Mzawa Halisi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 637
- 361
Miaka michache kabla ya kifo cha Nyerere, ilianzishwa taasisi iliyoitwa Mwalimu Nyerere Foundation (MNF), taasisi hii iliendelea hata baada ya kifo cha mwalimu ikiwa chini ya uenyekiti wa Salim Ahmed Salim, na mtendaji mkuu Joseph Butiku. Kwa taarifa ambazo nimeshindwa kuzithibitsha, ni kuwa taasisi hii iko chali kiuendashaji hata ilishindwa kulipa wafanyakazi wake mishahara. Na kwa kiasi kikubwa kuanguka kwa taasisi hii kumechangiwa na uzembe na kiburi cha uongozi wa juu ukiongozwa na Bw. Butiku. Inasemekana kuwa wahisani ikiwa ni pamoja na GOT waliokuwa wanaisaidia taasisi hii walishindwa kuendelea kutoa misaada baada ya viongozi wa MNF kuanza kutumia misaada hiyo nje ya malengo yaliyokusudiwa.
Kama kuna member ana taarifa za uhakika juu ya majaaliwa ya taasisi hii naomba anifahamishe.
Kama kuna member ana taarifa za uhakika juu ya majaaliwa ya taasisi hii naomba anifahamishe.