matabaka ya udini huu tunaouongelea hapa. Hata kama alishindwa (kulingana na baadhi ya mawazo ya wenzetu humu) lakini alijitahidi; kauli na dhamira yake ilikuwa wazi kwa kile alichokuwa anafanya na kuongea! Hakuweza kukaa kimya bila kuchukua hatua ya haraka yalipojitokeza haya; hakuogopa mtu.
MBONA KERO YA VIJANA KURUDIA DARSA LA SABA HAIKUIFANYIA KAZI HARAKA KWA KUJENGA SECONDARI NYINGI? hayo mambo ya kutaifisha shule na kuvunja uchifu hayana nguvu kuliko kuwaelimisha watu wengi kwa mpigo. kwa miaka 40 ya utawala wake na wa mwinyi, kero hiyo ya vijana kurudia darsa la saba haikuwa na maana kwao mpaka alipokuja Kikwete , wewe unafikiria nini? kuna watu walikuwa wanaingia secondari wakiwa na umri wa miaka 24, hii ilikuwa kero kubwa sana na nyerere haikuipa kipaumbere, yeyey alitoa kipaumbere kwa Frelimo, MPLA, matatizo ya burundi,syshell na sauth africa badala ya kuangalia watu wake wasio na ajira wala elimu ya kutosha.
 
Pamoja na kwamba umetoka nje kidogo ya mada ya udini na kuingia kwenye huduma za jamii ni vizuri ukafahamu kuwa Nyerere hakuwa 100% mkamilifu. Alifanya kazi na watu wenye mawazo kama haya walionayo washauri wa Rais wetu. Ikumbukwe kuwa hakuna kipindi kabla na baada ya utawala wa mwalimu Nyerere tanzania ilifikia kiwango cha juu zaidi cha watu wake kujua kusoma na kuandika. Usione elimu kuwa ni kwenda secondary, la hasha; elimu ni zaidi ya kuhitimu. Kulikuwa na vyuo vya maendeleo ya jamii kila wilaya (FDCs) kwa ajili ya kufundisha vijana wahitimu "ujuzi" mbalimbali ambavyo kwa sasa baadhi vinakaliwa na popo tu. Kumbuka ili taifa liendelee linahitaji wasomi wa kada mbalimbali na kadri unavyosoma zaidi idadi ya wataalamu hao inabidi ipungue. Tunatakiwa tuwe na vijana wengi walio na ujuzi katika fani ya ufundi, wengi kiasi katika fani ya ufundi mchundo, na wachache ngazi ya digrii. Jambo jingine ni vizuri kama ulishawahi kutembelea vijiji mbali mbali utakuta miundo mbinu mingi ya maji iliyojengwa miaka ya 70; kipindi hicho maji yalikuwa mengi vijijini si kama leo. Mzee Mwinyi alifanya kazi kubwa sana katika kuimarisha umoja; leo hii unapoona kuwa hawa wazee hawakufanya kitu hakika huwatendei haki. Pamoja na kuwa tunajenga miundo mbinu lakini angalia deni la taifa lilivyokuwa kwa kujenga viwanda vya kuzalisha wajinga mashuleni na vyuoni. Unadhani elimu inayotolewa katika shule za umma ndo tunayoihitaji? Nina wasiwasi kama watoto wako wanasoma katika shule hizi (kama unao); maana yake nini? unajificha kwa nani ili uonekane kuwa unawapatia elimu watoto wa Tanzania? Kwa kawaida, serikali inatakiwa kushitakiwa mahakamani kwa kudanganya kuwa inatoa elimu kwa vijana wakati inawapotezea muda na kuwafanya wajinga. Fikiria kama ni mtoto wako amesoma miaka minne na ametoka hajui kusoma na umetumia gharama kubwa kumsomesha ungejisikiaje? wewe na yule ambaye hakumpeleka mtoto wake secondary nani ana unafuu? Bwana usichokoze majeraha ya elimu kwa wazazi! Kama huna mtoto huwezi kuuona uchungu huu!
 
Mtu ukiwa na upendeleo huwezi kutoa hukumu ya haki. Waliokuwepo wakati wa utawala wa Nyerere wanaweza kukushuhudia kuwa wakati wa kupata uhuru watu walitaka watambulike kwa udini, ukabila na utajiri wao. Aliweza kulifanyia kazi hilompaka likafifia.
Posti kadhaa zilizopita umekumbushwa jinsi alivyomuweka Mchungaji Mushendwa katika moja ya nafasi za juu TANU kwa ajili tu ya Ukristo wake halafu unakuja unaandika maneno kama hayo! ajabu!
 
Wewe uliyesema Nyerere alimpa Mchungaji nafasi ya juu ya TANU,ulijuaje ni udini. Je,alipotaifisha shule za kanisa zilikuwa za dini ama la? Ni vizuri mkatafakari kabla hamjaongea. Nyerere hakuwahi kupendelea dini fulani hata dhehebu lake. Hizo chuki zenu ni uchonganishi tu,hakuna msingi wo wote.
 
Back
Top Bottom