Mwalimu JK Nyerere: An intellectual cannibal?

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Heshima Mkuu!

Professor Ali Mazrui katika moja ya kitabu chake "The African Condition" aliandika Mwl. Nyerere is an "Intellectual Cannibal". Baada ya kusoma context ya matumizi ya maandishi haya nimeshindwa kuelewa alikuwa akimaanisha nini? Tafsiri ya kamusi:

Cannibal - "a person who eats the flesh of other human beings."
na
Intellectual - "having a highly developed intellect: a person with a highly developed intellect".
(Concise Oxford Dictionary-Tenth Edition)

Baada ya kuambatanisha maana za maneno yote mawili, pia nimeshindwa kuelewa what he meant. Kwa kuwa naamini wapo the Great Thinkers ndani ya Jamii forum ambao wana utajiri wa busara katika kupambanua mambo, nimeona ni vyema kuwasilisha uzi huu kwa maana ya kuwekana sawa.

Nawakilisha!
 
Kuna ule msemo wa kiswahili: Nyoka wa Vichwa viwili huuma akivuvia au akipuzia!

Kwa hiyo Cannibal ni kile kichwa kinachouma na Intellectual ni kile kichwa kinachopuzia.

Nadhani ndio maana si rahisi kuweza kuamua kwa mara moja kuwa Nyerere Alifeli au Alifaulu.
 
Mbelwa,

..ungetuletea walau chapter nzima ya Prof.Mazrui mahali alipaondika "Nyerere is .." tungekuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuchangia.
 
Mbelwa,

..ungetuletea walau chapter nzima ya Prof.Mazrui mahali alipaondika "Nyerere is .." tungekuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuchangia.
Good, usijeukakuta hata hakuna sehemu ameandika kitu kama hicho.
 
Leta "context" tukusaidie mawazo, ikiwezekana leta paragraph nzima au kama una link ya humu mtandaoni tuwekee tukasome tuje na mawazo mengine au kama yako kwa kilichokusudiwa. Lakini at the same time, nakiri kusema hii ya leo ni moja ya description nzuri sana kwa Nyerere niliyowahi kuisikia.
 
Most Likely (80% likely) alikuwa anamaanisha moja kati ya mambo haya matatu:
(1) Alikuwa hapendi intellectuals for they posed a threat to his position and thus he somehow made them dissapper either intelectually or physically eg Tuntemeke Sanga
(2) Alikuwa anakula aidea zao kwa kuzifanya zake au kuzizika zisikike wala kutumika eg Edwin Mtei
(3) Both 1 and 2.
 
kuna hii makala inawezal kushade some lights raiamwema.co.tz/twaalika-kifo-kwa-kuua-vuguvugu-la-wasomi... ni ya toleo namba 158 la tarehe 3 novemba 2010 iliyoandikwa naJoseph Mihangwa

......Je, ni kweli Mwalimu alichukia wasomi? Je, ni kweli alikuwa msomi mla nyama ya wasomi [intellectual cannibal]? Wapo waliofikiri hivyo; lakini wapo pia waliokuwa na mawazo tofauti. Mmoja wa wanazuoni waliomwona Mwalimu hivyo kwa hatua alizochukua dhidi ya wanafunzi walioandamana mwaka 1966 ni Profesa Ali Mazrui.

Katika makala yake iitwayo “Tanzaphylia”, iliyochapishwa na Jarida la “Transition” mwaka 1967, Profesa Mazrui alimwelezea Mwalimu kama msomi aliyekosa uvumilivu kwa changamoto za kisomi.
Kitu ambacho yaelekea Profesa Mazrui hakukielewa ni mtazamo wa Nyerere juu ya wajibu na nafasi ya wasomi kwa jamii yake. Kwa hiyo, tuhuma za Mazrui zilimkera Mwalimu, akaamua kujibu mapigo.

Akihutubia jamii ya Chuo Kikuu cha Liberia Februari, 1968 chini ya mada “Msomi Anahitaji Jamii”, kama jibu kwa Profesa Mazrui aliyeshikilia dhana tofauti kwamba “Jamii inahitaji Msomi”, Mwalimu alisema: “Nimetuhumiwa kuwa mimi ni msomi mla nyama ya wasomi. Lakini nasema kwamba ili elimu ya Chuo Kikuu iwe na maana na ikidhi hoja ya kuwepo kwake, lazima wale wanaopata elimu hiyo wajione kuwa ni watumishi wa jamii wenye wajibu mkubwa kwa jamii hiyo, na si kujipatia manufaa, upendeleo au kujiona wao wana haki zaidi kuliko wale wasiokuwa na elimu”.

Ni kweli, tangu uhuru, Mwalimu ndiye aliyekuwa mwamuzi mkuu wa mahitaji ya jamii ya Kitanzania. Alikitumia Chama tawala na Bunge kupitisha na “kuhalalisha” mahitaji hayo chini ya dhana ya uongozi shirikishi.
Na kwa kufanya hivyo, wasomi wengi hawakupata nafasi kubwa ya kuchangia mawazo katika masuala ya kisiasa, uchumi, demokrasia na maendeleo; lakini mawazo na maamuzi yake yalikuwa ya kimantiki
..........
 
Hebu chungulieni makala hii labda kuna concept ya alichouliza mtoa mada japo kwa kunusanusa!

Na Joseph Mihangwa

HATIMAYE wimbi la migomo katika Vyuo vya elimu ya juu nchini limetulia. Chanzo ni kusimamishwa masomo kwa wanafunzi wengi, waliopinga sharti la kuwataka kulipia asilimia 40 ya gharama za masomo, wakidai kuwa walikuwa wakiadhibiwa hivyo kwa sababu tu wao walikuwa watoto wa wazazi masikini.

Wanafunzi hao hawakuona mantiki kwa Serikali kuwasimamisha masomo kwa kosa tu la kuzaliwa katika familia masikini, wakati Serikali imeshindwa kudhibiti matumizi yake makubwa na yasiyo ya lazima; ufisadi uliokithiri, ubinafsishaji na uwekezaji usiojali, huku mikataba mibovu na uporaji wa rasilimali za taifa ukiendelea kulitafuna Taifa. Migomo hii iliashiria migongano ya kitabaka inayoanza kuibuka katika jamii yetu.

Kama ilivyokuwa mgomo wa Oktoba, 1966, ambapo asilimia 90 ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam walifukuzwa kwa kupinga mpango wa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, na Agizo la kukatwa kwa lazima asilimia 60 ya mishahara ya wahitimu na hatimaye wote wakarejeshwa bila masharti, migomo ya sasa inabeba maudhui yale yale na yametafsiriwa na jamii ya wasomi kama "ushindi" kwa kuifanya Serikali itambue jinsi tabaka la walio nacho linavyoweza kushindwa kupora demokrasia na haki za msingi za wanyonge, zikiwamo haki ya elimu kwa wote, kwa mfumo wa sera kandamizi na za kitabaka, kama umma utaungana.

Tofauti na mgomo wa 1966, ambapo baadhi ya Wabunge wenye msimamo makini waliwaunga mkono wanafunzi, katika migomo ya Zanzibari, hakuna Mbunge aliyetoa sauti, isipokuwa Viongozi wachache tu wa vyama vya upinzani wenye jadi ya kupigia kelele karibu kila jambo, walitoa malalamiko yao.

Hata hivyo, Wabunge waliounga mkono mgomo wa 1966 walifukuzwa ubunge na uanachama wa Chama pekee cha Tanganyika African National Union [TANU], licha ya Serikali kutambua mahali ilipoteleza kwa kuwafukuza wanafunzi hao.

Hatua hiyo kali ya Serikali dhidi ya wasomi [1966] iliitwa na mwanazuoni mahiri barani Afrika, Professa Ali Mazrui, akiandikia Jarida "Transition" mwaka 1967, kuwa ni ugonjwa wa Kitanzania [Tanzaphylia] wa kuchukia wasomi, na kwamba Rais Julius Nyerere alikuwa msomi mla nyama ya wasomi [Intellectual cannibal].

Akijibu tuhuma hizo dhidi yake, kwa hotuba aliyoitoa Chuo Kikuu cha Liberia, Februari 1968, juu ya "Msomi anahitaji Jamii", Mwalimu alidakiza kuwa, wasomi wanakuwapo kwa ajili ya Jamii na siyo kinyume chake.

Alisema, wajibu mkubwa wa Msomi katika jamii ni kukidhi mahitaji ya jamii yake ambayo inaundwa pia na wasio na elimu. Msomi anapaswa kumulika njia; ni mshika kurunzi.

Tatizo la mtazamo huu ni kuhusu jinsi msomi huyu anavyoshirikishwa katika kubainisha mahitaji ya jamii yake. Swali linalozuka hapa ni; Nani anayepanga mahitaji ya jamii? Ni watu?. Ni Viongozi?. Viongozi wa aina gani?.

Tunapodai kwamba jamii yetu inatakiwa kujitosheleza kwa wataalamu ili tuweze kuendelea, ni nani anayeweka mfumo wa elimu na masharti ya utoaji elimu hiyo?. Nani anayeweka sera za uchumi?. Kwa manufaa ya nani?.

Je, ni mahitaji ya jamii kujenga matabaka ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, kama inavyotokea sasa?. Je, ni mahitaji ya jamii kwamba wenye nguvu ya pesa ndio washike hatamu za uchumi wa nchi, utawala na siasa?.

Uzoefu umeonyesha kwamba ni Viongozi [wanasiasa] wanaopanga mahitaji ya jamii kupitia bunge lililodhibitiwa na watawala. Tazama jinsi wabunge wasomi wanavyoasi maadili ya taaluma zao kwa kujifanya popo wanapoingia bungeni kwa kuridhia hoja na sera wanazofahamu fika ni za kuangamiza jamii, wakitetea pepo ya tabaka la watawala!

Alvin Toffler, katika kitabu chake "Powershift", anatoa changamoto kwa wasomi kwamba, "kwa kuwa elimu [usomi] ndiyo kisima pekee cha demokrasia na madaraka, basi, wasomi wana wajibu wa kutetea na kulinda uhuru wa mawazo, kukosoa na kufundisha pamoja na kupinga kwa nguvu zote urasimu na ukandamizaji. Wanatakiwa kuepuka utii pofu, kujikomba na nidhamu ya woga".

Naye Profesa Arthur M. Schelesinger Jr, anatukumbusha katika kitabu chake: The Cycles of American History, kwamba, demokrasia haijiendeshi pekee; na kwamba jukumu la kujenga, kulinda na kuimarisha demokrasia na utawala bora haliwezi kuwa la Serikali pekee, vyama vya siasa na "vigogo" wachache wenye nguvu za kiuchumi au kisiasa; bali jamii nzima inapaswa kuwa wakala wa demokrasia na udemokrasishaji. Na kwa sababu hiyo, wasomi wana wajibu mkubwa katika hilo kwa kuwa wao wanazo zana [elimu] na nyenzo za uchambuzi wa jamii na mahitaji yake.

Na katika kufanya hivyo lazima watakumbana na vikwazo vya wasiotaka mabadiliko, na vya wenye kulinda na kutetea maslahi binafsi kwa maangamizi ya jamii. Wafanye nini?.

Msomi hapaswi kuogopa kutetea maslahi ya walio wengi, lazima akubali kuwa mhanga wa mfumo. Socrates [Greece] alikuwa mmoja wa wahanga wa kwanza wa mifumo kandamizi katika kutetea misingi ya demokrasia [L. Housman: The Death of Socrates]. Na karibu na zama zetu, tunakumbushwa na Abraham Lincoln, [1863] kwamba: "Taifa hili, chini ya Mungu, litazaa uhuru mpya; na kwamba Serikali ya watu, iliyo mikononi mwa watu, na kwa ajili ya watu, haitaangamia juu ya nchi".

Ni wajibu wa wasomi kuona kuwa Serikali kama hiyo inazaliwa na kudumu. Lakini nani kama Socrates, miongoni mwa wasomi wetu?.

Katika jukumu hilo, kuna wakati [miaka ya 1967 – 1977] Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam [UDSM] kilijipatia jina na sifa ya kuwa kitovu cha mawazo na fikra za kimapinduzi, uwanja wa harakati na changamoto za kimapinduzi na kimaendeleo, kiasi cha kuonewa wivu na Vyuo Vikuu vingine ndani na nje ya bara la Afrika.
Sifa hizi zilianza kutoweka baada ya 1977 pale wanasiasa [wasio na hoja] walipogeuka "wala nyama ya watu wasomi" [intellectual cannibals], kwa kuwaona eti ni wabishi na kidhibiti mwendo kwa maendeleo ya nchi, ambapo ukweli ni kinyume chake.

Kwa mtazamo wa wanasiasa, maendeleo na umoja wa kitaifa ni kipaumbele kabla ya demokrasia. Matokeo yake yalikuwa ni kuporomoka kwa uchumi kwa kiwango sawa na cha kulewa madaraka kwa watawala.

Hii ilitokana na mfumo wa chama kimoja uliozuia uhuru binafsi wa mawazo juu ya mchakato wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hakutokea "Socrates" msomi wa kuiokoa hali mpaka tumekutwa na sera kandamizi za utandawazi kwa maangamizi yetu.
 

HUYU NDIYE MR. NYERERE NA JELA ZAKE


Katika mwaka 1968 Hakimu Seaton, Hakimu wa Mahakama Kuu; alitembelea gereza la Mwanza.
Nilimuuliza kama kuna uhalali wowote juu ya kuwekwa kwetu kizuizini.

Mkuu wa gereza akamwambia Hakimu kuwa hakuna karatasi zozote zilizoletwa pamoja na mawaziri wa zamani wa Zanzibar.

Hakimu akaahidi kulifuatilia suala hili. Baada ya miaka minne tangu wakati huo, nikiwa katika gereza la Bukoba, Katibu wa Mkuu wa Mkoa alitoa shauri kuwa nimuombe Raisi anitoe kizuizini.

Nalimwambia kuwa kwa vile sijui nini kosa langu la kuwekewa kizuizini naona sina hoja za kimsingi juu ya ombi langu.


Alinijibu, "Hapana shaka ulipotiwa kizuizini ulisomewa amri ya kutiliwa kizuizini."

Nilimwambia kuwa, vile ninavyo kumbuka mimi hapakuwepo amri ya mimi kutiwa kizuizini.
Suprintendent wa magereza akanambia kuwa ilikuwepo amri, hapo akanisomea hio amri ambayo ikionesha kuwa inatokana na Raisi na ambayo imeandikwa kwa lugha ya kisharia.

Amri hio inasema kuwa Raisi baada ya kutoshelezeka kuwa, fulani na fulani; akiwataja mawaziri wote wa Serikali ya Muhammad Shamte, kuwa walikhusika na vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya nchi, alitoa amri tutiwe kizuizini.

Nalipomuuliza amri hio ilitiwa sahihi lini, ilidhihiri ilikuwa ni mwaka wa 1968, baada ya muda mchache tangu pale nionane na yule Jaji Mkuu, Seaton kwenye gereza la Mwanza!


Sisi tulivamiwa nchi yetu na kutiwa vizuizini katika mwaka wa 1964. Najuwa kulikuwa na mapinduzi (mavamizi) huko Zanzibar, na hicho kitendo cha kiharamia iwe kimetokea huko.

Lakini tangu kati ya mwaka wa 1964 pale tulipotiwa vizuizini mpaka hii 1968 ambapo hii amri ya kutiwa kizuizini kutolewa na kutiwa sahihi; wakati huo wote - miaka minne - kuwekwa kwetu kizuizini na yeye Raisi Nyerere ambae ndie aliekuwa na hukumu yote huko Tanzania bara basi hakukuwa kisharia hata katika hio sharia ya kidhalimu ya Tanzania.

Kwa muda wa miaka minne kabla ya kutiwa sahihi hii amri ya kuwekwa vizuizini sisi tulikuwa basi ni wafungwa wake yeye Nyerere.

Je, ndio inayumkinika katika muda huo iwe yeyote miongoni mwetu sisi tuweze kufanya vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya taifa?

Tujaalie kuwa inakusudiwa ule muda kabla ya kukamatwa na kutiwa kizuizini.

Wakati huo sisi tulikuwa ni mawaziri wenye mas-ulia kwa vile tulichaguliwa kulingana na sharia ya kikatiba iliokuwepo nchini - Zanzibar - wakati huo.

Je, sisi wakati huo tutaweza kuwa tutende kama vile ilivyoelezwa katika hio amri iliotiwa sahihi na Julius Nyerere?

Kama itakavyokuwa, hilo taifa linalo elezwa kuwa ni Tanzania; halikuwepo kabla ya sisi kukamatwa na kutiwa vizuizini.

Huyo ndio mkuu wa nchi, anaejigamba kuwa yeye ni mwenye kuweka haqi, anafika kuzuwa na kupanga uwongo kama huo; ni jambo la kushangaza sana; lakini kwa watu kama yeye sio ajabu kulitenda.

Baada ya kupata hoja hizi ndipo nilipomwandikia Raisi, bila shaka maandishi yangu yalikuwa ni ya upole na kweli za hakika.

Sikupata majibu. Kwa hakika sikupata hata mara moja jawabu au hata kuarifiwa kuwa zimefika, baruwa zangu kadhaa wa kadhaa nilizompelekea Nyerere, tangu niko kizuizini na hata baada ya kutoka. Utaritibu wa hishima kama hio Tanzania inaonekana ni mpango wa kikoloni uliokwisha pitwa na wakati.


Dr. Kleru alikuwa ni Mkuu wa Mkoa aliepigwa risasi na mkulima, Abdulla Saidi Mwamindi; siku ya krismasi mwaka 1971. Mkulima huyu, Abdulla Saidi, alikuwa ni miongoni mwa watu kadhaa wa kadhaa walionyang'anywa mashamba yao kwa kuwanzishia vile vijiji vya ujamaa. Jeuri ya Mkuu wa Mkoa huyu ilifurutu ada.

Waliokuwa wakiteswa na kudhulumiwa na Mkuu wa Mkoa huyu walishitaki kwa wakuu wa chama.
Kila wakishitaki huambiwa wakashitaki polisi; na wakifanya hivyo.

Kamanda wa Polisi, Abubakar aliwaonya wakuu huko Dar es Salaam juu ya vitendo viovu na vya kuudhi vya Mkuu wa Mkoa huyu na juu ya ile tabia yake ya ulevi kufika kuanguka na kuingiliwa na wahuni.

Baada ya kupigwa marisasi na kuuliwa, wale jamaa wote waliokuwa wakipeleka mashtaka yao Polisi walikamatwa na kuwekwa kizuizini mpaka Abdulla Saidi Mwamindi ahukumiwe na kunyongwa. Hata kabla ya kesi kumalizika, magazeti na vyombo vyote vya khabari vya Serikali na vya Chama, vyote vilianza shutuma zao, sio tu dhidi ya Mwamindi, bali dhidi ya wakulima wote, huku wakisemwa, "mabepari", "wanyonyaji", "wakoloni" na makhaini".

Mudhahara uliopangwa na Sirikali ukaingia njiani kupita kuwashutumu na kuwalaani watu hawa. Kwa hali hii ikawa Mwamindi kesha hukumiwa na vibaraka vya Sirikali hata kabla ya kufikishwa mahakamani.

Mashahidi wote wale ambao wangeliweza kutowa ushahidi japo kuthibitisha juu ya vitendo vya uchokozi vya yule Mkuu wa Mkoa walizuiliwa mpaka pale kesi kumalizika.

Khatuwa hii ilikusudiwa kumtia khofu yeyote yule aliekuwa na fikra ya kutaka kutowa ushahidi upande wa mshitakiwa.

Hivi ndivyo sharia inavyo firigiswa katika nchi kama hivi Tanzania wakati ambapo sharia ya kumtia mtu kizuizini bila ya kupelekwa mahakama inatumika.

Watu kumi na mbili wa Iringa pamoja na yeye Mwamindi mwenyewe walikuwa pamoja na mimi gerezani Dodoma.
Kamanda wa Polisi Abubakar, na yeye vilevile aliwekwa na sisi siku mbili gerezani akiwa yumo katika pirika za kuhamishwa kutoka gereza hii na kupelekwa gereza jengine.


Ilani nyingi zilitolewa na kutangazwa ulimwenguni juu ya maafa na mateso katika magereza ya Zanzibar na Pemba.

Lakini hapana lililosemwa na kuelezwa walimwengu kukhusu mateso yanayowapata wazuiwa katika magereza ya Tanzania bara.

Sio kuwa uwovu na mateso wanayotendewa wazuiwa magerezani huko Tanzania bara hayajuulikani; mengi yake hayafiki ulimwenguni basi kwa sababu ya kukosekana demokrasia na heshima ya haki za binadamu juu ya haki ya kueleza na kujieleza.

Kutokana na hali hii, mateso na vitendo vya kikhabithi havielezwi nje kwa walimwengu kukhofia hao watakaoeleza kuadhibiwa na utawala wa kidikteta. Niliona kwa macho yangu nilipokuwa gereza la Mwanza, wakati ambapo Superintendent Odenyo ndie aliekuwa mkuu wa gereza wakati huo; niliona wafungwa walipozuiliwa chakula na maji kwa muda wa siku nne, kisha wakapelekwa hospitali (nusu maiti) na ripoti kuwa (ati) walikuwa wamegoma kula.

Nilipokuwa Dodoma nilikuwa nikisikia kadhia kama hizo.
Nikisikia, kwani baina yetu ilikuwa ni kuta, baina ya chumba niliokuwemo na vile vyumba vya mateso.

Katika gereza la Dodoma aliekuwa katili hivyo ni Ofisa Mkuu, aliepangwa jina "Iron Face" (Uso wa Chuma), kwa vile akijuulika kuwa hajapata kuwa na huruma.

Mkuu wa magereza hapa, alifika kuwa hajishughulishi tena na kazi yake; hivi ni kwa sababu kwa hichi cheo chake cha juu na daima kuwemo katika vikao na sherehe za kisiyasa, takribani alimuachilia uendeshaji wote wa gereza mikononi mwa msaidizi wake - huyu Ofisa Mkuu. Mabwana wawili hawa waliyafanya maisha ya gerezani hapa hayastahamiliki hata kidogo.


Ile mikutano ya kawaida ya kila Jumamosi ambapo ofisa mas-uli hutarajiwa asikilize malalamiko ya wafungwa ikawa haifanywi tena.

Ziara za kila mwezi gerezani za Mahakimu mbalimbali nazo pia zikasita. Wafungwa hutiwa gerezani na kufika kutolewa bila ya kujuwa kuwa wanahaki ya kuwasiliana na watu wao.

Inafaa ifahamike kuwa hivi kuharibika hali kiwango hichi, sio tu katika gereza la Dodoma. Niliiona hali kama hiyo katika gereza la Mwanza.

Gereza la Bukoba ilikuwa haijambo pale nilipoondoka.
Lakini, wakuu wa kisiasa; kama vile Mkuu wa Mkoa na Mawaziri dhahiri shaahir walikuwa wakijiepusha kuyazuru magereza na kujuwa hali za wafungwa na wazuiwa waliomo humo magerezani.

Ama Raisi na Makamu wa Raisi, si dhani kama iko siku wamewahi kuzuru gereza lolote lile katika Tanzania bara, licha kuzungumza na mabwana au mabibi waliowatia humo magerezani.

Hali katika gereza la Dodoma ilizidi kufanywa kuwa mbaya kwa ukhabithi wa huyu "Uso wa Chuma" na kulemaa kwa ulevi wa marungi Msaidizi wa Superintendent.


Mpango ulifanywa kumuuwa "Uso wa Chuma". Mmoja wa wafungwa aliweza kupata kisu na akataka kumpiga nacho huyo "Uso wa Chuma", kwa bahati akaanguka kifudifudi, kichwa chake mbali na yule mfungwa ambae alikuwa na pingu za chuma miguuni mwake na yeye vilevile akaanguka upande wake.

Wakati huo mfungwa aliweza basi kuipata miguu ya "Uso wa Chuma" na kuanza kumpiga visu vya miguuni mpaka pale ilipowezekana kuzidiwa nguvu akanyang'anywa hicho kisu.

Hapo tena akaingiliwa mfungwa huyo kupigwa marungu mpaka akawahijiwezi ndipo alipotiwa pingu za mikono. Askari wa gereza akaamrishwa kumpiga marisasi ya miguu.

Hivyo ikawa kafungwa kila upande na marisasi miguuni mwake, hapo tena akasukumizwa katika chumba cha adhabu.
Baadae kidogo msaidizi wa superintendent akaja na yeye akaanza kumpiga vile alivyopenda.

Vilio vyake tukivisikia kutokea katika hicho chumba cha adhabu alimokuwemo na tukamuona askari aliekuwa zamu kwenye kidungu akigeuza uso na kupiga ukelele: "Wanamuuwa huyu mtu!" Binadamu huyu akavurumishwa tena humo chumbani kisha bomu la kutowa machozi likatupwa katika hicho chumba ambacho sehemu yake ya kupitia upepo ni ndogo kabisa. Usiku uleule akajifia.


Asubuhi yake wafungwa wote wakasimamishwa kwenye uwanja na maiti ikaletwa mbele yao uchi kama alivyozaliwa. Hapo tena msaidizi wa superintendent akawa anamchocha maiti kwa gongo huku akimwambia yule maiti: "Inuka uwaambie wenzio vipi ulivyokuwa hodari, na nini mwisho wa uhodari wako?"

Baada ya hivyo tena akawahutubia wafungwa kwa kuwaambia kuwa hivihivi ndivyo tutakavyomfanya yeyote yule miongoni mwenu asiposhika adabu yake.
Hapo tena wafungwa wote wakafungiwa vyumbani mwao kisha mabomu ya kutowa machozi yakatupwa humo vyumbani mwao.

Haya yalifanywa kwa makusudio ya kuwataka watajane wale waliokhusika na mpango huu. Haukupita muda isipokuwa wengi wakatajana na kukiri makosa yao.

Lakini adhabu na mateso yaliendelea kwa wiki kadhaa wa kadhaa. Chakula kikapunguzwa, hata kwetu sisi wazuiwa. Kila mtu alitaraji mauwaji haya yatafanyiwa uchunguzi na hukumu ya haki kupitishwa. Askari wa gereza ikawa wanasema hadharani kuwa ukifanywa uchunguzi watawaambia askari Polisi hakika ya mambo ilivyo. Lakini hapana lilokuwa.

Tulisikia katika redio, kama maneno ya kupita tu yaliosemwa Bungeni - kwa woga - na mmoja wa Wabunge kuwa kulikuwa na askari makhabithi walio waadhibisha wafungwa mpaka kufika kuwauwa.

Kubwa lililotokea ni uhamisho wa kawaida wa maofisa wa magereza wa vyeo vya juu kutoka magereza mbali mbali nchini. Khabari ikamalizikia hapo.

Katika nchi yenye sheria ya kutiwa watu vizuizini bila ya kupelekwa mahakamani, kelele zozote zile ni sawa na mbwa mwenye kubweka hazina athari yoyote ile, na sharia basi ni kwa kumtumikia bwana mtawala aendelee katika utawala wake na atende vile anavyopenda.

 
Back
Top Bottom