Mwalimu Afukuzwa Kazi Kwa Kunyonyana Ndimi na Mwanafunzi Wake

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18




Mwalimu wa shule moja ya msingi nchini Australia amefungiwa kufanya kazi ya ualimu kwa miaka mitano baada ya kufumaniwa akinyonyana ndimi na mwanafunzi wake wa kike mwenye umri wa miaka 12.

Mwalimu mmoja wa shule ya msingi katika jimbo la Queensland nchini Australia amefungiwa kufanya kazi ya ualimu kwa muda wa miaka mitano baada ya kukamatwa akinyonyana ndimi na mwanafunzi wake wa kike mwenye umri wa miaka 12.

Kamati ya nidhamu ya walimu ya jimbo la Queensland ilimuona mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 26 [jina kapuni] ana hatia ya kujaribu kuwavuta kimapenzi wanafunzi wake wawili wa darasa la saba.

Aliwasiliana na mwanafunzi mmoja wiki chache kabla ya kumaliza shule na alimtumia meseji nyingi za kimapenzi kwenye ukurasa wake katika tovuti ya MySpace.

Mwalimu huyo alifumaniwa na wanafunzi wawili akinyonyana ndimi na mwanafunzi wake huyo mwenye umri mdogo ndani ya mazingira ya shule.

Ingawa polisi walijaribu kuichunguza kesi hiyo, waliamua kuitupilia mbali baada ya msichana aliyenyonyana ndimi na mwalimu huyo kukataa kushirikiana na polisi kwenye upelelezi wao.

Kamati ya nidhamu ya walimu ya mji huo ilisema kwamba uhusiano kati ya mwalimu huyo na mwanafunzi wake ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kwamba mmoja wa wanafunzi wake alisema walikuwa kama wapenzi.

"Kunyonyana ndimi na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 12 na kutumia tovuti za My Space na Facebook kuendeleza uhusiano na wanafunzi ni kukiuka misingi ya ualimu na kwa kufanya hivyo amedhirisha kuwa hafai kusajiliwa kama mwalimu", alisema mwenyekiti wa kamati hiyo Lisa O'Neill.

Hata hivyo mwalimu huyo aliendelea kukanusha kuwa na uhusiano na mwanafunzi wake.

 
Huyo Mwalimu ni bradhuli!
Kama ni mnyOnyaji wa ndimi akawanyonye wanae huko kwake!
Wa kwangu humnyonyi aisee,... nakunyonya macho!
 
Back
Top Bottom