Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Fina Lyimo, Rombo
MWALIMU wa Shule ya Msingi ya Kwamaksau iliyopo Useri, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro anatuhumiwa kuwalawiti wanafunzi sita wa kiume kwa nyakati tofauti baada ya kuwarubuni kwa kutumia vishawishi mbalimbali.
Vishawishi hivyo ni pamoja na kuwapa fedha, kuwatafutia ada na wengine akiwapa chakula kingi cha mchana wawapo shuleni.Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Absolom Mwakyoma alisema uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha kuwa kitendo wanachodaiwa kufanyiwa wanafunzi hao si kulawitiwa bali kushikwashikwa korodani zao.
Tusiwe wepesi wa kuwalaumu polisi bila kuwa na uhakika na kile tunachowalaumu nacho, mimi nimefika mwenyewe shuleni hapo na nimezungumza na daktari aliyewafanyia uchunguzi na vipimo havionyeshi waliingiliwa, alisema.
Mwakyoma alifafanua kuwa tuhuma kuwa kila mara mtuhumiwa huyo anapofikishwa polisi huachiwa si sahihi kwani amekuwa akifikishwa mahakamani na anapopewa dhamana na mahakama, wananchi wanadhani ni uamuzi ya polisi.
Mzazi wa mmoja wa mtoto wanaodaiwa kulawitiwa alidai mtoto wake ambaye yuko darasa la saba shuleni hapo alifika nyumbani na kumweleza kuwa mwalimu alimpa Sh500 na kumwingiza stoo na kumfanyia kitendo hicho.
Mzazi huyo, alidai mtoto wake alikuwa na rafiki yake ambapo wote walipewa Sh500 kwa ajili ya kufanyiwa kitendo hicho na kuwa mwalimu huyo alipomaliza kumfanyia mmoja alimchukua mwingine na kuanza kumfanyia.
Mtoto wangu alikuja nyumbani akiwa anachechemea huku akiwa hawezi kutembea vizuri na nilipomuuliza ndio akaanza kunielezea kilichomtokea na nikampeleka hospitali Ngoyoni ambapo alilazwe siku mbili kwa kuwa alikuwa amevimba sehemu za siri, alidai baba huyo.
Aidha alidai hali ya mtoto huyo bado ni mbaya kwa kuwa bado ana maumivu makali, ambayo yamesababishwa na kuvimba kwa sehemu za siri kutokana na kufanyiwa kitendo hicho kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa mzazi huyo alidai kuwa mwalimu huyo aliwachukua wanafunzi wawili na kuwafanyia kitendo hicho kwa kuwapa kiasi cha Sh1,000 wote wawili na kwamba mtoto wake hali yake ni mbaya lakini mwenzeke anaendelea vizuri.
Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya hiyo, Peter Toima alithibitisha kuripotiwa kwa matukio hayo na kwamba tukio hilo lilitokea Julai 27 mwaka huu ambapo mwalimu huyo alilawiti watoto wawili kwa wakati mmoja.
Toima alisema kuwa mwalimu huyu alilawiti tena watoto wengi wawili mwezi Mei na wengine mwezi Aprili mwaka huu.
Mkuu huyo alisema kitendo hicho kilisababisha wakazi wa eneo hilo kuandamana na kufika shuleni hapo ili kwa lengo la kutaka kumchoma moto ila polisi waliwahi na kumwokoa na kuweza kumpeleka katika kituo cha polisi.
Hili ni jambo la kusikitisha kwa kuwa mwalimu huyo amekuwa akihamishwa hamishwa shule kutokana na kitendo cha kulawiti watoto wa shule na huwa anawafanyia watoto wa madarasa mbalimbali, alisema Toima
Alisema wazazi hao waliandamana shuleni hapo Agosti 2, kwa lengo la kutaka kumchoma moto mwalimu huyo ila polisi waliwahi na kumwokoa mwalimu huyo na kwamba mwalimu anashikiliwa na polisi .
Toima alizitaja shule za msingi ambazo mwalimu huyo amewahi kufundisha na kudaiwa kufanya matukio hayo kwa wanafunzi kuwa ni ni shule ya msingi Kimwingeni, Kiserini, Keni Mengeni na Ubetu.
Mkuu huyo alisema mwalimu huyo akiwa anafundisha shule ya msingi alimlawiti mtoto mmoja ambaye alijulikana ambapo alikunywa sumu baada ya kufanyiwa kitendo hicho na mwalimu huyo na hivi sasa ni marehemu.
Wazazi wa watoto hao wameiomba Serikali kumchukulia hatua kali mwalimu huyo na hata ikiwezekana kufukuzwa kazi hiyo kwa kuwa hafundishi bali anawaharibu watoto.
Chanzo:Gazeti la Mwananchi